Wolper: Ufundi cherehani unalipa kuliko kucheza filamu

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
STAA wa filamu za Bongo, Jacqueline Wolper, ameibuka na kudai kwamba ufundi cherehani ndiyo unaomlipa zaidi kuliko filamu alizowahi kucheza.


Kutokana na kauli hiyo, mwigizaji huyo ambaye kwa sasa ni mjasiriamali anayekua kwa kasi, ameweka wazi mpango wake wa kuanza kuwashonea nguo watu maarufu ndani na nje ya Tanzania ili aingie kwa nguvu kwenye orodha ya wabunifu wenye majina makubwa duniani kote.


Licha ya madai hayo, Wolper alisema anaiheshimu sanaa kwa kuwa ndiyo iliyomtambulisha kwa jamii na kumwezesha kufanya shughuli zake nyingine kwa urahisi, lakini baada ya kuingia katika ushonaji wa nguo za mitindo mbalimbali, anaona inalipa zaidi ya filamu.


“Sikuwahi kufikiria kama ufundi cherahani unaweza kuwa na pesa hasa ukiwa mbunifu mzuri wa mitindo ya nguo, kwa sasa nategemea zaidi kazi hii kuliko uigizaji na kutokana na hilo nitafanya filamu chache tu kwa mwaka ili akili yangu kubwa nielekeze kwenye biashara ya ushonaji,” alisema Wolper.

Chanzo: Mtanzania
 
Hatafanikiwa katika ufundi cherehani labda iwe ufundi nguo/ushonaji.

Hivi hadi anafikia uamuzi huo na bado hajui tofauti ya ufundi cherehani na ufundi nguo!!,haya safari njema kwa uamuzi wake huo wa kuanza kutengeneza charehani mbovu.
 
Weka picha akiwa anashona...

Sent from my Diamond Crypto using JamiiForums mobile app
 
Hawa hawana akili, wamezungushana na dealers wa cd wakishirikiana na Bashite leo kila mmoja kapiga kimya.
 
Hata bongo flava nayo hailipi.

Sent from my SM-G950F using JamiiForums mobile app
 
Kesho diamond, omy dimpoz, ali kiba na sheta watasema kukata mauno kunalipa, wanamkatia nani mauno sisi hatujui wakate na kushonana tuu liwalo na liwe waiiii
 
Atafanikiwa kama ataacha kudesign nguo kama alizovaa aunt Ezekiel harusini ya prof Jay.

Sent from my E5306 using JamiiForums mobile app
 
Reactions: THT
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…