"Woooo! Mke wangu kasema"

"Woooo! Mke wangu kasema"

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Eti! "Woooo! Mke wangu kasema"😀😀😀😀

Yule wa pili akasema, "juha ni mimi, jana nilikwenda sokoni nikanunua nyama, na mchele, na nazi, na bizari na kunipia nikaja nikampa mke wangu akapika akaisha. Na mji huu una amri ikifika saa nne milango hufungwa, lakini ikifika sa nne kama hukufunga mlango hukamatwa ukalazwa korokoroni, asubuhi huzungushwa mji mzima kisha hupelekwa kuchinjwa.

Basi nyumbani petu tumekaa hata ikapita saa nne bado hatujafunga mlango, wala chakula hakijapakuliwa.

Nikamwambia mke wangu, Pakua chakula! Akapakua akaisha akaweka juu ya meza, tukitaka kula nikamwambia mke wangu Tusile, nchi hii ina amri na wewe unaijua, basi kafunge mlango kwanza ndiyo tuje tule; mke wangu akaniambia, 'Kafunge wewe,' nikamwambia, Kafunge wewe, akaniambia, 'Kafunge wewe.'

Nikamwambia mke wangu, Hatuna haja ya kubishana, basi na tukae hivi hivi tu, na chakula tusile, atakayekula, na akafunge mlango, na atakaye sema, na akafunge miango.

Basi tukakaa mimi na mke wangu kimya tukatazamana tu. Tukakaa hata akaja punda mle nyumbani, akala mtama hata ukaisha, punda akatoka, hapana asemaye, atakayesema na akafunge mlango. Akaja mbwa akaingia nyumbani, akaramba vyombo vyote akaja pale mezani akala ule wali wote, sahani akazivunja akaenda zake, hapana asemaye kama Mbwa amekula wali wote,

Atakayesema na akafunge mlango. Tukakaa hata saa saba. akaja askari, akatuuliza, 'sababu gani hamkufunga mlango?'

Tusiseme, tukanyamaza askari akatuchua akatupeleka korokoroni hata asubuhi tukapelekwa kwa Sultani. Sultani akasema, 'Wazungusheni mji mzima kisha mkawachinje.' Mimi na mke wangu tukazungushwa mji mzima hatusemi, hata tulipofika karibu na nyumba yetu, mke wangu akasema, 'Mume wangu, si ile nyumba yetu mbona twaipita?' Mimi nikamzomea mke wangu, Woooo! Mke wangu amesema, Eeeeee Woooo! Mke wangu amesema!'

Yule askari akasema, 'Ah! Watu hawa wana ninii? Sultani ameniambia niwazungushe, nikifika pwani niwachinje, sasa wanasema hivi! watu hawa nitawarudisha kwa Sultani.' Askari akaturudisha, akamweleza Sultani, Sultani akatuuliza, nasi tukamjibu, akatupa ruhusa tukarudi kwetu nyumbani.

Je, Waonaje? Wali wangu, mke wangu, nyumba yangu ikitaka kuniua, Je! Bwana mimi si Juha?'''

Akamwambia, "wewe ni Juha zaidi ya yule wa kwanza."
 
Ahsante kwa muongozo mkuu, wana Uzalendo mkubwa wa kukaa kimya kisa kuogopa matokeo ya kusema
 
Back
Top Bottom