Working as a content/chat moderator in Tanzania

mafolebaraka

New Member
Joined
Aug 10, 2021
Posts
1
Reaction score
5
Ushawahi kusikia watu wanaolipwa kwa kutazama na kureview maudhui ya mtandaoni? Ushawahi kutamani kupata kazi ya aina hiyo?. Je vipi kuhusu faida na hasara zake? shuka nayo

Mapema mwishoni mwa mwaka jana nilipata kazi kwenye moja ya jukwaa la freelancing ninalolitumia kwa kipindi kirefu.Wakati kazi inapostiwa sikuwa interested nayo sana kuiomba sababu kuu hadi wakati naenda kuomba zaidi ya watu 15 walikuwa wameomba.

Bahati mbaya kazi hii ilijitokeza sana kwenye profile yangu to extent nikavutiwa zaidi kuiomba. Kazi hii ilipostiwa na client kutoka Netherland na alikuwa anataka content moderator anayefahamu kiswahili.

Kitu ambacho sikuwa nafahamu ni kuwa huyu client alikuwa anahitaji mtu mwenye sifa kama za kwangu na kati ya watu wote aliowainterview, ilibidi awainterview kwa njia ya Zoom.

Kufanya story hii kuwa fupi sitoenda deep kwenye vitu gani zaidi tulizungumza na huyo client but mwisho wa siku alinipa hiyo kazi. Ni moja ya client walionilipa hela nyingi zaidi na malipo mengi tulifanyia nje ya jukwaa.Unaweza ona pesa alinilipa kwa kazi tulifanya kupitia Upwork.

Naweza kusema hii ndio nilikuwa introduced na kazi ya content moderation.

Disclaimer: Baadhi ya maudhui kwenye makala hii hayatowafaa watu walio chini ya miaka 18 pamoja na watu wenye misimamo mikali ya kiimani na kimaadili.Tafadhali unaweza kukwepa kusoma andiko hili ama ku unsubscribe newsletter hii.

Tafadhali soma Disclaimer hapo juu kabla hujaendelea kusoma

Kitu cha pili nimekitaja kwenye kichwa cha makala hii ni Chat moderators .Chat moderators ni kundi la watu ambalo sio maarufu sana kwenye nchi zetu hizi za kiafrika.

Kwa wenzetu upweke na msongo wa mawazo ni moja kati ya matatizo ambayo yanawasumbua watu wengi hali inayopelekea watu kujinyonga na kufanya maamuzi mengine yasiyofaa.

Moja ya sababu kuu inayosababisha watu kuchukua maaamuzi hayo magumu ni kutokana na kukosa watu wa kuzungumza nao.

Wafanyabiashara wa mtandaoni baada ya kugundua tatizo hilo imebidi wabuni njia ambayo watawasaidia watu hao kupata watu wa kuzungumza nao pamoja na wao kujiingizia kipato.

Hilo ndo chimbuko ya kuanza kwa majukwaa ya kutafuta chat moderators.Tushuke nayo taratibu

Kiasi gani wanalipwa hawa watu?

content moderators na chat moderators wanalipwa kuanzia 1 usd hadi 30 usd kwa lisaa kulingana na aina ya platform, client na ulipopatia kazi.

Mara nyingi content moderator na chat moderator wanaoishi Africa wanalipwa kidogo kulinganisha na wanaofanya kazi kwenye mabara mengine hususani ulaya.

Wapi naweza kupata kazi hizi?

Kuna sehemu nyingi sana za kupata aina hii ya kazi

  • Freelancing platforms: Ingawa kazi hizi sio nyingi kwenye majukwaa ya freelancing lakini kuna fursa ya wewe kupata hizi kazi kwenye majukwaa ya freelancing.Majukwaa ya freelancing yenye hizi kazi ni pamoja na Upwork na Fiverr.
  • Google: Kazi hizi zinatangazwa sana Google chamsingi uwe unajua keyword za kutafuta, ukisearch neno Looking for online chatters utaona kazi nyingi sana zinazotangazwa.
  • Marketplace: Kuna masoko mengi sana yanayotafuta watu wa aina hii, moja ya marketplace ni pamoja na Cloudworkers.
Dark side ya hii kazi

Nimefanya research kidogo ya hizi kazi na haya ni moja ya mapungufu nimeona

  • Malipo kiduchu: Majukwaa haya mara nyingi yanalipa kidogo kwa wafanyakazi hususani kwa wafanyakazi wanaotokea Afrika hivyo ni jukumu lako kupanga bei inayoweza kukunufaisha.
  • Erotic content: Kazi hizi mara nyingi utakutana na maudhui ama filamu za ngono, hivyo ni muhimu kusoma vigezo na masharti ya kazi husika. Moja ya content moderator nimewahi msikia akidai moja ya kazi walipewa ni kureview maudhui ya Necrophilia { kwa kiswahili ni maudhui yanayoonyesha watu wakifanya mapenzi na maiti}
  • Satanic content: Kuna wakati utakutana na maudhui ya jumuiya za kishetani kama freemason nk. Hivyo kama aina hiyo ya maudhui yanaweza kukuathiri kiimani huna budi kuachana na hizi kazi.
 
Bado unaendelea na hiyo kazi au ilikua temporary ikaisha na muda.
 
Vipi hiyo kazi mtu akiifanya with his or her all efforts anawezs Ku- earn I million per month?
 
Back
Top Bottom