Workshop #02; Kahama Real Estate Workshop Namba 1

Workshop #02; Kahama Real Estate Workshop Namba 1

Aliko Musa

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
209
Reaction score
315
Tutakayojifunza:
flyerdesign_08112023_122122.png


(a) Lengo kuu la programu.

(b) Shabaha/Fokasi ya programu ya leo.

(c) Ufafanuzi wa Fokasi ya programu.

(d) Sababu za uwepo wa fursa kwa kila taarifa.

(e) Dondoo muhimu kuhusu vibanda.

Utangulizi.

Taarifa zimejazwa na Aliko Musa. Hii ni baada ya kukosekana mwanachama yeyote kujaza taarifa za REAL ESTATE WORKSHOP katika wilaya au mkoa husika. Nakukaribisha ujaze taarifa ili tuweze kufanya programu ya aina hii kutoka katika wilaya unayopendekezwa nayo. Karibu sana rafiki yangu.

(a) Lengo Kuu La Programu.

Lengo kuu la programu ni kujifunza kwa undani zaidi kuhusu soko mahalia (local real estate markets). Mafanikio makubwa sana kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo hutegemea ufahamu wa soko mahalia.

Soko mahalia hubadilika kila mara. Ndiyo, sababu mwekezaji anatakiwa kufokasi kwenye wilaya anayowekeza kwa miaka miwili hadi mitatu ya mwanzo wa uwekezaji wake.

Muda maalumu wa kufokasi unategemea na njia anayotumia mwekezaji kujiingizia kipato au faida kupitia uwekezaji wa ardhi na majengo.

Moja, unahitaji kubobea kwenye eneo moja kwa miaka kadhaa kama ilivyo tajwa hapo. Mbili, unahitaji timu bora yenye ushirikiano wa wazi kwenye kujifunza soko la eneo (wilaya au kata unapowekeza.

Wiki hii ya Tarehe 12/11/2023, ninakuletea taarifa za soko la uwekezaji kwenye ardhi na majengo katika wilaya ya KAHAMA. KAHAMA iliyopo Mkoani Shinyanga, Tanzania.

(b) Shabaha/Fokasi ya Kahama Real Estate Workshop.

Hii ni programu ya kwanza kuifanya kwa halmashauri ya Kahama, Shinyanga Tanzania. Fokasi kuu ya programu ni KUMILIKI ARDHI KWA MUDA MREFU (LAND BANKING).

Kumiliki ardhi/benki ya ardhi (landbanking ) ni njia ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo ambayo huhusisha kununua kipande kikubwa cha ardhi kwa lengo la kulifanyia maendelezo siku zijazo.

Ni njia bora sana sana kwa ajili ya kutunza utajiri kuliko kumiliki nyumba za kupangisha. Hii ni kwa sababu ardhi za aina hii hupanda thamani kwa zaidi ya 100% kwa kila mwaka kwenye miji yenye hali nzuri ya masoko ya ardhi na majengo.

Mji wa Kahama ni moja ya miji ambayo hili linaweza kutokea hata baada ya miaka 10 ijayo. Uwekezano wa ardhi yako unayomiliki pale Kahama kupanda kwa 100% kwa mwaka ni mkubwa sana.

Hii ina maana kuwa, ardhi ambayo utainunua mwaka huu (2023) kwa Tshs.5,000,000. Baada ya miaka 10 itakuwa inauzwa kwa zaidi ya Tshs.50,000,000 (itakuwa inauzwa milioni 50 kutoka milioni 5). Kanuni hii inakuwa ni kweli, endapo utamiliki ardhi kwa miaka 10 au zaidi.

Unatakiwa kumiliki angalau ekari moja. Hii itaongeza uwekezano kupata manufaa makubwa zaidi kwenye uwekezaji wako.

(c) Ufafanuzi Wa Umiliki Wa Ardhi (Land Banking).

Ardhi hupanda thamani kutegemea na mambo makuu manne (4):

✓ Nguvu ya kisiasa (political forces).

✓ Nguvu ya kijamii (social forces).

✓ Nguvu ya kiuchumi (Economic forces).

✓ Nguvu ya miundombinu (Physical forces).

Miundombinu Yenye Athari Chanya Kahama Mji.

Moja.

Barabara.

Wilaya ya kahama ina barabara ya kiwango cha lami. Ina barabara nyingi zinazo unganisha na sehemu tofauti tofauti za nchi. Hivyo, kutoa usafiri wa uhakika:

✓ Kutoka Kahama kwenda Tabora.

✓ Kutoka Kahama kwenda Shy Gali.

✓ Kutoka Kahama kwenda Ushirombo.

✓ Kutoka Kahama kwenda Halmshauri ya Ushetu.

✓ Kutoka Kahama kwenda halmashauri ya Msalala.

✓ Kutoka Kahama kwenye Tinde, Masumbwe, Lunze, Kagongwa, Isaka, Kakola na kadhalika.

Pia, Kahama ina kituo kizuri cha kuegesha malori (Nyihogo) kwenda Burundi, Rwanda Na Uganda. Hii inakuwa fursa kwenye uwekezaji wa nyumba za wageni.

Mbili.

Bandari ya nchi kavu (Bandari kavu).

Kahama ina bandari kavu katika eneo la Isaka. Bandari kavu hii husaidia kupunguza gharama za usafirishaji wa mizigo. Pia, hupunguza muda wa kusafarisha mizigo. Bandari kavu hurahisisha usafiri wa mizigo:

✓ Kati ya Kahama na nchi ya Rwanda.

✓ Kati ya Kahama na nchi ya Uganda.

✓ Kati ya Kahama na nchi ya Sudani Kusini.

✓ Kati ya Kahama na nchi ya Burundi.

✓ Kati ya Kahama na nchi ya Democratic Republic Of The Congo.

Tatu.

Uwanja wa Ndege wa Buzwagi.

Nne.

Reli ya mwendo kasi kutoka Mwanza hadi Isaka (Kahama).

Matawi Ya Benki Yaliyopo Kahama.

Moja ya kitu kilichonishangaza na kuvutiwa sana na mji huu ni uwepo huduma za kifedha. Benki zinazopatikana Kahama:

(01) Benki ya NMB (Matawi mawili).

✓ Namba za eneo ni 5HCW+Q9F na 5J93+3HR.

(02) Benki ya CRDB (Matawi wawili).

✓ Namba za maeneo ni 4QG6+97P na 5HCW+X9J.

(03) Benki ya AZANIA (Matawi mawili).

✓ Namba ya eneo ni 5H6V+XGG.

(04) Benki ya Standard Chartered (mtaa wa Kakola).

(05) Benki ya ACCESS (AMBT, Access Microfinance Bank Tanzania).

✓ Namba ya eneo ni 5HCX+MX7.

(06) Benki ya EQUITY (Barabara ya isaka).

(07) Benki ya NBC (Mtaa wa Lumelezi).

(08) Benki ya TCP (Tanzania Commercial Bank)

✓ Namba ya eneo ni 5T93+VRP.

✓ Barabara ya mama Farida.

(09) Benki Ya Afrika (BOA).

✓ Namba ya eneo ni 5HFW+3HR.

✓ Mtaa wa Igalilimi.

(10) Finca Microfinance Bank.

✓ Namba ya eneo ni 5JC2+9G4.

(11) Diamond Trust Bank (DTB).

✓ Namba ya eneo ni 5HCX+Q6C.

(12) DiTarck GPS Technology.

Kahama ina masoko mawili ya kisasa, ina stendi mbili. Kahama ni sehemu ambayo wafanyibiashara wa mikoa ifuatayo hutembelea kuangalia bidhaa na huduma mbalimbali:

✓ Wafanyabishara wa mkoa wa Tabora.

✓ Wafanyabishara wa mkoa wa Geita.

✓ Wafanyabishara wa Kigoma.

✓ Wafanyabishara wa Shinyanga.

(e) Dondoo Muhimu Kuhusu Umiliki Wa Ardhi (Landbank).

Moja.

Ardhi yako itakuwa na bei mara 10 ndani ya miaka 10 ijayo.

Ardhi yako unayoenda kuinunua kwenye mji wa Kahama itapanda thamani kwa zaidi 1,000% kwa miaka 10 ijayo. Hivyo, bei ya sasa ya ardhi yako itakuwa mara 10 baada ya miaka 10 ijayo.

Mbili.

Hati ya umiliki wa ardhi kutoka wizarani.

Endapo umepanga kutumia njia hii (land bank) kutunza fedha au kuongeza fedha ni lazima uwe na hati ya ardhi kutoka wizarani. Huu sio ushauri ni lazima. Ni kigezo mojawapo cha uwekezaji kwa njia ya umiliki wa ardhi kwa miaka mingi (landbanking).

Tatu.

Uangalizi wa karibu wa ardhi yako.

Baada ya kuwa na umiliki wa ardhi na una hati kutoka wizarani. Unachotakiwa ni kuwa na uangalizi wa karibu. Au unaweza kuwa na mtu wa karibu na eneo ardhi ilipo. Ikiwezekana kodisha kwa ajili ya matunzo yafuatayo:

✓ Kodisha kwa wafanyabishara wa kuni na mbao kama ardhi ipo mjini.

✓ Kodisha kwa wakulima wa mbogamboga hasa kwa majiji kama Dodoma.

✓ Kodisha kwa wakulima wa mazao ya biashara kama alizeti,

✓ Egesha mabanda ya biashara kaa wafanyabishara wadogo.

Nne.

Mtandao unaohitaji kuwa nao.

Kipengele hiki ni muhimu sana endapo unategemea kununua na kuuza viwanja na mashamba. Orodha ya watu hawa ni muhimu sana:

✓ Mahusiano mazuri na ofisi ya mipango miji na vijiji.

✓ Mahusiano mazuri na ofisi za mawakili wabobevu kwenye ardhi na nyumba.

✓ Washauri wabobevu kwenye uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

✓ Madalali wa viwanja, mashamba na majengo ya eneo husika.

Hawa watakuwa ni sehemu ya watu wako wanaoweza kukusaidia kutengeneza fedha kupitia kununua na kuuza viwanja.

Tano.

Historia ya umiliki wa ardhi husika.

Ninategemea utakuwa ununua ardhi ambayo haina hati ya umiliki wa ardhi kutoka wizarani. Hivyo, ni muhimu sana kudadisi kwa undani historia ya umiliki wa ardhi unayotaka kuwekeza katika mji wa Kahama. Baadhi ya historia muhimu ni:

✓ Ardhi iliyokuwa inatumika kwa shughuli za ujamaa.

✓ Ardhi ambayo ina historia ya kumilikiwa na chama tawala.

✓ Ardhi ambayo ina historia ya kutengwa kama Hifadhi ya Taifa.

✓ Ardhi ambayo ina historia ya kutumika kwa matumizi ya kanisa au msikiti (ikiwa haina hati kutoka wizarani).

✓ Ardhi ambayo ina historia ya kumilikiwa na kijiji lakini hakuna uhakika wa uwepo wa nakala yoyote.

Hizi ni sababu ambazo zinaweza kupelekea migogoro ya ardhi ikiwa haupo makini. Sababu hizi hazipewi uzito na wawekezaji wengi. Ndiyo, sababu nimekushirikisha hapa wewe rafiki yangu.

Thamani ya ardhi hupanda kwa sababu kuu 2. Nazo ni;

✓ Mabadiliko ya hali ya masoko yasiyotegemea juhudi, maarifa na usimamizi wa mwekezaji husika.

✓ Mabadiliko ya thamani ya ardhi yatokanayo na juhudi za kiusimamizi za mwekezaji husika.

Katika uwekezaji kwenye ardhi, ni muhimu sana kuzingatia sababu namba 1. Sababu namba 2 inakuwa matokeo makubwa sana sana pale ambapo sababu namba 1 imehusika kuongeza thamani ya ardhi.

Njia 10 Za Kuongeza Thamani Ya Ardhi.

Moja.

Kukifanya kifikike kwa urahisi.

Ardhi inayofikika inakuwa na thamani kubwa sana ukilinganisha na ardhi isiyofikika kwa urahisi. Ardhi inatakiwa kufikika kwa usafiri wa miguu ya watu, magari, pikipiki, baiskeli, ndege, na kadhalika.

Vilevile ardhi ambayo hufikiwa na usafiri wa kisasa kama vile usafiri wa ndege au barabara za kiwango cha lami huwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo hufikiwa na usafiri wa baiskeli tu.

Ardhi ambayo ipo katikati ya mtaa ambapo gari, bajaji haviwezi kufika kwa urahisi inakuwa na thamani ndogo ukilinganisha na ardhi ambayo ipo mtaa mzuri ambayo inafikika kwa urahisi na usafiri wa magari na bajaji.

Kuongeza au kuboresha geti kwenye ardhi yako huongeza thamani ya ardhi yako ukilinganisha na ardhi ambayo haina geti ya aina yoyote. Kuongeza au kuboresha daraja sehemu ambapo haipitiki vizuri pia huongeza thamani ya ardhi yako.

Ardhi ya Kahama inafikika na nchi zifuatazo:

✓ Burundi.

✓ Uganda.

✓ Rwanda.

Pia, ardhi ya Kahama inafikika na wilaya mbalimbali kutoka mikoa ifuatayo:

✓ Geita.

✓ Tabora.

✓ Kigoma.

✓ Shinyanga.

Mbili.

Kuweka/Kuboresha huduma za jamii kama vile maji, umeme, mfumo wa taka, n.k.

Ardhi ambayo ina huduma za kijamii huwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo haijafikiwa na huduma kama vile umeme, maji, miundombinu ya usafiri (barabara na viwanja vya ndege) na mfumo wa takataka laini na taka ngumu.

Tatu.

Kupima ardhi yako (land survey).

Ardhi iliyopimwa inakuwa na thamani kubwa sana ukilinganisha na ardhi ambayo haijapimwa. Upimaji wa pamoja wa ardhi unakuwa wa gharama nafuu sana ukilinganisha na upimaji wa ardhi kwa mtu mmoja mmoja.

Kitendo cha kupima ardhi kwa gharama nafuu ni sababu nyingine muhimu sana ya kuufanya uwekezaji wa ardhi yako uwe na matunda mazuri sana.

Nne.

Kuweka uzio (fence) kuzunguka ardhi yako.

Ardhi yenye uzio inakuwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo haina uzio kwa sababu zifuatazo;-

✓ Faragha kubwa kwenye ardhi yenye uzio.

✓ Ulinzi na salama mkubwa kwenye ardhi yenye uzio.

✓ Utulivu wa shughuli za maendeleo ikiwemo kilimo na ufugaji kwenye ardhi yenye uzio.

Ardhi yenye uzio mbovu na mbaya kwa wengi inakuwa na thamani ndogo ukilinganisha na ardhi yenye uzo6wa kisiasa, uzio imara na uzio wenye mvuto kwa wengi.

Tano.

Miliki au nunua haki za umiliki wa madini, gesi na mafuta.

Kwa sheria ya nchi nyingi sana ikiwemo Tanzania, umiliki wa madini, gesi na mafuta unakuwa chini ya serikali. Hii ina maana kuwa endapo mafuta, gesi na madini vitaonekana kwenye ardhi yako ambayo una hati ya hakimiliki, bado utakuwa huna umiliki wa malighafi hizi ni mpaka uwe na kibali maalumu.

Ardhi ambayo ina hati ya umiliki wa mafuta, gesi na madini inakuwa na thamani kubwa sana ukilinganisha na ardhi ambayo ina hati ya kawaida kutoka wizara husika.

Sita.

Panda miti au mazao yenye thamani kubwa.

Katika kila eneo kuna mazao ya chakula/biashara (hasa mazao ya kudumu) ambayo yanaongeza thamani ya ardhi. Panda mazao ya aina hiyo, na ardhi yako itaongezeka thamani yake maradufu.

Matunda ya machungwa yanaweza kukuletea pesa kama walivyofanya eneo la Mgodi wa Buzwagi hapa Kahama. Katani ni moja zao lenye kuliangazia kwa kuwakodishia wakulima wa zao hilo la katani.

Saba.

Kuwa na mpango kutoka halmashauri.

Ardhi ambayo inaeleweka mipango yake kutoka halmshauri na wizara ya ardhi inakuwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo bado haijapangiwa matumizi yake.

Baada ya kuwa na mipango hiyo, kisha ardhi inatakiwa kupimwa. Baada ya kupimwa unatakiwa kuwa na kibali cha ujenzi. Kibali cha ujenzi kinatakiwa kuombewa kwa kutumia ramani ya nyumba inayolipa sana.

Kwa Kuzingatia haya ardhi yako itakuwa na thamani kubwa ukilinganisha na ardhi ambayo haina mipango kutoka halmshauri na wizara mpaka mwekezaji mmoja mmoja.

Nane.

Kuondoa takataka za vimiminika, gesi na taka ngumu.

Ardhi ambayo imekuwa ni sehemu ya kuhifahia takataka inakuwa na thamani ndogo sana ukilinganisha na ardhi ambayo ni safi na salama kwa ajili ya makazi au biashara za watu.

Tisa.

Badili matumizi ya ardhi yako.

Ardhi ya matumizi ya makazi inakuwa na thamani ndogo ukilinganisha na ardhi ya matumizi ya makazi na biashara. Ardhi ya makazi na biashara inakuwa na thamani ndogo ukilinganisha na ardhi ya biashara tu.

Kumi.

Njia Nyingine Za Kuongeza Thamani Ya Ardhi.

Njia za kuongeza thamani ya ardhi zinaweza kuwa tofauti kulingana na mahitaji na mazingira husika. Njia hizo ni kama ifuatavyo:

✓ Kupima vipimo wa udongo.

✓ Kutumia ardhi kwa shughuli za mifugo yenye tija kama vile ufugaji wa kisasa wa samaki, kuku, ng'ombe na mbuzi wa nyama.

✓ Kuwekea mifereji ya kupitishia maji kipindi cha mafuriko au mvua za masika.

✓ Kusaini mkataba wa zaidi ya miaka 5 wa ukodishaji wa ardhi yako.

✓ Kupanda, kuboresha au kutunza bustani ya ardhi yako.

✓ Kujenga nyumba, kiwanda cha matofali, na kadhalika.

Programu hii limeandaliwa na mbobezi majengo Aliko Musa. Karibu ujiunge na kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM (TRT) upate masomo ya haya BURE. Waalike jamaa zako wako nao wapate maarifa haya. Asanteni sana.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

MUHIMU; Jiunge na kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM. Ukiwa hapa utapata masomo na mijadala kuhusu uwekezaji kwenye ardhi na majengo (real estate investment).

Nitumie ujumbe usemao "WORKSHOP"...

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom