World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

ktk mapopoma ndio anaonelana bora,angalia timu za amerika nyingi anavyokuwa hafurukuti hadi anapandwa na hasira,hata angekuwepo jana asingefanya chochote,thiago silva ndio pengo kubwa sana jana maana ukiangalia walikuwa kichochoro sana jana brazil beki,ujerumani wanafurahi kiboko yao Spain na Italy zimetoka
 
PSG wana hasara kwani central defenders wao ni bure kabisa Luiz, Silva

ni soka lolote laweza tokea...vip kipigo cha man u kwa city, arsenal kwa man u, bayern alikula 4 na madrid ambapo ndo german yenyewe na spain alivyopigwa 5 je wacheaji wa hizi timu ni magarasa!?
 
ni soka lolote laweza tokea...vip kipigo cha man u kwa city, arsenal kwa man u, bayern alikula 4 na madrid ambapo ndo german yenyewe na spain alivyopigwa 5 je wacheaji wa hizi timu ni magarasa!?

Ndo mpira huo ukizubaa unapigwa nyingi
 

Wewe una ugomvi binafsi na dogo.unanikera hadi najisikia kurudi bonde kidogo labda tutaelewana.kila siku wasungia kideo,kuguuta kote kule nkhuzati kumwona mgosi Neymar?yaani mbilinge zoote zile huzioni?
 

mbona jana ukakimbia tena ?
 
Nimeshawapiga chini hao everlenk, nisingependa kuona kombe linaenda masafa marefu. Si unajua hapa jinsi tunavyoswitch allegiance kila kukicha lol!!! Kama WC Final itakuwa kati ya Germany na Netherlands basi ni bora Waholanzi wachukue.

Aisee!!! tuwatakie kila la heri,leo wadachi umepiga chini?
 
Last edited by a moderator:

Hivi unafahamu forwardline isipomiliki mpira defence inakuwa na mzigo mara mbili?sasa jumlisha hilo na style ya Brazil ambao hulinda goli kwa kushambulia,inapotokea hawawezi kushambulia,basi na kulinda pia inakuwa hivyo.hii zahma ya jana iliwakuta na France,Ronaldo akiwemo,forwardline ilikufa,balaa likawakuta kutoka kwa Zizzou and co kule nyuma.ilikuwa hivi hivi,kasoro tu jana defence yao ilikuwa mbovu kupitiliza na magoli yakawa mengi,lakini ukitazama,tatizo kuu lilikuwa kumanage mfumo wa kupeleka attacks,mbele walishindwa,wakawa frustrated na goli la mapema.hivi Neymar awekwe na akina Fred,hulk na vile vimeo vyao unategemea nini?brazil ilikufa ilipochaguliwa,hata Neymar hawezi kuiokoa,hata Messi au De lima wangewekwa na kikosi hiki wasingebadili matokeo.Neymar mnamuonea bure jamani!
 
Dah!!!! Shukrani kwa kuyasikia maombi ya wadau hapa na kuyafanyia kazi, ungechukua maamuzi haya kabla ya mechi ya jana basi labda tungekuwa tunaongea mengine lol!!! 🙂🙂

kwa sasa sina, timu yeyote atakayechukua kombe kati ya walioingia hatua hii poa tu.
 
Uko sahihi ndg..Neymar ni classic sana na hata Oscar mzur pia tatizo lililopo ni beki haikuwa makini katika kukaba hasa beki za pembeni na dante..

Vile vile ukiangali mtu kama T.silva alikua akimsaidia marcelo pale anapopanda na kuziba pengo lake lakini jana hakukua na mtu mwenye akili kama hivo, luise ni mzuri lakini mpaka aambiwe wewe cheza hivi na T.silva ndio aliokua akimchezesha luise. Nahisi ujerumani wametumia vilivo mapengo yaliyokuwepo ndio sababu ya ile mvua
 
PSG wana hasara kwani central defenders wao ni bure kabisa Luiz, Silva

Game ya jana sio Luiz tu wakulaumiwa timu nzima ilichemsha, magoli 2 yametoka kwa Fernandinho kanyanganywa mpira mara mbili na Kroos na Khedira ndio maana Scolari alimtoa half time,2 kwa Marcelo then Luiz na Dante.David Luiz alishindwa kuiongoza na kuipanga timu kama nahodha,Marcelo na Luiz walikuwa wanapanda wanajisahau kurudi kukaba
Willian alipaswa kuanza nafasi ya Neymar.Fred hata Taifa Stars hawezi pata namba
,Brazil hii ilikuwa average sana tactics za kocha ndio zilipaswa kuwabeba but nae akachemka.Holland wana timu average but tactics za kocha zimewabeba
 
Nimeshawapiga chini hao everlenk, nisingependa kuona kombe linaenda masafa marefu. Si unajua hapa jinsi tunavyoswitch allegiance kila kukicha lol!!! Kama WC Final itakuwa kati ya Germany na Netherlands basi ni bora Waholanzi wachukue.

Hmmm....hapo tutakuwa pande kinzani. Kama Wadachi wakipita leo basi aacha tu Majerumani yachukue. Siwapendi kabisa mimi hao Wadachi.

Na licha ya Wajerumani kuleta maumivu jana (ingawa nadhani maumivu yalikuwa self-inflicted na Brasi wenyewe) siwezi kabisa ku-root kwa Wadachi.

Na kwa jinsi ninavyoona tayari hayo Majerumani yameshaleta hofu kwa yeyote yule atakaye cheza nayo hiyo Jumapili. Ushindi wa jana umeathiri saikolojia za wengi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…