World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Mechi za leo kweli ni kali.Ukiacha hii ya Brazil na Chile iliyoisha muda si mrefu Brazili katokea tundu la Sindano.Colombia ingawa hawajawahi kuchukua kombe hili tokea michuano hii kuanza hapo 1930 inaonekana kujaribu bahati yake dhidi ya Uruguay ambayo ilikwisha lichukua kombe hili mara mbili, mwaka 1930 kombe hili lilipoanza na mwaka 1950.

Leo hii wewe UNATABIRI nani awezaye kuibuka MSHINDI katika MECHI HII kati ya Uruguay na Colombia.
piga kura kwa kubofia hapa.:hail:
 
Kesho nitakuwa kwa Netherlands nataka wakutana ne Brazil huko mbele walipize machungu ya 2010

Kesho timu zote zangu japo moja inalazimika kudondoka ila nitakuwa mexico kwa ajili ya kukutia presha, jipange vizuri.
 
Haya mlioko live hebu tupieni updates mkizingatia dk na magoli kwa kila timu na ikiwezekana na vitukio vya hapa na pale kama labda kuna mtu katysoniwa mguu, mkono, sikio ama kiungo chochote.

Dak ya 23 bilabila na mpira upo kawaida tu ngoja tuendelee kuwacheki.
 
Kesho timu zote zangu japo moja inalazimika kudondoka ila nitakuwa mexico kwa ajili ya kukutia presha, jipange vizuri.

Duh mkuu kesho nitawahi kula sana ili isije nitokea hali ya leo hadi njaa imeisha na chakula kimepoa
 
hivi huyu bwana mdogo cuardado wa colombia anacheza ligi gani na timu gani wakuu?
 
Dak ya 23 bilabila na mpira upo kawaida tu ngoja tuendelee kuwacheki.

Vipi hakuna aliyenyofolewa japo ngozi? Maana timu mojawapo nasikia ina mafundi wa kushughulika na minofu ya watu achilia mbali kucheza kandanda.
 
Cuadrado yuko kwenye sayari ya akina Messi na C Ronaldo
 
Hamna visingizio, kesho dunia haitaamin Uholanzi wakila kichapo, tena kichapo chembamba 1-0. Amin usiamin Uholanz kesho analala kwa Mexico.

Hata mimi napenda watolewe
 
mexico hamna timu hapo..

Sawa, hamna team, lakini dunia haitaamini kitakachotokea. Kumbuka katika stage hii kila team iko determined. Hatuangalii historia! Kesho Uholanzi anakula kichapo chepesi: 1-0, 2-1 au 3-2!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…