Nimewasikiliza sana lakini nimevumilia nimeshindwa. Watangazaji mnaopiga porojo (uchambuzi) wakati mpira unachezwa katika matangazo yenu ya Redio mnakera, sisi tunaotembea na redio mkononi mnatukera muda mrefu mnaujadili mchezo,
mpaka mnajisahau. Wanaotazama TV watakubaliana nami kwamba hata kwenye TV wakati mpira unachezwa uchambuzi ni sehemu kidogo sana. Kama mtapata salamu hizi badilikeni elezeni mpira msijadili mpira.