World Cup 2014, Brazil: June 12 - July 13

Wapi nitapata ratiba za mechi kwa kutumia muwa wa East Africa? I mean GMT+3

Angalia kwa huyo mdau

Costa Rica wanajitahidi kutia presha katika lango la uruguay
 
Kweli mkuu sio kma ile waliyopwa spain na brazil zilikuwa za kimagumashi

Kama ile ya Spain ilikua ni ya laana ndio maana wakashushiwa mvua ya magoli, wakati mwingine maamuzi ya Refa yanaharubu ladha ya mpira.
 
Costa rica ni mdhaifu sana, yaani kama nimasuala ya vyama basi ni uruguay (CCM) vs Costa rica (ukawa)......... wanaboa mno bora nilale nisubiri mechi ya maana
 
Costarica watulie tu uwezo wa kupata bao wanao.
 
Arsenal wana talent kibao, huyu Campbell mzuri sana. Tatizo Wenger anaangalia wafaransa zaidi ..
 
Costa rica ni mdhaifu sana, yaani kama nimasuala ya vyama basi ni uruguay (CCM) vs Costa rica (ukawa)......... wanaboa mno bora nilale nisubiri mechi ya maana

Usituharibie jukwaa kwa siasa zako uchwara.
 
Reactions: BAK
Costa rica ni mdhaifu sana, yaani kama nimasuala ya vyama basi ni uruguay (CCM) vs Costa rica (ukawa)......... wanaboa mno bora nilale nisubiri mechi ya maana
Yaani wewe jamaa bila siasa inaonekana huishi kwa amani, hebu nenda kule siasani bhana usituharibie uzi wetu....
 
Wanaombagua ni baadhi ya wataliano(wapuuzi) katika jamii ya wataliano lakini si wote.

Hizo nchi ulizozitaja ukiacha Portugal na Belgium (kwa uelewa wangu) zilizobaki zina kesi nyingi tu za ubaguzi, lakini hatuwezi kusema waingereza wabaguzi kwa sababu tu John Terry alimbagua Antony Ferdinand, hatuwezi kuwatilia maanani wapuuzi wachache na kuyafanya mawazo yao yawe ya jamii nzima.

Swala la Balotelli kuvaa tu jezi ya Azzuri inaonesha kwa kiasi gani Wataliano kama jamii wameanza kuushinda ubaguzi, wana hadi mbunge mwanamke mweusi huko Italia, kwa hiyo tusiruhusu mawazo ya wapuuzi wachache watufanye tuuone ulimwengu in black and white.
 
Italy vs England ni saa sita kamili?????? Nijuze fasta kabla sijalala please
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…