Inabidi uelewe kipimo wanachotumia hawa waandishi wengi ni irrelevant kwa Tanzania.Watanzania walio wengi wanaishi vijijini.a hawaihitaji pesa kununua chakula sababu wanalima for consumption.
Kwahio ishu ya food security labda kwa maskini wa mjini.Ambao na uhakika ukiwachukua hawawezi zidi hata 25% ya watanzania.
Things are very different for Kenya. Most of you need money to buy food.
Sent using
Jamii Forums mobile app
Na hata huko maashambani sio kila mtu ni mkulima.
Anyway kuhusu hio sentensi yako ya "Things are very different for Kenya. Most of you need money to buy food." Hili ni jambo hua nishawahi kujaribu kuelezea watanzania wenzako mara nyingi sana bila kufanyikiwa,labda wewe mmoja wao unaweza kujaribu.
Ukiskia Turkana kuna njaa na mtu amekufa, usianze kucheka eti Kenya hakuna chakula, Chakula kiko! hata kama kimeagiziwa kutoka nje, kiko na kinapatikana madukani, shida ni kwamba kuna maskini ambao hawawezi kununua hichi chakula cha madukani. Hawa maskini hua wanategemea mifugo au kupanda chakula (wakitegemea mvua) ili kupata lishe. Mvua ikikosekana basi hakuna nyasi za kufuga mifugo na hakuna maji ya kupanda chakula.
Kuna sehemu zengine Kenya huenda hata miaka mitatu au miine bila mvua kuonekana! Kama we ni maskini na unaishi huku!!! itafika wakati ukose la kula kabisa, na akwavile hauna uwezo wa kununua chochote basi utabaki kupunga upepo chini ya mti!!!
Asilimia 70 ya Kenya ni kame u inakaribia kua kame, Tofauti na Tanzania ambapo yule maskini hohe hahe ambaye hana uwezo wa kununua chakula bado anaweza kufuga mifugo au kupanda chakula akitumia maji ya mvua.
Lakini kwa upande mwengine,, sababu kubwa kwanini hauioni Kenya ikiwa mbele ya Tanzania kwa njaa hapo kwa World Hunger Index ni kwavile Wakenya wengi wanahamia kuishi kwenye maeneo yaliyo na rotuba, huko sehemu karme utapata ni watu wachache.
Yani kulingana na takwimu, 70% ya wakenya wanaishi ndani ya 30% ya ardhi. Au ukipenda kuna watu 30% ya wakenya wanaishi juu ya 70% ya ardhi.
Ukilinganisha huko ambako 70% ya wakenya wanakoishi na unagalie Satelite Image ya Kenya unagundua hao wakenya wamerundikana kwanye ardhi yenye rotuba alafu hayo maeneo kame ndo watu wengi wamekwepa.