WORLD LUNG FOUNDATION yazindua kampeni ya kuhamasisha uzazi wa mpango mkoani Kigoma

WORLD LUNG FOUNDATION yazindua kampeni ya kuhamasisha uzazi wa mpango mkoani Kigoma

WLF Tanzania

Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
38
Reaction score
22
unnamed (4).jpgMwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Cosmas Swai, akizindua kampeni mpya ya kuhamasisha Faida na Matumizi ya Uzazi wa Mpango jijini Dar es Salaam jana, kampeni itakayotekelezwa mkoani Kigoma. Wanaoshuhudia ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la, World Lung Foundation (WLF), Nduke Mwakatundu (mwenye tai) na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk.Leonard Subi (watatu kulia) na baadhi ya wafanyakazi wa (WLF).

unnamed (5).jpgMkurugenzi Mkuu wa Shirika la World Lung Foundation (WLF), Nduke Mwakatundu, akijibu maswali ya waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha faida na matumizi ya uzazi wa mpango jijini Dar es Salaam jana, mpango utakaotekelezwa mkoani Kigoma. Kushoto ni Mwakilishi wa Kaimu Mkurugenzi wa Huduma za Kinga Wizara ya Afya, Dk.Cosmas Swai na Mganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Dk.Leonard Subi.

unnamed (6).jpgMganga Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, Dk. Leonard Subi, akizungumza wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa kampeni mpya ya kuhamasisha faida na matumizi ya uzazi wa mpango jijini Dar es Salaam jana, mpango utakaotekelezwa mkoani Kigoma chini ya Shirika la World Lung Foundation (WLF).

Picha zaidi za kilichojiri kwenye kampeni hizo;

5.JPG
8.JPG

6(1).JPG
 
Attachments

  • 7.JPG
    7.JPG
    198.5 KB · Views: 50
Kwanini hizi kampeni za uzinduzi hamkwenda kufanyia kwenye mkoa husika ambao ni Kigoma? Kwanini kila kitu Dar?

Ila mmefanya Jambo zuri sana maana mikoani hasa sehemu za vijijini hawana habari na suala la mpango wa Uzazi,wao wanachojua ni kuzaa.

Hasa familia masikini ndio wahanga wakubwa wa kuzaa zaa kama sungura. Hapa naamini msemo unaosema kuwa "starehe ya Masikini ni Kuzaa"

Kazi njema WLF.
 
Lung na uzazi wa mpango wapi na wapi???

Anyway kampeni ni nzuri
 
Kwanini hizi kampeni za uzinduzi hamkwenda kufanyia kwenye mkoa husika ambao ni Kigoma? Kwanini kila kitu Dar?

Ila mmefanya Jambo zuri sana maana mikoani hasa sehemu za vijijini hawana habari na suala la mpango wa Uzazi,wao wanachojua ni kuzaa.

Hasa familia masikini ndio wahanga wakubwa wa kuzaa zaa kama sungura. Hapa naamini msemo unaosema kuwa "starehe ya Masikini ni Kuzaa"

Kazi njema WLF.

Mambo ya fursa hayo yakhee...

Natania tu. Ila kama ni kweli wana nia ya dhati, basi hakuna shaka ni kampeni nzuri na angalau itawasaidia wanakijiji walio mbali na huduma muhimu kama hizi. Sio huduma tu, itasaidia pia hata ku-boost muamko wao ambao pia ni mdogo kutokana na kukosa uelewa wa haya masuala kwa kina. Nawapongeza kwa hili kwa kweli..

Lakini nachelea isijekuwa ni mwendelezo wa kuwatumia wahitaji kama ngazi ya kufikia kwenye malengo yenu tu!
 
Back
Top Bottom