Manyanza
JF-Expert Member
- Nov 4, 2010
- 16,464
- 35,629
Dar es salaam
Ikulu ya Mjerumani ikiteketea baada ya kupigwa kombora toka kwenye meli ya mwingereza.
Kwenye eneo hilo ilibidi mwingereza ajenge Ikulu mpya
Miongoni mwa maeneo yaliyoshambuliwa siku hiyo ni pamoja na mnara wa mawasiliano (wireless tower) ambao Wajerumani walikuwa wakiutumia kwa mawasiliano ya ndani na nje ikiwamo kwao Ujerumani na duniani kwa ujumla. Lengo likiwa kukata mawasiliano kati ya vikosi vya Wajerumani vilivyoko Afrika Mashariki na kule Ulaya. Hata hivyo, Wajerumani walikuwa na minara mingine miwili mikubwa na yenye nguvu iliyokuwa Tabora na Bukoba. Historia ya Vita ya Kwanza ya Dunia huku Afrika Mashariki inavutia sana na ina mafunzo mengi.
Ikulu ya Mjerumani jijini Dar es Salaam baada ya kupigwa na makombora ya mwingereza
Madhara ya vita ya kwanza ya dunia jijini dar es salaam
Majeruhi wa vita
Hii ilikuwa Battle of Mahiwa,kusini ya nchi ya Tanganyika.Ukiondoa battle ya Tanga hii ilikuwa kubwa, askari wa Waingereza 2700 walipoteza maisha wengi wao wakiwa South africans na Nigerians.Upande wa Mjerumani askari 600 walipoteza maisha kati yao wazalendo wakiwa 570. Vitabu vyingi vya historia vimeandikwa kuhusu hii battle na ile ya Tanga.
Hii battle Mjerumani alishinda lakini jeshi lake likiwa dogo askari 600 waliouawa walikuwa wengi ikabidi Von Lettow akimbilie Portuguese East Africa ambayo ni Msumbiji kuanzia hapo wajerumani wakawa wanapigana kama askari wa msituni.Mjerumani von lettow ikumbukwe kiswahili kilipanda na alikuwa kipenzi cha askari wazalendo