Hiyo degree ya Mh Mrema kama nakumbuka vizuri ni ya chuo cha Pacific Western University. Kuna watu wanawazodoa wasomi wa Mzumbe University na VC wao Warioba ambao pia wana PhD kutoka chuo hicho. Inaelekea kuna namna fulani ya kutokikubali chuo hicho pale Bongo.
Tukirudi kwenye on-line degrees, zinaweza kukubalika kama utaratibu wa chuo husika unawezesha wanafunzi kusoma genuinely na kupata instructions na assessment ambazo kimsingi zina ubora sawa na wale wanaosomea chuoni. On-line degrees ni mfumo uleule wa Open University, tofauti iliyoongezeka hapo ni teknolojia ambayo inaharakisha mawasiliano baina ya wanafunzi na chuo. La muhimu ni kujiunga na chuo ambacho kiko accredited na mamlaka husika kutoa distance education, kama Tanzania kuna HEAC ambayo inashauri watu kupata kutoka kwao inventories za vyuo kabla hawajaamua kujiunga. Kwa hapa UK kuna board inayohakiki distant learning, na zote zimewekewa standards, na mara kwa mara wanafanya quality checks.
Kwa hiyo distance learning inakubalika kama njia mbadala ya kupata elimu ambayo ni convenient kwa mwanafunzi na ni bei nafuu, japo huchukua muda zaidi kuliko campus-based learning. Cha maana cha kuzingatia ni reputation ya chuo unachotaka kujiunga nacho, na accreditation, mambo ambayo ni muhimu pia hata unapotaka kujiunga na campus-based course.