Wosia alotoa Mloka kwa watunzi chipukizi.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
MAMBO MATANO MUHIMU TOKA KWA MLOKA KWENDA KWA WASHAIRI CHIPUKIZI.
Amani ya mwenyezi Mungu ziwe nanyi nyote,baraka zake ziwafikie na Mola awaepushe na kila la shari lisitufike.
Charles Mloka alizaliwa mwaka 1957 katika kijiji cha Kiswira mkoani Morogoro.
Ni mmoja kati ya watunzi maarufu wa mashairi na muandishi wa vitabu anaetoka katika familia ya waandishi Tanzania.
Mwaka 1988 alitoa diwani yake maarufu ijulikanayo kama DIWANI YA MLOKA,diwani ambayo ilichapishwa na kampuni ya BENEDICTINE PUBLICATIONS NDANDA-PERAMIHO,huku ikikusanya mashairi ya kimapokeo yaliyoandikwa katika mitindo tofauti tofauti.
Leo tutazame kwa ufupi kabisa mambo matano ambayo ndugu MLOKA aliwausia washairi chipukizi katika kitabu chake hicho cha DIWANI YA MLOKA.
Jambo la kwanza anawausiwa washairi kwa kuwaambia kwamba,ushairi una asili yake na asili yake ni vina na mizani,anasema:

"Mosi vina na mizani
Vya kubidi kwa makini
Kutumia kwa idhini
Ya utunzi asilia.

Pia anawausia washairi chipukizi jambo la pili la muhimu kabisa ni kuzingatia mambo yanayoweza kutoa mwanga katika jamii,anasema katika beti ya nane shairi la WOSIA KWA CHIPUKIZI:

" Pili upende kutunga
Mambo yaliyo ya mwanga
Watu watayo yaunga
Yaliyo ya kuvutia.

Jambo ka tatu,anawausia washairi kutukupenda tabia ya kujisifu na kujifanya maarufu,akiamini tabia hiyo umuharibia mtu.
Anasema:

"Tatu sipende jisifu
Kujifanya maarufu
Tungo unapo sarifu
Huko kujiharibia.

Anaendelea kusema kuwa tabia ya kujisifu imewaingia wengi na wanaona jambo la kawaida.

" Ingawa hii tabia
Wengi imetuingia
Kila tunapotokea
Haifai Mara mia.

Wosia wa nne anawaambia washairi chipukizi wasijione wanajua sana kuliko washairi waliopita,anasema:

"Usijifanye kuona
Kwamba yu wajua sana
Kuliko wale wa Jana
Hiyo kamwe siyo njia.

Anamalizia kwa kuwaambia washairi chipukizi wapende kutazama kazi za watu wengine ili kujiongezea maarifa,akisema:

"Penda kutazama kazi
Walizotenda watunzi
Uuongoze ujuzi
Na wewe kuendelea.

Muandaaji-Idd Ninga
Tengeru,Arusha
Voice of youth Tanzania
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Rejea-DIWANI YA MLOKA,1988,NDANDA MISSION PRESS.
 
"THE WONDERFUL SURGEON AND OTHER POEMS" by Charles Mloka.
 
Back
Top Bottom