SoC02 Wosia wa Yuda: Ukweli kuhusu funguo

SoC02 Wosia wa Yuda: Ukweli kuhusu funguo

Stories of Change - 2022 Competition

TheMoneyMindset

New Member
Joined
Aug 28, 2022
Posts
1
Reaction score
0
IMG_9633.jpg

[Source: unsplash.com]

Nikiwa katikati ya likizo ya chuo mwezi wa nane nilienda kwa rafiki yangu aitwaye Hafidhi huko Kigamboni.Nia na dhumuni nikucheza tu magemu na kupiga story.

Mida ya saa nane tukasikia geti likifunguliwa,mara gari aina ya BMW X6 ikaingia.Nikamuuliza rafiki yangu "Huyu ndio mdingi?" akanijibu "Ndio,huyo ndio Mzee Yuda."

Alivyoegesha gari lake akaingia ndani nakukaa sebuleni kwenye kochi mahali ambapo tulikuwepo.Tukamsalimu "Shkamoo Baba" huku nikiwa na mshangaa kwani ndio mara ya kwanza namwona Mzee Yuda.Akatujibu "Marahaba wanangu,Hafidhi naomba uzime magemu yenu kwa muda kuna fumbo nataka niwaachie wanangu." Hafidhi akaenda kuzima TV na kurudi kuketi.

Ndio akaanza kuteta;
"Maisha yetu tumelelewa kwenye mfumo ya kwamba mwisho wa siku yatubidi tupate funguo ya maisha yetu.Funguo hii imezoeleka sana kupatikana shuleni ,lakini sasa na utandawazi na mitandao ya jamii kuna njia nyingi tu inayofanya iwe rahisi kuipata.


IMG_9638.jpg

[Source: unsplash.com]

Funguo hii kuipata kwa njia iliyozoeleka inachukua muda sana ya kwamba wengi huishia njiani na kutafuta njia mbadala.Hata hivyo vitasa vimezidi kupungua na vyenye masharti ili mradi vifungue,hivyo sio funguo tu bali unahitaji pia kujuana na watu ambao wamefungua hicho kitasa kinachokusumbua ili mradi uweze kufanikiwa.

IMG_9639.jpg

[Source: unsplash.com]

Ukitumia funguo hii kwa ajili ya kufungua vitasa ambavyo vishafunguliwa basi njia ni nyembamba sana hata usiifurahie,lakini ukitumia funguo hio na kufungua vitasa ambavyo bado havijafunguliwa basi njia yako itakua pana sana na kuifurahia.Cha kushangaza ni kuwa watu tumeelekezwa na tunatumia muda mwingi tupate funguo ili tupite njia nyembamba huku tukikatishwa tamaa yakuwa funguo kufungua njia ambayo ni pana ni vigumu sana labda kama familia yako imepita njia hio.

Je funguo ni nini?,kitasa ni nini?,njia ni nini? Tafakarini kwa makini na wakwanza awezaye kudadafua fumbo hili nitampatia kiasi cha shillingi laki moja kama zawadi tu aifanyie akipendacho yeye."

View attachment IMG_9632.jpg
[Source:unsplash.com]

Mzee Yuda akanyanyuka na kuondoka sebuleni kuelekea chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika.Jioni iliwadia huku bado tunatafakari,mmoja mmoja tukaanza kuondoka kurudi nyumbani kwani giza lilianza kutinga.Niliondoka nakurudi nyumbani lakini fumbo lilinikaa sana kichwani kwani kila mara nilikua nataka nilitatue.Katika kuhangaika siku nzima mpaka usiku bila mwanga ndipo nikaamua kesho yake niende kwa Mzee Yuda aweze nipatia jibu la jawabu kwani nimejaribu fikiria ila nimeshindwa.

Kesho asubuhi na mapema nikaamka na kujiandaa nikachukua baiskeli na kuelekea nyumbani kwa Mzee Yuda.Nilivyofika na kugonga geti nikashangaa Mzee Yuda anafungua geti kwa tabasamu na kusema "Tazama katika wengi wewe ndio shujaa.Twende ndani ukapate kifungua kinywa"

Tukaingia ndani kwake na kuenda kuketi kwenye kiti,yeye akaenda kwanza chumbani kwake,kisha akatoka na bahasha na kuja nayo sebuleni.Baada ya kuketi akasema "Bila shaka huna jibu na wala usiogope,kiu yako yakutafuta majibu ndio imekufanya uibuke kidedea.Chukua hiki kiasi cha fedha kama zawadi" Nikakichukua na kushukuru huku nikitetemeka kwa furaha.Ndipo akaanza kunifafanulia fumbo hilo

DHUMUNI
Hii ni story fupi iliyonikuta katika likizo yangu.Funguo ni elimu,kitasa ni mwanga ,njia ni ajira.

Msingi wa story hii ni kila mmoja awe na kiu ya kutafuta maarifa na ujuzi mbali mbali kwani huenda kwenye kutafuta huku fursa nyingi zinafunguka na tunapata uelewa.Maarifa hutafutwa ,huwa watu wenye ujuzi na kubobea kwenye hilo jambo linalokusihi wengi wao huwapatia vijana bure tu.

Elimu yetu sasa ina changamoto sana kwani kazi zimekua chache ,pia inatumia mda mpaka mtu kuhitimu,hata hivyo bila kujuana na watu wenye vyeo kwenye hizo ajira basi ni ngumu kupata nafasi ya kuajiriwa siku hizi.

IMG_9643.jpg

[Source:unsplash.com ]

Wewe kama kijana,haina haja ya kutafuta ajira kwani kama Mzee Yuda alivyotusihi,elimu ni kwa ajili ya kuondoa ujinga kwenye nyanja fulani ili mradi ikupe ujuzi kwa ajili ya kugundua au kuleta fursa mpya ambazo hazijajulikana zinazotokana na hio nyanja ya elimu uliyobobea.

Maisha ya ajira ni ya kujirudia,tofauti ni kwamba mteja anakuwa mwingine tu lakini mara nyingi vitu vilevile ulivyokua unafanya vinafanyika mpaka sasa.Hivyo basi humfanya mtu kuboreka na kazi kwani hakuna jipya sana tofauti na alivyofanya zamani nakumfanya mtu asifurahie na kuwa na shauku na kazi yake.

View attachment IMG_9642.jpg
[Source:unsplash.com ]

Tuamke sasa kila mmoja hasa nawasihi vijana tubadilishe fikra zetu ili tuweze kutatua changamoto za kijamii huku tukijiingizia kipato.
 
Upvote 0
Back
Top Bottom