Wosia Wangu Kwako

Wosia Wangu Kwako

ubongokid

JF-Expert Member
Joined
Apr 30, 2017
Posts
2,154
Reaction score
4,184
Mwanangu
Yatazame tu maisha hivi hivi ila asikuambie mtu;
Hapa duniani hukuomba uletwe,Ulijikuta tu huko hapa umeunga mstari so inabidi uendelee ila asikuambie mtu maisha yatazame tu.Ila wacha nikwambie ukweli mdogo niliojifunza kuhusu Maisha.Huenda ukakusaidia

Kuhusu Siku na Wakati
Kila siku ni siku mpya na ni mwanzo mpya. Yaliyotokea yameshatokea na hakuna namna unaweza kurudi nyuma kufanya yawe hayajatokea. Hata hivyo usisahau kwamba kila siku inakupa fursa mpya,fursa ulizopoteza zilishapotea.Usipokuwa makini hata fursa ulizonazo au unazodhani unazo nazo zitapotea.

Kuhusu Msamaha na Kukosea
Kila mtu anakosea na maisha yetu yote ni Makosa Kwa hiyo basi Usiogope kukosea lakini usiogope kuomba msamaha wala usiogope kusamehe kwani kuomba au kutoa msamaha hakutakupunguzia kitu. Msamaha pia ni namna ya kukuwezesha wewe kuendelea na maisha badala ya kupoteza muda ambao nao unaenda kwa kasi.

Kuhusu Kupenda na Kupendwa
Usiogope kupenda wala kupendwa kwani kupenda au kupendwa kutakuongezea vitu vingi sana maishani. Usisahu Kumpenda akupendaye na zaidi kumuacha yule ambaye hakupendi.Maumivu ya mapenzi hupoteza muda na kukunyima fursa ya kupenda mwingine.

Kuhusu Ukamilifu
Hebu fikiri uliposhindwa kukamilisha jambo na ukumbuke ulichojifunza kwani ukamilifu ambao hauna mafunzo ni upungufu.Kukua kwa mwanadamu hupimwa katika kujifunza na sio kukamilisha mambo

Kuhusu Fursa
Hebu tazama fursa ila zaidi angalia namna ya kujiongezea uwezo na ujuzi wa kutumia Fursa,kwani duniani hakuna uhaba wa fursa bali kuna uhaba wa uwezo na ujuzi na maarifa yanayowezesha mtu kutumia Fursa flani-Kama unakataa jaribu kufikiri tena ni fursa gani unazikosa kwa sababu tu ya kuwa na uwezo mdogo au kwa sababu ya kukosa Ujuzi.

Kuhusu Uhusiano wako na Mungu
Angalia Juu kwa Mungu halafu jiulize ni uwezo gani ulio ndani yako.Usijichukulie POA.Kauli yako ina nguvu,fikra zako zina nguvu na nguvu yako ina nguvu kweli kweli.Kama huamini katika Uwezo jaribu tu kutafakari ni mangapi mema au mabaya ambayo ulijiwazia ambayo yalitimia katika maisha yako.

Kuhusu wanaokuvumilia
Usimdharau anayekubeza wala kumchukulia POA anayekuvumilia.YUPO kwa ajili yako na kuna wakati utamuhitaji ndo maana yupo hapo.

Kuhusu Pesa
Hebu fikiri hivi kuhusu PESA.Pesa ni kwa ajili ya matumizi tu.Ukijua kuitumia PESA vizuri itakutumikia ila usipojua kuitumia PESA vizuri utaitumikia.Kuitumikia PESa ni rahisi kuliko Kuitumia hivyo usishangae ukiona unaitumikia kwani tupo wengi ambao tunatumikia Pesa.

Fikiri hivi kuhusu MAPENZI.
Kupenda kupo na mapenzi yapo.Kupenda sio kosa ni jambo la heri.SIO kila mara utakutana na umpendaye na anayekufanya ukose usingizi. Ukimpata Mpende tu kwani huyo anayapa maisha yako maana.

Fikiri hivi kuhusu Marafiki
Duniani hakuna urafiki wa kweli wala uadui wa kweli ila unafiki upo. Kila rafiki uliye naye ni mnafiki na kila mnafiki unayemjua ndiye rafiki yako.Jichangaye na watu ila angalia wasikuchanganye ukajikuta unachanganyikiwa.

Fikiri hivi kuhusu Kufilisika
Ukiwa na pesa ukafilisika usiogope na kujutia jinsi ulivotumia PESA zako.Wala ukiwa fukara ukatajirika usilalamike kuhusu nyakati ngumu ulizopitia. Huko ni kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi.Ukiwa huna Pesa Tumia muda wako kuzitafuta vizuri na ukiwa na PESA basi tumia muda wako katika kuzitumia vizuri.

Kuhusu Sala na Ibada
Usiogope kusali na kumuomba Mungu.Kila uombalo litakuwa. So unaposali wewe lia na Mungu wako na umweleze yote na kufungua moyo wako kwake.Kila utakaloomba Atakujalia

Mwisho wa yote usishau hili;
Utakufa tu, Hakika Utakufa hata kama hutaki hilo halina mjadala. Jambo bora kabisa ni kutumia muda wako mchache hapa duniani kuweka mambo yako sawa hasa yale madogo madogo ambayo yanaweza kukuamsha kaburini wakati umeshazikwa.

JARIBU KUFIKIRIA HALI YAKO UTAKAPOSHTUKA UKIWA KWENYE JENEZA AU UMESHAZIKWA kabisa KISA TU kuna vijimambo vidogo vidogo tu ambavyo hujaweka sawa.

Nawatakia maisha Mema SANA
 
Mwanangu
Yatazame tu maisha hivi hivi ila asikuambie mtu;
Hapa duniani hukuomba uletwe,Ulijikuta tu huko hapa umeunga mstari so inabidi uendelee ila asikuambie mtu maisha yatazame tu.Ila wacha nikwambie ukweli mdogo niliojifunza kuhusu Maisha.Huenda ukakusaidia

Kuhusu Siku na Wakati
Kila siku ni siku mpya na ni mwanzo mpya.
Yaliyotokea yameshatokea na hakuna namna unaweza kurudi nyuma kufanya yawe hayajatokea.
Hata hivyo usisahau kwamba kila siku inakupa fursa mpya,fursa ulizopoteza zilishapotea.Usipokuwa makini hata fursa ulizonazo au unazodhani unazo nazo zitapotea.

Kuhusu Msamaha na Kukosea
Kila mtu anakosea na maisha yetu yote ni Makosa Kwa hiyo basi Usiogope kukosea lakini usiogope kuomba msamaha wala usiogope kusamehe kwani kuomba au kutoa msamaha hakutakupunguzia kitu.
Msamaha pia ni namna ya kukuwezesha wewe kuendelea na maisha badala ya kupoteza muda ambao nao unaenda kwa kasi.

Kuhusu Kupenda na Kupendwa
Usiogope kupenda wala kupendwa kwani kupenda au kupendwa kutakuongezea vitu vingi sana maishani. Usisahu Kumpenda akupendaye na zaidi kumuacha yule ambaye hakupendi.Maumivu ya mapenzi hupoteza muda na kukunyima fursa ya kupenda mwingine.

Kuhusu Ukamilifu
Hebu fikiri uliposhindwa kukamilisha jambo na ukumbuke ulichojifunza kwani ukamilifu ambao hauna mafunzo ni upungufu.Kukua kwa mwanadamu hupimwa katika kujifunza na sio kukamilisha mambo

Kuhusu Fursa
Hebu tazama fursa ila zaidi angalia namna ya kujiongezea uwezo na ujuzi wa kutumia Fursa,kwani duniani hakuna uhaba wa fursa bali kuna uhaba wa uwezo na ujuzi na maarifa yanayowezesha mtu kutumia Fursa flani-Kama unakataa jaribu kufikiri tena ni fursa gani unazikosa kwa sababu tu ya kuwa na uwezo mdogo au kwa sababu ya kukosa Ujuzi.

Kuhusu Uhusiano wako na Mungu
Angalia Juu kwa Mungu halafu jiulize ni uwezo gani ulio ndani yako.Usijichukulie POA.Kauli yako ina nguvu,fikra zako zina nguvu na nguvu yako ina nguvu kweli kweli.Kama huamini katika Uwezo jaribu tu kutafakari ni mangapi mema au mabaya ambayo ulijiwazia ambayo yalitimia katika maisha yako.

Kuhusu wanaokuvumilia
Usimdharau anayekubeza wala kumchukulia POA anayekuvumilia.YUPO kwa ajili yako na kuna wakati utamuhitaji ndo maana yupo hapo.

Kuhusu Pesa
Hebu fikiri hivi kuhusu PESA.Pesa ni kwa ajili ya matumizi tu.Ukijua kuitumia PESA vizuri itakutumikia ila usipojua kuitumia PESA vizuri utaitumikia.Kuitumikia PESa ni rahisi kuliko Kuitumia hivyo usishangae ukiona unaitumikia kwani tupo wengi ambao tunatumikia Pesa.

Fikiri hivi kuhusu MAPENZI.
Kupenda kupo na mapenzi yapo.Kupenda sio kosa ni jambo la heri.SIO kila mara utakutana na umpendaye na anayekufanya ukose usingizi. Ukimpata Mpende tu kwani huyo anayapa maisha yako maana.

Fikiri hivi kuhusu Marafiki
Duniani hakuna urafiki wa kweli wala uadui wa kweli ila unafiki upo.Kila rafiki uliye naye ni mnafiki na kila mnafiki unayemjua ndiye rafiki yako.Jichangaye na watu ila angalia wasikuchanganye ukajikuta unachanganyikiwa.

Fikiri hivi kuhusu Kufilisika
Ukiwa na pesa ukafilisika usiogope na kujutia jinsi ulivotumia PESA zako.Wala ukiwa fukara ukatajirika usilalamike kuhusu nyakati ngumu ulizopitia.Huko ni kupoteza muda kwa mambo yasiyo ya msingi.Ukiwa huna Pesa Tumia muda wako kuzitafuta vizuri na ukiwa na PESA basi tumia muda wako katika kuzitumia vizuri.

Kuhusu Sala na Ibada
Usiogope kusali na kumuomba Mungu.Kila uombalo litakuwa.So unaposali wewe lia na Mungu wako na umweleze yote na kufungua moyo wako kwake.Kila utakaloomba Atakujalia

Mwisho wa yote usishau hili;
Utakufa tu,Hakika Utakufa hata kama hutaki hilo halina mjadala. Jambo bora kabisa ni kutumia muda wako mchache hapa duniani kuweka mambo yako sawa hasa yale madogo madogo ambayo yanaweza kukuamsha kaburini wakati umeshazikwa.
JARIBU KUFIKIRIA HALI YAKO UTAKAPOSHTUKA UKIWA KWENYE JENEZA AU UMESHAZIKWA kabisa KISA TU kuna vijimambo vidogo vidogo tu ambavyo hujaweka sawa.
Nawatakia maisha Mema SANA
Safiiii

Sent from my SM-N960U using JamiiForums mobile app
 
MashAllah! Nilikua na siku nzito, shukrani kwa maneno yako
 
Umenena vyema, tatizo binadamu wa siku hizi ni wabishi sana...
 
Back
Top Bottom