Wote;NCHI IMEFIKIA HAPA..

Tugutuke

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2011
Posts
501
Reaction score
166
Kichwa kimeanza kuchoka, ebu niwaze Taifa...

1. Taifa ambalo binti zake wakimwona Mzungu wanadhani ana ela.
2. Taifa ambalo ukiongea kiingereza unaonekana umesoma.
3. Taifa ambalo bank haikutafuti we ndo unaihonga ikukopeshe.
4. Taifa ambalo ukifeli unakuwa mtangazaji wa kipindi maalumu kabisa.
5. Taifa mbalo simu kali ni dili hata kama vocha waweka za jero jero.
6. Taifa ambalo unazaliwa umeme shida, unafika miaka 30 hata huna bajeti ya Jenereta/Solar, unailaumu tu TAAnexo!
7. Taifa ambalo warembo washajiona wao ni waomba kusaidiwa daima.
8. Taifa ambalo kila mtu anataka ajue bei ya kitu ulichonunua!
9. Taifa ambalo usipoiba unaonekana ----!
10. Taifa ambalo kila mtu analalamika hana ela, mpe dili sasa, anaanza longolongo
11. Taifa ambalo sanne lina foleni ya watu wanaenda makazini
12. Taifa ambalo ukisema upo ofisini satatu usiku unashangawa ila upo club sanane usiku unasifiwa
13. Taifa ambalo kusema jana nlikuwa bata sana ile mbayaaaa ni dili na waonekana mjanja
14. Taifa ambalo bila kuigana siku haijapita
15. Taifa ambalo kila anayehojiwa anasema "Naiomba Serikali iliangalie suala hili"
16. Taifa ambalo ukiwa na gari hutongozi unatoa tu lift kitu shaa
17. Taifa ambalo kulipa bili yako pekeako ukaruka za wengine ni vita
18. Taifa ambalo ikinyesha dakika 5 tu foleni masaa
19. Taifa ambalo viongozi wanajua "hawa watazoea tu" washazoea umeme, washazoea "haijajulikana", watazoea na hii
20. Taifa ambalo kijiMC kidonyo tu kinaweza kufariki Taifa zima likageukia Msiba
21. Taifa ambalo kuteswa ni kunyofolewa Meno na Kucha
22. Taifa ambalo viongozi wake wana mipasho ka taarabu
23. Taifa ambalo vijana wameombwa wasipondee bali wasifie nchi
24. Taifa ambalo hata bomu likilipuka Arusha, wa Mbagala anajichagulia jina la Mlipuaji
25. Taifa ambalo, dah, nmechoka, endeleeni nyie....
 
Mkuu hii taarifa kwa kukushauri ungemwandikia slaaa na lwakatare kunavitu vingi ambavyo umeongea lakini hawa ndiyo walengwa wanajua kutekeleza haya uliyoondika.
 
26. Taifa ambalo lina chama cha siasa cha wapiganaji wakati hakuna vita.
 
Mkuu hii taarifa kwa kukushauri ungemwandikia slaaa na lwakatare kunavitu vingi ambavyo umeongea lakini hawa ndiyo walengwa wanajua kutekeleza haya uliyoondika.

Bora kuolewa kwa kweli!Maana joto linakufanya uwafikirie Slaa na Lwakatare tu, asubuhi yote hii jaman?
 
nyongeza:taifa ambalo kijana anaenda mlimani city mall kuzurula na kuuza sura siku nzima bila kufanya manunuzi halafu anajiita wa kisasa.window shoppers.
 
26.taifa ambalo linawatetemekea wawekezaji kama ndio mkombozi wa maskini kumbe na wawekezaji wamekuja kuwaibia
27 .taifa ambalo limeua viwanda vyake vyoote na kutegemea kulalamika hamna ajira
28.taifa ambalo viongozi wake wanadai wamesoma ilhali mchango wa elimu zao hazionekani.wanawaza kwa masaburi
29.taifa ambalo chama tawala kiko juu ya sheria ham,na haki kwa wananchi wake.
 

28.Taifa ambalo lina re seat mitihani badala ya wanafunzi
29.Taifa ambalo wanafunzi wana faulu pasipo kujua kuandika na kusoma
30.Taifa linalo ongozwa na Dhaifu!
 
Nashkuru sana kukutana na huu uzi... Wadanganyika na maisha yetu bana it is so sad.. Ukweli mtupu 100% na atakaebisha atakuwa co raia wa nchi hii
 
Taifa ambalo lina rasilimali ya kutosha kisha maskini
Taifa ambalo wa nje wanaona "bikira" wa ndani wanaona "kahaba"
ehy this my loved country???!!!
SP
 
taifa ambalo ukiwa chma tawala kupata uongoz lazma uwe
mtoto wa kigogo tena aliye fisadi.
 
taifa ambalo governor wa benki kuu anaiba matilion alafu ambao wangemwazbu wanasema kafariki.
 
12 na 15 umelenga sn na ndo maana individuals hawaendelei
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…