BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
Huko Tanganyika kila mtu ni machinga, hata wasio na ujuzi wa kibiashara nao unawakuta wanachuuza malapa mitandaoni.
Tangu Watanganyika waambiwe kujiari basi imekuwa fujo mno, mara huyu anauza ubuyu, mara huyu anauza tumikoba twa kike!
Mitandao imechafuka biashara uchwara za kuchuuza malapa na kandambili. Kila ukifungua WhatsApp unakutana na tumalapa tumejipanga kwenye utitiri wa status. Ati "online business".
Mwingine naye unakuta ameajiriwa ajira rasmi kabisa lakini naye yumo tu anang'ang'ana amepanga ubuyu mitandaoni anauza etii! Sijui ni ugonjwa wa akili?
Mlipoambiwa mkajiajiri tulitarajia kuona vijana wasomi wakija na mawazo bunifu ya kuunda vitu vikubwa na sio kuuza tumalapa kwenye WhatsApp!
Nikiona umeweka malapa kwenye WhatsApp nakulima BROKU.
Hatuwezi kuwa machinga nchi nzima. Jiongezeni mnatuchefua na tumalapa twenu. Eboo!!