MASIKIN JEURI
Senior Member
- Jan 31, 2013
- 134
- 22
Wana jamvi, nimevutiwa na aliyekuwa mh.waziri wa mambo ya ndani ya nchi, bwana Lawrence Masha ktk kipindi cha mkasi kilichorushwa jana na EATV. Pamoja na mambo mengine bwana Lawrence Masha alisema ametembea nchi nyingi sana, na bila kumunyamunya maneno alisema watanzania ni "waongo sana" kuliko nchi yoyote, kitu ambacho nimekiamini. ktk maelezo yake pia aligusia appreciation ya wa tz kwa mtu anaeleta mchango ktk jamii ni mdogo, mfano yeye alikuwa akisomesha watu 290 kama sikosei kwa familia zisizojiweza,amesaidia kujenga shule ya mkolani ya jijini Mwanza kwa hela na mchango wa wafadhili alioutafuta yeye mwenyewe. LKN pia wapiga kula wake wengine hawana lugha nzuri hasa mtu anaporopoka kuwa sisi ndiyo tuliokuchagua kwa hiyo tunapokuita lazima uje, kwa ubinadamu wa kawaida kabisa, kwa lugha kama hizo hata kama ni mimi, wewe na mwingine lazima uudhike.
Hebu tumlinganishe na mhe.Wenje ktk mchango wake ktk jimbo, je ni yupi alieleta maendeleo zaidi? wote wazuri, lkn namshauri bwana Lawrence Masha aachane na CCM na kujiunga na CHADEMA au, abakie CCM lkn ajitofautishe na ufisadi na unyonyaji wa CCM, awe kama akina Magufuli, Mwakembe, Deo Philikumjombe, mh.mbunge wa Kisesa, na wengine wachache walio ccm ambao siyo wanafiki kwa raia wao, hakika atapata kula za watu wengi.
Nawasilisha.