FORBES AFRICA kwenye jarida lao la mwezi September (cover page) wameandika, nitanukuu “BITCOIN, CRYPTOCURRENCY THE FUTURE”
(Tazama picha chini)
BANK OF TANZANIA (BOT) nao kwa mara ya kwanza katika historia wamezungumzia kwenye gazeti la THE GURDIAN (9th October 2017) juu ya Cryptocurrency na Bitcoin.
Hizi ni Taasisi kubwa zenye uelewa mkubwa sana juu ya mambo ya Fedha na Biashara. Hivyo wana AUTHORITY kwenye chochote wanachopendekeza/ elekeza.
Well, Hii BITCOIN na CRYPTOCURRENCY ni nini?
Kwa Lugha rahisi, Bitcoin ni Pesa ya kidigitali (digital currency) ambayo unaweza kuitumia kulipia bidhaa na huduma mbalimbali.
Mfano: Unaweza kununua mikate Tasty bakery Mikocheni DSM ukalipa kwa bitcoin.
Au Ukanunua gari Kwenye Kampuni ya Beforward Japan, ukalipia kwa bitcoin.
Au ukanunua software kwenye mtandao ukalipa kwa bitcoin.
(Tazama picha chini)
Pesa hii ilianza kutumika mwaka 2009 ikiwa na thamani ya pesa za kitanzania Takribani SHS 250/=
(Shilingi mbia mbili hamsini) kwa bitcoin moja.
Miaka (8) nane baadae yaani leo 2017 Bitcoin moja ina thamani ya sh 12,571,326/= ( Milioni Kumi na mbili, laki tano sabini na moja elfu, mia tatu ishirini na sita) Tazama picha chini au Google.
Kama ungenunua bitcoin zenye thamani ya Tsh 500,000 tu mwaka 2009, ungepata kiasi cha Bitcoins 2000. Leo hii bitcoin hizo zingekua na thamani ya Tshs 25,142,652,000 (Bilioni ishirini na tano, milioni mia moja arobaini na mbili, laki sita hamsini na mbili elfu.)
Kwa Mwaka mmoja na zaidi sasa nimeisoma sana na kununua kiasi cha hizi Bitcoins.
Mwezi January 2017 kama sehemu ya kujifunza nilinunua kiasi kidogo cha hizi pesa zenye thamani ya Tshs 800,000/= na kuzihifadhi kwenye “Bitcoin wallet”
Bitcoin moja ikiwa na thamani ya Tsh 2,000,000/= wakati huo.
Hivyo nilipata 0.4 bitcoins.
Leo hii thamani ya bitcoin imepanda, hivyo hizi 0.4Bitcoins Zina thamani ya Tsh 5,028,400
Huu ni ukuaji wa zaidi ya 500%
Nawaza tu kama ningekua na mtaji wa sh 100,000,000 januari mwaka huu, leo hii ningekua nina mtaji mkubwa kiasi gani.
Too good to be true, right? Many people have fallen in this trap.
Nilicho elezea hapo juu ni personal experience yangu.
Watu wengi HUDHANI:
1. Bitcoin ni kampuni
2. Bitcoin ni Biashara ya mtandao (Network Marketing)
3. Bitcoin ni utapeli
4. Bitcoin ni kitu hatari
5. Bitcoin Haipo.
Ukweli ni yote ambayo watu hudhani hapo juu SIO KWELI. Ukweli ni kwamba BINADAMU wengi huogopa vitu wasivyovijua, na wengi hawaijui bitcoin.
Bitcoin ni somo pana sana.. hivyo sitaweza kueleza kila kitu leo. Nitaendelea siku Nyingine.
[HASHTAG]#Bitcoin[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Cryptocurrency[/HASHTAG]
[HASHTAG]#Digitalcurrency[/HASHTAG]
[HASHTAG]#BlockchainTechnology[/HASHTAG]
[HASHTAG]#TheFuture[/HASHTAG]
Kama utapenda kujua namna ya kufanya uwekezaji kwenye Bitcoin au ungependa kuifahamu zaidi Tuwasiliane kwa no +255765780139.
Attachments
-
626FD598-522A-4047-B2B1-39AC78D230DB.jpeg455.4 KB · Views: 68 -
7AA17922-CB9A-4998-840F-CCA2F475619B.jpeg260.2 KB · Views: 72 -
F328FC54-D949-4371-BD1B-CC38E5DF7850.jpeg182.2 KB · Views: 72 -
8994053C-FB2A-4CEE-8563-3CA6FF2D5366.jpeg55.4 KB · Views: 68 -
575C7CAB-97F7-40DE-8088-F7217B138E58.png117.6 KB · Views: 77 -
137BB593-07B1-4CF0-AB4E-3485E3AB5F7F.jpeg33.8 KB · Views: 73