Hizi internet services katika nchi yetu naona bado ni matatizo tu, nadhani bado inaonekana kama ni luxury item tu, huwezi uka afford kutumia internet kwa ajili ya utafiti wa vitu mbalimbali na kujielimisha (browsing & downloading) kwa convenience, bei au speed ndogo ya internet itakuangusha tu.
Majuzi Zain wameleta offer nzuri sana kwa bundle kama DATAWIKI = 3gb kwa 15,000 = tsh 5 kwa mb. imekuwa afadhali sana, lakini speed yake ni ndogo, ukilinganisha na zantel pia haina convenience kuitumia kwa kuangalia video streaming websites kama youtube, video zinakatakata kwa ajili ya speed ndogo.
Na kwa hivi sasa watu wengi duniani wanapata taarifa na maarifa mbalimbali kwa kujielimisha kwa hizi internet video streaming programs, hapa sisi tunashindwa kabisa, tunakwamishwa na bei au na pia kasi ya mtandao.
Zantel wana speed kubwa na na stable, kwa matangazo ya ki ushindani inaonyesha wana bei nzuri, lakini ki ukweli katika matumizi huru ya internet bei yao pia ni kubwa. minimum yao ni tsh 24 kwa mb katika bundle ya 250mb z-small. kwa matumizi ya kujielimisha natumia zaidi ya shilingi elf kumi kwa siku. hii sio affordable kwa watumiaji wengi.
Nafikiri wanaofurahia internet services hapa nchini ni wale wanaotumia kwa kujibu e-mail tu, au wanaotumia ku browse katika specific websites kwa kazi zao maalum, eg wanaotumia alibaba.com au amazon.com kwa specific short time online shopping activities. Kwao hizi bundle limits na low speed haziwakwamishi sana.
Kwa maoni mi naona , kama kweli tunataka kufaidika na maendeleo haya ya mtandao, basi lazima hii namna ya gharama na speed limits iangaliwe upya,
nafkiri gharama lazima ziwe na muelekeo wa unlimited data capacity, of high speed, kwa muda maalum eg mwezi, kwa around 25 us dollar. Au kama kunawekwa capacity limit basi iwe juu zaidi ya 15gb. hii ni kama kweli tunataka watu wetu hasa vijana walioko katika elimu mbalimbali wafaidike na teknolojia hii mpya kwa maana ya kutumia most of its potentials affordably, ama sivyo tanataka tu kuwafaidisha madalali wa kimataifa wasioshiba kujifanya wanawezesha, kumbe wana tutumia sisi desperate citizens kama mtaji wao. Wanacheza TRICKS.
Kwa sasa watu wanazuia (disable) hata computer zao zisipate free updates za windows(operating systems), antivirus programs au kupata software mbalimbali za bure, au kudownload free new beta testing software. kwa kuogopa expensive internet bandwith zinavyolika au na pia its low speed. Huku sasa siyo kufaidika na maendeleo mapya. Huku ni kushuhudia jinsi tunavyobaki nyuma katika maendeleo mapya duniani na tusijue la kufanya.
Mambo haya yanahitaji mabadiliko, ama sivyo tunajiandaa kuwa tegemezi wa wataalam wa baadae. Wakati tunaizuia njia hii mpya ya kuwapatia na kuwashirikisha wataalam wetu elimu na maarifa mapya kwa Kisingizio cha biashbara, malipo yake yatakuwa makubwa sana kwa siku za baadae.
Iachiani teknolojia ya internet iwafikie watanzania katika potentials zake zote wala isiminywe na iwe nafuu maana inawezekana, hii atakuwa chachu au changamoto ya vijana na watanzania wote kushiriki kikamilifu katika dunia mpya ya utandawazi. ama sivyo tutazembea kwa kisingizio cha kutowezeshwa kimawasiliano ya habari, kisha kuwa Mategemezi na pia Watumwa wa maarifa.