Wanajamvi naombeni ushauri wenu,uyu dada niliwah kumchumbia,nikamsomesha toka form four mpaka mwaka jana kamaliza degree yake ya education pale SAUT,akantosa miezi sita kabla hajamaliza chuo kwa kunipa live kuwa alikuwa hanipendi miaka yote ile bali alikuwa anataka kusoma tu amalize,sasa juzi kanipigia sim kwa no mpya nisiyoijua,akaniomba nikutane nae na tena anataka kuja nyumbani kwangu baada ya kujua bado sijaoa,na alivyonimwaga alinikashifu vibaya na sina hata ham ya kumuona walau kwa bahati mbaya,na ye ndo anang'ang'ania kuja kwangu,nifanyeje?
Hapo pekundu na hasa kwenye mstari ni jibu tosha kwamba unapaswa wewe mwenyewe uzingatie hayo.
1. alikuambia yeye shida yake kwako ilikuwa ni mali yako na hakuwahi na wala hakupendi.
2. Alikukashfu sana.
Mimi binafsi, ni kwamba katika yote fanya lkn suala la kunikashfu ni fedheha sana. Hivyo, nakupa pole sana kwa yaliyokukukuta. Ulijinyima kwa kiasi kidogo ulichokuwa nacho badala ya kuwasaidia ndugu zako au kufanya mambo ya maendeleo, lkn kwasababu ulisikumwa na upendo kwa huyo dada ulijinyima kwa vyote ili afanikiwe kufikia malengo yake. Si ajabu hata wewe labda hayo mafanikio ya elimu haukujaliwa kama ulivyomfanikisha (samahani kama nitakuwa nimekukwaza hapa, lkn ni hasira ya kutokana na alivyokutenda huyo dada). Lkn katika yote mwishowe ulikuja kuambulia Fedhea na si ajabu hata matusi ya nguoni.
Ndugu yangu, mimi nakuambia jibu moja tu kwamba huyo dada HAKUWAHI KUKUPENDA NA HATATOKEA KUKUPENDA, lkn sasa mambo yake hayajanyooka na anakumbuka ulivyojitoa kile kipindi anasoma, hivyo anaamini kwamba utampokea tu.Hivyo mimi nakupa ushauri ufuatao,
1. Kamwe usionane naye, kwani hakuwahi kukuhitaji na kama anakuhitaji sasa ni kwasababu kakwama au katoswa na sasa kwako ndiyo pakumalizia stress na matatizo yake.
2. Na kama utaamua kuonana naye, jitahidi sana isiwe kwako unapohishi.
3. Kuwa na tahadharii zaidi, kwani si ajabu ana matatizo hata ya kiafya anataka akugawie. Hili likitokea itakuumiza zaidi, kwani itakutonesha kidonda ambacho kilishaanza kupona.
4. Kuwa na msimamo kama mwanaume na usikubali kurudi nyuma,kwani kuna hatari mabo yake yakishamnyokea ATAKUMWAGA TENA: