Xclusive interview with Diamond, Fahamu mengi usiyoyajua juu yake.

kipenga

JF-Expert Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
219
Reaction score
55
UKIFIKA katika mtaa anaoishi mwanamuziki Diamond maeneo ya Sinza Mori jijini Dar es Salaam utaanza kuhisi kuwa kuna staa anayeishi maeneo hayo, macho ya wengi huanza kumtazama mtu anayeelekea katika geti la nyumba anayoishi msanii huyo. (HM) Muda wote geti hilo limefungwa. Ili uweze kuingia ndani itakulazimu ubonyeze kengele itakayoashiria kuwa kuna mgeni nje anahitaji kuingia ndani. Hata hivyo hauwezi kupenya kirahisi ndani hadi uulizwe shida yako na kama hauna miadi na mtu yeyote anayeishi ndani ya nyumba hiyo haitakuwa rahisi kuingia. Mwanaspoti lilitinga katika nyumba ya msanii huyo na kushuhudia ukimya wa hali ya juu ilhali kuna watu ndani. Baada ya kufunguliwa geti tuliingia ndani na kupokewa na Diamond aliyekuwa ameketi katika sebule iliyonakshiwa na mapambo makini ukutani huku ikiwa na samani chache lakini za gharama kubwa. Tulitumia saa mbili mfululizo katika mahojiano na Diamond ambaye alifunguka kwa kila swali aliloulizwa na kujibu kwa ufasaha na ufafanuzi mpana. Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje katika muziki? Diamond: Nina mipango makini katika kazi zangu. Mambo yote lazima yapitie kwa meneja wangu
ndipo yanifikie mimi, mara nyingi mtu hawezi
kuzungumza na mimi moja kwa moja lazima apite
huko na hiyo ndiyo staili ya Diamond. Nimejipanga
kuhakikisha nafanya kazi gani, kwa wakati gani
na sikurupuki tu, japo katika utengenezaji wa nyimbo zangu naweza nikapata wazo basi hapo
hapo nikatengeneza mistari. Mwanaspoti: Utendaji kazi wako ukoje kuanzia asubuhi hadi jioni? Diamond: Saa tano asubuhi, nikishaamka kitu cha kwanza ni kwenda 'gym', mara nyingi ni hapa
nyumbani kama unavyoona hapo nje kuna
sehemu ya mazoezi na sehemu
nyingine zilizopo ndani, mara nyingi hutumia
muda wa saa moja. Ifikapo saa sita na nusu huwa
naanza kufanya kazi zangu lakini itategemea na ratiba zangu za siku ambazo ndio mwongozo
wangu wa kuimaliza siku. Baada ya hapo
napumzika kwa muda fulani na baadaye jioni
huendelea na kazi na mara nyingi kazi zangu
huwa nazimaliza usiku wa manane. Mwanaspoti: Unalala saa ngapi? Na unalala kwa muda gani? Diamond: Muda wangu wa kulala mara nyingi ni saa kumi na moja alfajiri na kama sikuwa na kazi
nyingi studio basi nitalala saa nane usiku. Muda
wangu wa kulala ni saa sita mpaka nane kwa siku.
Ila hata kama nikilala mapema kuamka ni saa tano
asubuhi ila itategemea na nini ninakifanya siku
inayofuata na kama nina kazi maalumu na ya mapema itanilazimu niamke mapema ili
kuzikamilisha. Mwanaspoti: Shughuli gani zinazokuchelewesha mara kwa mara kulala? Diamond: Ni kurekodi na wakati mwingine shoo. Kwa wiki ninafanya shoo nyingi, kama ni tatu basi
siku zote tatu nitalala alfajiri. Siku nyingine
zinazosalia ninalala usiku wa manane kwa kuwa
huwa nakuwa studio na sehemu nyingine ambazo
hunilazimu kufanya kazi kwa kipindi kirefu usiku. Mwanaspoti: Kati ya usiku na mchana ni muda upi unaopenda kurekodi? Diamond: Kazi zangu narekodi usiku na ndiyo muda ninaopendelea zaidi. Mara nyingi napenda
kurekodi saa 7 usiku ili niwe na muda na saa
nyingine ni kuepuka lawama kurekodi mchana,
kwasababu vijana wengi chipukizi wataona
napendelewa. Unajua ninapoingia studio napenda
kufanya kazi kwa muda mrefu, hata hivyo iliyo bora sifanyi bora liende na siwezi kufanya kazi na
prodyuza anayenipeleka tu, ni lazima na mimi
nipime kama kazi niliyoifanya inakwenda vile
ninavyotaka au kama yeye anavyotaka ilimradi
tufanye kazi nzuri na iliyo
bora. Mwanaspoti: Unatumia muda gani kurekodi singo moja na kwa upande wa video ni siku
ngapi? Diamond: Inategemea, inaweza kuwa siku mbili au miezi sita lakini nyimbo nyingi zinatumia muda
mwingi kwasababu wakati mwingine naanza
halafu napata shoo hivyo inanibidi nipange muda
mwingine wa kurekodi. Kuna nyimbo zangu
ambazo nilizifanya kwa muda mrefu sana hizo
huwa sizisahau ikiwemo Ukimwona, Mbagala, Nataka Kulewa na nyinginezo. Nakumbuka katika
kazi nilizofanya kwa muda mfupi ni My Number
One nilioufanya kwa prodyuza Sheddy Clever kwa
kipindi kifupi sana pamoja na Mapenzi Basi
sambamba na Binadamu hizi ni baadhi ya kazi
ambazo hazikunipasua sana kichwa kuzikamilisha. Mwanaspoti: Una prodyuza wako maalumu au studio yako mwenyewe? Diamond: Sina prodyuza maalumu kila kazi nitakayotaka kuifanya ninatafuta prodyuza yule
ninayemtaka hata kama sijawahi kufanya naye
kazi. Ninafanya hivi nikiwa na malengo maalumu
kwa kujiweka vizuri mimi kama msanii na hata
kuwapa nafasi maprodyuza mbalimbali kutia
mkono kwenye kazi ya mikono yangu. Ninaogopa kuwa na prodyuza maalumu kwa kuwa najua
atanisumbua ikiwa atajua kwamba namtegemea
yeye pekee katika kazi zangu. Studio sina kwa
sasa ila nina mikakati ya kuwa na studio kwani
nimeshanunua baadhi ya vifaa. Mwanaspoti: Unadhani ndiyo sababu iliyokufanya ukagombana na Bob Junior au
Manecky? Diamond: Hapana haya mambo yalishapita lakini nilijifunza mengi ndiyo maana niliamua kuja na
staili hii. Naogopa kubaki kuwa msanii
ninayetegemea prodyuza fulani, bila yeye siwezi
kufanya muziki, lakini mimi ni Diamond ninaweza
kufanya muziki na prodyuza yeyote naye
akaonyesha ufundi wake kupitia kazi yangu. Mwanaspoti: Shoo gani kubwa kuliko zote uliyowahi kufanya ambayo haijawahi kujirudia? Diamond: Diamond Forever. Hii ilikuwa kubwa sana ambayo sitakaa nikaisahau, ilihudhuriwa na
watu wakubwa na maarufu hapa nchini hata
hivyo ilikuwa ya kipekee ambayo haijafanana na
yoyote ile. Ya pili ni ile ya Dar Live ambayo nilifanya
baada ya kushuka katika helikopta ile pia ilikuwa
kubwa. Lakini kwa nje ya nchi ni Mombasa na Comoro huko nilifanya shoo kubwa sana ambazo
siwezi kuzisahau. Mwanaspoti: Ni shoo ipi iliyowahi kukuingizia pesa kubwa kuliko zote? Diamond: Shoo ile ya Mlimani City ya Diamond Forever, ile iliniingizia pesa kubwa sana na tangu
pale ndipo nilipoanza kufurahia matunda ya kazi
yangu. Nilifanya shoo pia Burundi, Mombasa na
Congo shoo hizi ziliniingizia kiasi kikubwa sana
cha pesa siwezi kutaja ni shilingi ngapi lakini ni
pesa nyingi ambazo sitakaa nizisahau. Mwanaspoti: Shoo ipi ilikuwa ya bei chee ambayo huwezi kuisahau Diamond: Kwa kweli siwezi kusahau nilipofanya shoo yangu ya kwanza kubwa mwaka 2009
kwenye Fiesta iliyofanyika Dar es Salaam, ilikuwa
ndiyo shoo yangu ya kwanza na kubwa wakati
huo nilikuwa natamba na wimbo Kamwambie,
ilinichukua muda mrefu sana kujiandaa mimi
pamoja na madansa wangu wanne tulilipwa Sh 50,000 lakini sikukata tamaa kwani ilikuwa ndiyo
mwanzo wangu wa kujuana na watu wengi na
wadau wakubwa wa muziki hapa nchini ambao
nilikutana nao kwenye ile shoo. Mwanaspoti: Kwa hivi sasa ni shoo gani ambayo unaweza kusema kwamba utafanya kwa bei ya
chini na ni shilingi ngapi? Diamond: Shoo ninayoweza kufanya kwa bei ya chini kabisa ni Sh 10 milioni za Kitanzania na hii
labda nione anayeniomba nifanye shoo hiyo
hayuko vizuri na pengine ni rafiki yangu na
hawezi kuninyonya, si hivyo tu itategemea pia ni
kampuni gani na ni watu wa aina gani ambao
watanitaka nifanye nao kazi. Mwanaspoti: Kwa kawaida Diamond ni msanii wa gharama gani kwa shoo moja ndani na nje ya
nchi? Diamond: Kwa kawaida shoo moja ninafanya kuanzia Sh15 milioni mpaka Sh20 milioni
kulingana na muda nitakaofanya shoo. Pia zile za
nje ninafanya kwa gharama ya Dola 20,000
mpaka 30,000 yaani ni Sh32 milioni mpaka 48
milioni hivi kwa fedha za Tanzania na nikiwa huko
nahakikisha ninafanya kazi vile inavyotakiwa. Lakini hali ni tofauti inavyokuja shoo ile ya
uwanjani yaani hapa nazungumzia shoo kubwa
zinazofanyika nje ya ukumbi, hizi natoza Dola
20,000 ambayo ni sawa na Sh32 milioni 32 kwa
fedha ya Kitanzania. Mwanaspoti: Kuhusu madansa wako unawachukuliaje? Diamond: Ni kama kaka zangu na ninawapenda sana kwani tumetoka nao mbali na wanajua kuwa
tunafanya kazi pamoja kutengeneza maisha hivyo
ni kama ndugu zangu na tunasaidiana kwenye
kila jambo ukizingatia kuwa kile tunachokipata
tunagawana. Kwa kweli najitahidi sana
kuwaambia hasa kuhusiana na masuala ya kimaisha, nahusika katika maisha yao ya kila siku
na nijuavyo mimi nikikosea tu mmoja akapotea
kundi langu litakuwa limeharibikiwa maana kila
mtu namtegemea kwa upande wake. Kwa sasa
wamejenga nyumba zao na wanaendelea vizuri
kimaisha hilo ndilo sharti langu lazima wafanye mambo ya maendeleo kwa kile tunachokipata. Mwanaspoti: Umesafiri nao nchi ngapi, na kwanini unapenda kuambatana nao? Diamond: Nimesafiri nao sehemu mbalimbali kama Burundi, Comorro na sehemu nyinginezo
ambako nimekwenda kufanya shoo, sina tabia ya
kusafiri peke yangu hata nikienda Ulaya na hata
Marekani lazima niwe nao. Ninapenda kuwa nao
kwani ni sehemu ya muziki wangu na imefika
wakati nimekuwa nataka mapromota kuhakikisha wanatulipia mimi na madansa wangu kwa ajili ya
shoo hasa tutakapojua kuwa shoo fulani itaingiza
watu wengi au udhamini mkubwa. Mwanaspoti: Kuna safari ambayo umewahi kusafiri peke yako? Diamond: Ziko nyingi, nilienda mwenyewe kutokana na ukubwa wa shoo, lakini ni miaka
kadhaa nyuma, baadaye nilijiwekea mikakati
kwamba siwezi kusafiri mwenyewe wakati shoo
nahitaji kufanya na madansa wangu, awali
mapromota walikuwa wagumu kunielewa na
wapo waliokataa. Niliachana nao na kuwataka wakishajipanga na kuhakikisha kwamba
wanaweza kunichukua mimi na madansa wangu
watafanya hivyo. Mwanaspoti: Umewahi kuwatema madansa? Diamond: Sijawahi kubadilisha madansa kwa sababu wanajua kazi yao. Ingawa nilikuwa na
madansa sita nilipokuwa naanza muziki lakini
niliachana na wawili kutokana na utendaji wao wa
kazi. Wawili hawa hawakuwa wabunifu kila siku
walikuwa na staili ileile, niliamua kuchagua vichwa
ambavyo vikikaa na mimi mwishowe tunatoka na kitu makini na chenye kueleweka. Kulikuwa na
tatizo pia la kukosea stepu wakati wa shoo hili
lilikuwa likinishushia sana hadhi yangu jukwaani,
hapo ndipo nilipoamua kuwaondoa. Mwanaspoti: Kwa upande wa malipo unawalipaje? Diamond: Ninawalipa vizuri lakini siwezi kutaja kiwango ila ingekuwa kwangu ningetaja, hiyo ni
haki yao wao wenyewe kutamka ila mimi siwezi
kutaja. Malipo ninayowalipa yapo machoni mwa
watu wanaowazunguka, dansa kujenga nyumba
kumiliki baadhi ya biashara si jambo dogo, hivyo
ninawalipa vizuri. Na hata gharama za kusafiri ndani na nje ya nchi vyote ni juu yangu, malipo
tunayoyapata tunagawana. Mwanaspoti: Unakumbana na changamoto zipi katika kazi yako? Diamond: Nakumbana na mengi, kwanza unapokuwa msanii unayeongoza lazima upate
vikwazo vingi. Nakumbana na watu wengi
wanaonichukia na kunitusi bila sababu za msingi,
hata hivyo nasingiziwa vitu vingi ambavyo havipo
nadhani hii ni changamoto iliyotokana na kufanya
vizuri katika muziki. Wapo ambao wanamwona Diamond anafanya
vizuri kwenye muziki badala ya kukaa na
kuangalia nimepita wapi na wapi anaanza kutoa
lawama kwamba ameibiwa na mengine ambayo
kimsingi hayana maana. Mwanaspoti: Siku za hivi karibuni kuna maprodyuza na wasanii wasiofahamika ambao
walijaribu kutengeneza kazi yako ya My Number
One na kukutusi kupitia wimbo huo na wapo
waliotunga mashairi mengine yaliyozungumzia
maisha yako kabla hujawa staa, ulijisikiaje? Na
unachukua hatua gani? Diamond: Awali niliumia sana nilipoibiwa mashairi ya wimbo wangu wa Mbagala, iliniuma sana kwa
muda wa wiki nzima uchungu nilioupata siwezi
kuuelezea. Lakini baadaye nilikomaa, huwezi
amini niliposikia zile nyimbo nilicheka sana kisha
nikawadharau sana watu waliofanya hivyo maana
nipo kwenye hii tasnia siwezi kuchukia watu wasiojua walitendalo kwani na wao wapo katika
kujitafutia riziki. Lakini hata hivyo sheria ya muziki
bado haijawa makini hapa nchini
nitachukua hatua gani mwisho wa siku nitaacha
kufanya mambo yangu ya msingi na
kushughulikia wezi wa kazi zangu ambao hata hivyo hawatabanwa kwa lile walilolifanya. Mwanaspoti: Msanii yupi hapa Tanzania anakutisha kama hayupo vipi huko nje ya nchi? Diamond: Kwa hapa Tanzania sijaona mwanamuziki anayenitisha, ila siwezi kujua
mashabiki wao ndio majaji, nafikiri kila mtu
anaweza kuwa na mtazamo wake. Kati ya
wanamuziki ninaowahusudu mimi kwa nje ya nchi
hasa Afrika ni P Square pekee, hawa wapo katika
nafasi kubwa sana kwenye ubongo wangu na nafikiria ni lini ninaweza kuwafikia, hiyo ndiyo
ndoto yangu daima. Mwanaspoti: Unapokuwa juu ya jukwaa unakumbana na vishawishi vipi ukiwa kama
msanii mkubwa? Diamond: Ninapata vishawishi vingi sana ninapokuwa jukwaani. Kwa kweli ninashawishiwa
na wakinadada, mfano kuna mwanamke mmoja
ambaye alikuwa mmoja wa mapromota wa shoo
nchini Uingereza alitaka kunibusu mdomoni kwa
lazima, kitendo kile kilinifedhehesha sana na
nilishindwa nifanyeje kwani nipo ugenini na jukwaani ilikuwa ngumu sana kwangu. Wakati
mwingine wanawake wanapanda jukwaani ili
wacheze na wewe mwisho wa siku wanaingiza
mikono kwenye suruali yaani sipendezwi kabisa
na michezo ya namna hii. Mwanaspoti: Umewahi kuibiwa ukiwa jukwaani? Diamond: Nimeshaibiwa sana hasa katika hizi shoo ndogo ndogo mara nyingi watu wanapanda
jukwaani na kuondoka na kitu chako.
Nakumbuka nimeshawahi kuibiwa saa, pete ya
dhahabu na kuna mmoja alitoa kali ya mwaka
yaani yeye alinivua nguo kwa lazima. Mwanaspoti: Inakuwaje nje ya muziki, unakumbana na changamoto zipi? Diamond: Kitu ambacho ni changamoto kubwa sana kwangu ni simu yangu ya mkononi. Kila
baada ya miezi sita au mitatu nalazimika kubadili
namba yangu ya simu, nasumbuliwa sana na watu
ambao hata hivyo hawana la msingi la kuniambia.
Ni kweli kwamba mawasiliano ni kitu cha msingi
na ninawapenda mashabiki wangu lakini namba
yangu inasambaa kwa kasi ya ajabu kiasi kwamba
nashindwa kupokea simu za maana kwa kudhani
kwamba na hao nao ni wasumbufu. Mwanaspoti: Ina maana milio yote ya simu hapo ni watu wanakupigia? Diamond: Yap, unavyoona inalia kila dakika watu wanapiga hapa. Muda mwingi hii simu ninaweka
'silent' yaani haitoi mlio wowote kwani inaita kila
dakika.
Mwanaspoti: Tuzungumzie uhusiano wako. Mpenzi
wako wa kwanza unamkumbuka? na je uliwahi
kumpa shilingi ngapi? Diamond: Mpenzi wangu wa kwanza kabisa enzi hizo ninajifunza mambo haya sikumbuki vyema
jina ila alikuwa anaishi Tandale na mimi pia
nilikuwa naishi huko na mama yangu. Sikumbuki
kama nimewahi kumhonga maana enzi hizo mimi
nilikuwa napewa tu na mama yangu pesa, sikuwa
na hela yoyote ya kumpa na ilikuwa ni kwa kipindi kifupi kama miezi minne hivi, hata hivyo tulikuwa
tunaibana tu kwa siri nilikuwa mdogo. Mwanaspoti: Kwanini mliachana? Diamond: Kwanza nilikuwa sijajua mapenzi ni nini. Hata hivyo haikuwa rasmi na wala nilikuwa sijawa
na akili ya kupenda sana na nilikuwa na fikra
kwamba ni mchezo tu hivyo tuliachana mapema
kwani hata yeye akili yake ilikuwa haijakomaa. Mwanaspoti: Mpenzi wako uliyekuwa naye kabla ya kuwa staa nasikia uliachana naye baada ya
kutoka kimuziki kwa nini? Diamond: Nilimpenda sana lakini aliniacha kabla ya kutoka. Mpenzi wangu wa kwanza alikuwa
anaitwa Sarah Sadick, sijawahi kumuhonga na
ndiye mwanamke niliyewahi kumpenda sana.
Wakati huo Naseeb Abdul kabla sijawa Diamond
nilikuwa nahaha kuhangaika ni vipi nitatoka
kimuziki. Msichana huyu ndiye aliyenipa hasira za kufanya muziki kwa bidii zote baada ya kunitema
na kuanza kuhangaika na wengine na aliniita
majina mengi yasiyo mazuri, kisa sina fedha. Si
kwamba nilimuacha bali yeye ndiye aliyeniacha
kama zali baada ya wiki kadhaa nikatoka na
wimbo Kamwambie, taratibu nikaanza kuwa staa naye akaanza kurudi ila nilishamuondoa moyoni
mwangu. Mwanaspoti: Kwa nini mliachana? Unadhani hakukufaa tena kwa kuwa ulishakuwa staa? Diamond: Alinisumbua sana kutokana na ugumu wa maisha niliokua nao kwa kipindi cha nyuma
hadi kufikia 2009. Nilimpenda sana huwezi amini
nilikuwa silali usingizi kwa ajili yake. Nahisi
ilitokana na mimi kukosa kazi ndiyo maana ilifikia
hatua alinipotezea. Lakini baada ya kupata na
kujulikana alinifuata lakini sikutaka tena hata baada ya kuniomba msamaha. Mwanaspoti: Umewahi kuwa na wanawake wangapi tangu uwe staa? Diamond: Sikumbuki kwa kweli wapo wengi mno, si unajua tena wapo walionitaka na
kunilazimisha nifanye hivyo, lakini idadi kamili
siwezi kukumbuka na kila siku nasumbuliwa na
hawa wanawake. Mwanaspoti: Ni wapenzi wangapi ambao umekuwa nao kipindi kirefu na kuwapenda kama
wapenzi wako? Diamond: Nimewahi kuwa na wapenzi wanne katika kipindi chote cha ustaa wangu na
sikupenda kubadili ovyo ila wengi wao
hawakuweza kutimiza haja ya moyo wangu. Mwanaspoti: Unaweza kuwataja majina? Diamond: Ndiyo ila wawili wanafahamika zaidi. Wa kwanza kabisa alikuwa anaitwa Sarah na wa
pili alikuwa anaitwa Hawa yule msichana
niliyeimba naye katika wimbo 'Nitarejea', huyu
alizidiwa ujanja na Wema Sepetu ambaye naye
alikuja kuondoka kwangu na baadaye nikawa na
Penieli Mungilwa. Mwanaspoti: Mwanamke yupi unahisi ulimpenda kuliko wote? Diamond: Mwanamke wangu wa kwanza Sarah Sadick huyu aliniingia sana moyoni sijajua ni
kwanini. Lakini nahisi huenda kwa kuwa awali
alinipenda kweli kwa kuwa wakati huo sikuwa na
kitu. Hata hivyo nahisi ilitokana na mimi kutokuwa
bize na wakati huo sikufikiria lolote zaidi ya yeye
ilitokana na kutokuwa na kazi ya kufanya. Siku hizi sina mapenzi ya kivilee, nawaza zaidi pesa na
ninaihangaikia na zaidi ni muziki wangu, hili ndilo
la kwanza kabisa linalonifanya niwe bize mapenzi
baadaye. Mwanaspoti: Umeshawahi kutongozwa na wanawake? Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya wanawake niliowahi kuwa nao
alinitongoza yeye mwenyewe ndipo nikawa naye
na nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu
tu. Wanaweza kumfikiria mwanamke fulani lakini
huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na
katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii, facebook, whatsapp,
Instagram na kwingineko na wapo wasichana
ambao wanatafuta namba zangu za simu na
kuanza kunisumbua. Mwanaspoti: Unapata usumbufu wowote toka kwa wanawake? Diamond: Ndiyo, wengi sana tena kuna mmoja kati ya wanawake niliowahi kuwa nao
alinitongoza yeye mwenyewe ndipo nikawa naye
na nilikaa naye katika uhusiano kwa kipindi kirefu
tu. Wanaweza kumfikiria mwanamke fulani lakini
huwezi amini ukweli ninao mimi mwenyewe na
katu hawawezi hata kumhisi. Ninatongozwa sana kwenye mitandao ya kijamii, facebook, whatsapp,
Instagram na kwingineko na wapo wasichana
ambao wanatafuta namba zangu za simu na
kuanza kunisumbua. Mwanaspoti: Ni mwanamke wa aina gani unataka awe mkeo? Diamond: Kwanza ninahitaji aijue kazi yangu na ajue kwamba mimi ni mtu maarufu hivyo
akubaliane na changamoto mbalimbali
atakazokumbana nazo kwa kipindi
atakachokuwa ndani ya ndoa, siyo siku mbili
anafungasha virago. Pia ajue kwamba nitamsikiliza
mama yangu kwanza kabla ya yeye hilo naliweka wazi, yeye ana nafasi yake katika maisha yangu
lakini mama yangu nimempa kipaumbele, tatu awe
tayari kuishi na mama yangu. Nne awe na akili na
mwenye utambuzi na atakayeniongoza katika kazi
zangu, sihitaji. Itaendelea…
 
Duuh interesting, ila hana privacy huy jamaa
 
Aisee huyu jamaa kichwa maji sana hana hata aibu muda mwingine.
 
Ya sirini anatoa ya bayana anaficha duuh kazi kweli kweli...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…