Mad Max
JF-Expert Member
- Oct 21, 2010
- 26,961
- 77,890
Kampuni ya magari kutoka China, Xpeng Motors, baada ya kufanya teaser kwa muda mrefu, hatimaye wamezindua P7+ EV leo tarehe 10 October.
Leo wakati wa uzinduzi, Xpeng walisema P7+ ni “World’s first AI car” na mauzo yataanza tar 14 mwezi huu October ila delivery itaanza November.
P7+ ina battery la (LFP) 60 kWh au 76 kWh inayokupa range ya 620 km au 710 km.
Design ya P7+ kwa nje iko sleek na imezingatia aerodynamics kupunguza wind resistance na Xpeng wanasema itakua na electric consumption ya 11.6 kWh kwa 100 km, ambayo kwa simple mathe ni kama 8.5 km/Kwh (unit) yaani unit moja ya umeme ya Tsh 360 unatembea kilometa 8.5!!!
Kwa ndani, kuna infotainment screen ya 15.6 inch, 2-spoke steering wheel, gear leaver ipo pembeni ya steering wheel na nyuma yake kuna cluster gauge ya LCD, pia iko na Eagle Eye autonomous driving system.
Kwa seat ya nyuma, kuna 8 inch screen na seat zina massage, na kuna meza ya kukunja.
Bei bado hawajatangaza officially, tunategemea kujua tar 14 mwezi huu kwenye Paris Auto Show (unyama upo hapa, usikose tutakua Live)