Ya Argentina yanatimia kwa TISS?

Yericko Nyerere

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2010
Posts
17,005
Reaction score
20,425
Tarehe 18 Januari 2015 Idara ya usalama ya Agentina ilituhumiwa kuhusika na mauaji ya mpelelezi binafsi bwana Alberto Nisman aliyekuwa akitaka kuanika madudu ya serikali hiyo ikiwemo ufisadi uliopelekea kulinda ugaidi wa Iran uliofanyika Agentina. Wairani walikuwa wamewahonga usalama wa taifa wa Agentina kwa vipande vya fedha ili wasiumbue Iran katika ugaidi huo uliotekelezwa katika kituo cha Kiyahudi kitwacho AMIA Jewish Community Centre" kilichomo mjini Buenos Aires Agentina.

Alberto Nisman akafanya uchunguzi, akagundua ukweli huo bila kuacha chenga ambapo sehemu ya ripoti hiyo ilimuhusisha rais wa zamani Cristina Fernández de Kirchner na ugaidi huo 1994, na kukazia kuwa rais aliitumia idara hiyo kuendesha mauaji ya raia wapinzani na wanahabari nchini humo. Rais wa Agentina wa miaka ya 2015 bwana Mauricio Macri nae akataka kuifutilia mbali kurugenzi ya ya ndani ya usalama ya Agentina kufuatia kashfa hiyo ambayo ilikaribia kuhatarisha mamlaka yake ya urais na nchi kwa ujumla. Jamaa wa Usalama kuona hivyo, wakamuua mpelelezi siku moja kabla hajawasilisha ushahidi wake bungeni bungeni ili aanike ukweli.

Bunge la Agentina baada ya kuona hali hiyo, likamualika Mkurugenzi wa zamani wa Usalama wa Taifa wa Agentina ili awaeleze utendaji wa taasisi hiyo. Ilikuwa afanye kazi hiyo Jumatatu. Naye leo ametekwa, hajulikani alipo. Sasa bunge likavunja Usalama wa taifa wa Agentina kwa sababu ya vitendo vya udhalimu na kuliunda upya kwa weledi kabisa...

Hali ya Agentina haina tofauti na ya Tanzania. Usalama wa Raia umekuwa jambo tete sana Kama ilivyokuwa Agentina ambayo maafisa usalama wanawekea vinasa sauti wanasiasa na kuwahujumu, kuwapiga na kuua wanaharakati, wanasiasa, na wanahabari. Uhuru wa kutoa maoni ulizimwa kabisa. Tanzania nayo iko hivyo (rejea mauaji ya kisiaaa, wanahabari na wanaharakati).

Fundisho kubwa kwa Tanzania ni wakati sasa wa kufanya marekebisho makubwa ya idara ya Usalama nchini na kuhakikisha uhai wa kila Mtanzania na kila mtu unalindwa na kuthaminiwa. Rais na Bunge la nchi yetu simameni mulimlike taifa kwa jicho la tatu.

Kwanini ripoti ya uchunguzi wa mauaji nchini ya Kamati ya Bunge iliyoongozwa na Mwenyekiti wake Mh Adadi Rajabu mwezi uliopita ilinyofolewa sekundu chache kabla ya kuwasilishwa bungeni? Nani aliratibu unyofoaji wa ripoti hii? Ana maslahi gani na mauaji haya?

[HASHTAG]#KitabuUjasusiwaKidolanaKiuchumi[/HASHTAG]


Na Yericko Nyerere
 
Kwa hiyo inawezekana usalama wa taifa umehongwa kufanya hiki tunachokinshuhudia? Je huenda lia kukawa na mkono na baraka za Rais wetu? Kama hakuna mkono wake juhudi zake kuliokoa taifa ni zipi?
 
Daah mazingira na wakati, mkuu subiri wanakuja watakudadavulia.

Sasa kama katika Jina tu anakosea hivi je tutamuamini vipi katika hayo mambo Nyeti na Muhimu ya ' Kiusalama ' anayojitutumua kutwa kuyajadili humu? Mtu aliyeiva kweli Kiintelijensia / Kijasusi huwa hafanyi makosa katika kila Kitu chake na huongozwa sana na umakini usio na hata chembe yoyote ile ya shaka.
 
Muda mwingine inabidi tukubali tu kuwa kuna vitu vimetuzidi uwezo wa kuvijadili
 
Kwa idadi kubwa ya wabunge vilaza tulionao sioni tofauti yoyote wala tumaini la kuvunjwa idara hii
 
Acha ujinga jina tu haliwezi kuwa hoja unaijua mother tongue yake? jibu hoja si blahblah za majina
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…