Ya CCM Dodoma hayatuhusu yetu ni Katiba Mpya

Ya CCM Dodoma hayatuhusu yetu ni Katiba Mpya

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Yatuhusu vipi ya hawa na barakoa zao?

IMG_20220401_162659_273.jpg

Au ya huyu na wahuni wake?

IMG_20220401_162632_898.jpg

Muhimu tutambue:

1. Wananchi walio wengi wanataka katiba mpya isipokuwa wenye maslahi binafsi na iliyopo.
2. Katiba Mpya haitapatikana kwa miito ya mitandaoni au maneno pekee.
3. Katiba Mpya haitapatikana bila ya watu (sisi) kuingia barabarani na kuidai kwa vitendo.

IMG_20220331_111155_045.jpg

Ukweli mchungu bila kuwepo na uongozi wa mfano kuwafikisha watu barabarani, #3 pale itabakia kuwa ndoto.

Shime waungwana Katiba Mbovu tuliyo nayo ndiyo chanzo cha matatizo yetu kama nchi.

Hayawezi kuwapo matunda bila jasho.
 
Hata hao walioko kwenye huo mkutano wengi wao hawako huru, wanalazimishwa kushangilia kila akitakacho mwenyekiti wao, hivyo naona ili nao waondokane na huo utumwa wa kumsifia mwenyekiti wao kama mungu mtu, nao wanaihitaji Katiba Mpya kama watanzania wengine wote.

Wasijidanganye na hizo uniform walizovaa.
 
Hata hao walioko kwenye huo mkutano wengi wao hawako huru, wanalazimishwa kushangilia kila akitakacho mwenyekiti wao, hivyo naona ili nao waondokane na huo utumwa wa kumsifia mwenyekiti wao kama mungu mtu, nao wanaihitaji Katiba Mpya kama watanzania wengine wote.

Kwa hakika hata huko CCM wanaohitaji Katiba Mpya wapo na si wachache. Utimilifu wa kauli ya kuwa - wananchi walio wengi wanataka Katiba Mpya.

Tulipo wanasubiriwa waanzilishi. Waswahili wakiita - nani mwenye kumfunga paka kengele. Walio na utayari wa kulipa gharama.

Ukombozi haujawahi kukosa gharama zake kwa kesho iliyo bora zaidi.
 
Back
Top Bottom