Ya Clatous Chama yananikumbusha ya Juan Mata

bryan2

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2016
Posts
3,323
Reaction score
4,679
Anayokumbana nayo Clatous Chama amenikumbusha pia aliyowahi kukutana nayo pia Juan Mata chini ya Jose Mourinho, Game na Mbeya city kwenye Dk za mwanzo Chama alitolewa na kwenda kupumzika kwenye mbao ndefu na kuleta hali ya sintofahamu kwa mashibiki wa Simba.

Juan Mata naye aliwahi kukutana na kadhia kama hii akiwa pale Chelsea ni baada ya kutoingia kwenye mfumo wa kocha wa Kireno mwenye maneno mengi Jose Mourihno na kumpekea kumpiga mnada ambapo alielekea pale Old Traford scenario zinafanana ila bahati mbaya moja imetokea wanapofahamu maana ya mpira na nyingine imetokea wanapoendeshwa na mihemko zaidi.

Jose alikua anataka watu wanaokimbia kila mara kiwanjani na kuwasumbua wapinzani wanapokua na mpira au hawana watu jamaii ya Michael Essien, Msambaa yule Ramires,John Obi, Lampard et al bila kupepesa macho Jose alisema Mata ni mchezaji mzuri ila kwenye mfumo wangu haingii tatizo lake likiwa ni mvivu kukaba.

Mbeya City vs Simba ile gemu nliicheck kipindi cha kwanza Mbeya city walidictate sana eneo la kati ila baada ya Chama kutoka Simba ikaanza kumiliki mali na timu kusogea mbele.

Ushauri wanaSimba kuweni wapole kila mtaalamu i mean kocha ana mifumo yake na kupenda kutumia wachezaji flani mambo ya sijui Kocha ndio aingie kwenye mfumo wa Kocha hakuna kitu kama hicho kwenye futball.
 
Pamoja na kutoka chama wala Simba haikukamata gae, shida ya simba ni pale kati, jana wamecheza na dodoma jiji, chama hata benchi hayupo lakini timu imepata tabu mnoo.
Tatizo la Simba SC Ni zaidi ya chama
 
Lakini Morinho huyo huyo alipoenda Man U akamkuta tena Mata na akaingia kwenye mfumo wake.
 
Tatizo la Simba SC Ni zaidi ya chama
Hakuna mchezaji mkubwa zaidi ya timu, nakubali hili.
Ila shida si chama, nimekkupa mfano jana chama hakuwepo timu ilitulia si Dodoma jiji ndio wakawa simba kisha simba ttukkawa dodoma jiji.
Hata game aliyotolewa bado timu haikutulia
 
Labda kocha atakuwa amegundua Chama ni kiungo konokono.
 
Chama haingii mifumo ningi ya makocha, Simba tu ujinga WA kumpa heshimauchwara.
Amini chama akienda tumu yyye Ile nje ya Tz haezi fanya chchte namna anavocheza haez ingiliana na mifumo ya walimu wengi na mahitaji ya timu.
Nihapo tu Kwa makolo ndo wanamuona mungu mtu.

Kama anaweza wamuuze na wamfatilie watagundua hajui kitu.
 
Mbeya City vs Simba ile gemu nliicheck kipindi cha kwanza Mbeya city walidictate sana eneo la kati ila baada ya Chama kutoka Simba ikaanza kumiliki mali na timu kusogea mbele.
Sio kweli. Siku zote mpira ni mchezo wa makosa, wachezaji kama Kibu, Kyombo na Kapama wanafanya makosa mengi kiasi yanaighramu Sana timu. Kilichobadilisha kidogo ni juhudi binafsi zawachezaji ikiwa pamoja na Sakho ambaye akiwa na mpira ima afike golini au afanyiwe faulo.

Wana Simba hatukuwa na shida kuingia Sakho lakini hatukuona sababu ya Sakho kuchukua nafasi ya Chama kwani tulitaka Chama na Sakho wacheze pamoja ili washirikiane vema na Saidoo.

Kibu Denis ndiyo kwa siku za hivi karibuni amekuwa akiigharimu timu kutokana na kukosa hata maarifa kidogo ya kiuchezaji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…