Nasri A Kulemba
Member
- Oct 16, 2015
- 20
- 56
YA CRISTIANO RONALDO NA MANCHESTER UNITED,NA UFUMBUZI KATIKA FUMBO LILILO GUMU.[emoji3576]
kalamu ya Nasri Kulemba [emoji3578]
Kile alichosema Cristiano Ronaldo dhidi ya waajiliwa wake Manchester united ,ni tarajio lililokua linasubiliwa na wapenzi wengi wa kandanda.
Tatizo sio kubaki Manchester united,hii ni klabu inayompa kila kitu katika maslahi anayohitaji pamoja na heshima ,anapata kila kitu ,tatizo ni hadhi na hali ya kiushandani iliyonayo Manchester United kwasasa.
Kuna msemo maarufu unaosema pesa sio kila kitu ,unaweza kuwa na pesa ila usiwe na furaha ,kila kitu Cristiano anacho lakini kwanini anataka kuondoka Manchester united !!?.
Jibu ni rahisi tu ,Ronaldo hataki kuindosha hadhi yake mapema ,imani yake inamwambia yeye bado ni mshindani,anahitaji kufanya zaidi kuendelea kuwa mkubwa ,anahitaji kuendeleza kuweka records mbali mbali .
Ronaldo ni mkubwa kwenye brand ,nyuma yake kuna makampuni binafsi anayoshilikiana nayo ,itakua ni anguko kubwa kama balozi ,kipindi ambacho mpinzani wake anacheza Uefa champions league yeye akiwa europa league ..kibiashara hii itaaharibu taswira .
Hasa kipindi hichi ambacho anahitaji zaidi wadhamini hao kuliko kitu chochote kwenye kuingiza kipato ,zingatia umri wake na kile alichokifanya ..anakila kitu binafsi ;nguvu yake sio ile katika kucheza soka .
Kwasasa anachohitaji ni kupiga pesa kupitia jina lake au kwa kile alichokifanya ,Cristiano haitaji hakikisho la kucheza zaidi uwanjani ,anahitaji hakikisho la kuendelea kujiuza kutokana na mafanikio ya uwanjani;na hapa ndipo suala la kujiuza linapochukua sura mpya .
Unajiuza ukiwa katika mazingira gani ;wapi na je wale waliopo nyuma yako watapta faida kupitia eneo uliopo!.Manchester united kwasas sio sehemu salama kwa upande wake hasa biashara anazofanya nje ya uwanja .
Kutokana na hili ndio sababu iliyowafanya watu wengi wawe na wasiwasi ni vipi Ronaldo ataendelea kubaki United ,Ronaldo anahitaji timu iliyo imara ili kuendelea kujiuza na sio timu ambayo inahutaji ubora wake ili iwe imara .
Cristiano Ronaldo wa miaka Nane nyuma alikua anauwezo huo ,kupitia yeye timu itapata faida ,ila kwasasa nguvu imepungua, anahitaji msaada wa vijana imara kwenye kikosi ili kuwa bora .
United kwasasa wapo kwenye ujenzi mpya chini ya Ten Hag ,katika ujenzi kuna mawili,kuwahi kufika lengo au kuchelewa .Hivyo ni lazima uhitaji wachezaji vijana wengi kwenye kikosi kilicho na mchanganyiko wa wachezaji wachache wenye uzoefu na ubora kama Cristiano.
Kwao United project yao inafaida wakiwa na Ronaldo,kupitia yeye watapata faida ya haki za mauzo na kupitia wale vijana watafikia lengo la ujenzi wao ..lakini je Ronaldo atakubali utiifu kwenye ujenzi huo !!! atakubali kuwa kwenye timu iliyo na vijana ambao hwajulikani ni lini watakua bora .
Sio rahisi kwa cristiano Ronaldo;anahitaji project yenye uwekezaji mkubwa wa muda mfupi kwasababu yeye ni mshandani,hivyo itawalazimu United kuingia sokoni na kumwaga pesa .
Kwa upaande wake Ronaldo ujenzi huu unafaida gani ikiwa kama utachelewa ..?hali yake kibiashara itakueaje ,hali yake ya matamanio kuendelea kuweka record zaidi itafikia lengo .
Ronaldo kuendelea kubaki United ni suala la kujitoa muhanga ,kuna mawili aidha apotee moja kwa moja maana haijulikani ni lini hiyo project itakaa sawa ,lakini pia kuibuka shujaa na kutengeneza kitu kipya ikiwa ujenzi huo utatoa matunda kwa nyakati za mapema .
Lakini kupitia maslahi yake binafsi naona ameamua kuondoka ,na hili jambo ndio lililua linatuumiza vichwa kumuona Ronaldo mshindani ndani ya manchester united iliyokosa muelekeo ,ni fumbo lililokua gumu sana .
Kwa upande wa United watapitia mambo makuu mawili ,kwanza ni kukosa pesa kutokana na haki ya jina la Ronaldo(Uchumi ) nje ya uwanja watapa hasara hasa kwenye kipindi hichi cha ziara za timu kwenye pre season, uuzwaji wa jezi pamoja na haki za matangazo ya mudhui katika michuano mbali mbali .
Eneo hili pekee ndio Manchester united wanapaswa kujutia ,lakini eneo la pili naiona United wakitengeneza project yao salama na kwa uhuru bila uwepo wa Ronaldo ,watafanya mikakati yao kwa ufanisi kwasababu hawatakua na mchezaji ambaye uwepo wake utawafanya kuwa kwenye plesha ya ushindani .
Uwepo wa Ronaldo utawafanya United wasipite kwenye maono waliyonayo na watahitaji kununua wachezaji wakubwa ili kumlidhisha cristiano ,na hapa ndipo watakapo bugi ..
Kwasasa United wanahitaji kutengeneza Falsafa za kiuchezaji (system of play ) ndipo baadae wasajili wachezaji watakao fiti katika falsafa ..Project yao inahitaji falsafa kwanza kisha wachezaji … uwepo wa cristiano utahitaji wachezaji kwanza kisha falsafa.
Kupanga ni kuchagua,United kama watanendelea kubaki na Cristiano basi watambue project yao inaweza isifanikiwe ,lakini kwa upande wa Ronaldo kama atakubali kuendelea kubaki united atambue hadhi yake ipo mashakani kutoweka ghafla au mapema na kujikuta anamaliza vibaya nyakati zake .
Najua united wanamuhitaji sana Ronaldo kwa ajili ya kibiashara na msaada wake wa mabao ,lakini uwepo wake utakua ni faida ya muda mfupi sana kuliko kama wataamua kuachana nae kwa faida ya baandae ya muda mrefu yenye manufaa enedelevu.
Kama wameamua kuanza upya,huu ni wakati wa kufanya maamuzi magumu.kila mtu anatakiwa achukue njia yake kwa ajili ya kufanyikisha ndoto anayoitarajia.
Wasalam ..
[emoji404] instagram nasri kulemba