Ya Erick Kabendera, kifo cha Ben Saanane na kisa cha mfalme mwenye masikio marefu kama ya punda

Ya Erick Kabendera, kifo cha Ben Saanane na kisa cha mfalme mwenye masikio marefu kama ya punda

LIKUD

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2012
Posts
18,037
Reaction score
33,681
Palikuwa na mfalme mwenye masikio marefu kama ya punda. Siku moja mfalme alimuita kinyozi amnyoe nywele zake lakini asitoe siri kwa atakacho kiona.

Kinyozi alipo mnyoa mfalme akaona mfalme ana masikio marefu kama ya punda. Kinyozi alijizuia sana asicheke wakati anamnyoa mfalme.

Na alipo fika nyumbani alijizuia sana asitoe siri hiyo kwa mkewe.

Hatimae uzalendo ukamshinda akaenda porini akachimba shimo dogo kisha aka whisper " mfalme ana masikio marefu kama ya punda"

Baadae sehemu hiyo paliota mti. Mti ule ukashindwa kuzuia siri hiyo. Kila upepo ulipo vuma yalisikika maneno " mfalme ana masikio marefu kama ya punda"


Siku moja mwanakijiji mmoja alienda kukata kuni msituni akasikia mti unatamka maneno " mfalme ana masikio marefu kama ya punda".

Mwanakijiji alistaajabu sana akaenda hadi kijijini na kuwaambia wanakijiji wenzake kuwa kuna mti unatoa maneno ya ajabu.

Baadae wanakijiji wakaenda hadi kwenye mti huo kuthibitisha maneno ya mwanakijiji mwenzao na kweli wakakuta mti unaongea maneno hayo.

Habari hizo zilisambaa kijiji kizima na hatimae zikamfikia mfalme.

Mfalme akasema kweli duniani hakuna siri.

.......

Back to kibendera na Madai yake kuhusu Ben Sa8 kupigwa risasi na " mfalme"

Kama asemacho kuhusu Ben ni kweli basi haihitaji nguvu nyingi sana kujua habari hizo zili mfikia vipi Kabendera.

Mtu au watu walio shuhudia tukio hilo walishindwa kukaa na siri hiyo wakaitoa kwa watu wao wa karibu na watu wao karibu wakaitoa kwa watu wao mpaka habari ikafika kwa Kabendera...

Tukio kama hilo hata Mimi Binafsi nisinge weza kubaki nalo moyoni.


Hii ni kwa wale wanao uliza swali Kabendera alipataje taarifa hiyo.

As a matter of fact tetesi hii ilikuwa inavuma tangu enzi za mwendazake sema ndo hivyo watu walikuwa wanaiongea kwa sauti ya chini. Kabendera amekuja kuiconfirm

Naomba Msiunganishe Uzi huu
Moderator
 
Back
Top Bottom