Ya kichina Makubwa

TIMING

JF-Expert Member
Joined
Apr 12, 2008
Posts
28,186
Reaction score
15,549
Hii tabia ya wadada kupaka mijitako ya kichina inaniboa sana.... unakuta bonge la toto kumbe manufactured bwana, si bora hizo dawa tupake ng'ombe na mbuzi ili tuuze nyama nyingi??

Jana ndani ya mwanza, hamasa nikaingia,
Nikaona ni ya kwanza, ya china kining'inia,
moyoni nikajikwaza, wazo baya lanijia,
hizi dawa za kichina, ni bora tupake mbuzi

ni bora tupake mbuzi, tena makalioni
na pia pale mbavuni, bila kosa ugimbini
mbuzi kunona budi, kapo paja lithamini
tukiwapaka na mbuzi, basi mauzo yatenda juu

mauzo yatenda juu, tukiwapaka na mbuzi
tuuze kilo za juu, kuzidi na kumi hizi
tupate pato la juu, na si kukuza mashuzi
na warembo kwa makuu, waache kujifitizi

waache kujifitizi, na mitako ya kichina
wanakua kama ndezi, bada muda na huchina
wamwfanywa wapuuzi, kupaka ya kichina
warejee kwenye necha, midawa wawape mbuzi
 

Cousin hii ya leo kali nimecheka mpaka basi hakyanani:biggrin1::biggrin1::biggrin1:
 
Kaka yangu visa vyako huwa haviishi kuna makubwa yapi yamekukuta Mwanza (Carlfornia)
 


hata mbuzi asiwape,wawape wenyewe wachina,mbona wao wako bapa wkt dawa yatoka jikoni mwao.
 
hahahahahahah!
ngoja niwahi chemba
 
Mkuu utunzi wako una uhusiano wowote na valuu??? au nyagi?
 
Cousin hii ya leo kali nimecheka mpaka basi hakyanani:biggrin1::biggrin1::biggrin1:
Hakyanani kazin hali nimbaya... mijitu inajitutumua utafikiri baluni bwana

kumbe tungepaka ng'ombe tungeuza sana tu
 
hata mbuzi asiwape,wawape wenyewe wachina,mbona wao wako bapa wkt dawa yatoka jikoni mwao.
si ndio hapo sasa

vichina vyenyewe bapa ka tv-plasma, kazi kudanganya dada zetu tu
 
hahahahahahah!
ngoja niwahi chemba
karibu sana, nishaagiza napanga kuanza kuomba anti infii combatants kuja kunisaidia kufukuza mashetani
 
Inasikitisha sana,na hii ni kwa wabongo zaidi!! sasa nashindwa kuelewa kuwa hatujiamini kiasi hiki!coz kama Mungu hajakupa hips/makalio kuna kingine cha thamani umepewa na uzuri si hips/makalio peke yake!
Anyway,labda wameona wanaume wakibongo wanapenda hapo zaidi
 

Kaka ungeambatanisha na picha ya mrembo mwenye ya KICHINA ingenoga zaidi
 

Beauty and pride ni perception... we hebu fikiria..

nywele za kununua, na meno ya kubandika
minyusi ya kuchonga, na kope za kubandika
na mat@ko ya kichina, na kucha ni za bandika
nazo nyonyo za kupampu, na tumbo limekaushwa

balaah wallahi!!!
 
ni bora tupake mbuzi, tena makalioni
na pia pale mbavuni, bila kosa ugimbini
mbuzi kunona budi, kapo paja lithamini
tukiwapaka na mbuzi, basi mauzo yatenda juu

Acidi navunja mbavu,
Natena sina ubavu,
Makalioni na mbavu,
Hakuna huko minofu!

Makalio binadamu
Kwa mbuzi hayo adimu
Nakupa hiyo elimu
Ujue yalo muhimu!

Kwa mbuzi ni mapajani
Minofu inasheheni
Halafu tena shingoni
Kwingineko kifuani!

Huko kote kunanona
Pasipo hata mchina
Noma nasema wachina
Tuwache hao watwana!
 
Beauty and pride ni perception... we hebu fikiria..

nywele za kununua, na meno ya kubandika
minyusi ya kuchonga, na kope za kubandika
na mat@ko ya kichina, na kucha ni za bandika
nazo nyonyo za kupampu, na tumbo limekaushwa

balaah wallahi!!!

No further comments, umemaliza kila kitu mkuu wangu
 

Message delivered!
 

sikatai sikatai, bali najiwazisha
ya kichina hayafai, hata uwe ni basha,
na kwambuzi hayafai, ni hayana bashasha
hili swali nauliza, kwanini mwatukwaza?
 
naskia kuna meno ya kuvaa siku hizi

balaa, mtu akiiondoa spare zote ukimcheki unazimia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…