Ya Mungu mengi ila Dunia ina mengi pia

Au ndo wewe mheshimiwa Waziri Wakutwanga na kukoboa uliingia mjengoni na miwani halafu arest in peace akakutumbua mara moja
 
Hayo mambo yapo kama huamini amini yapo
 
Sonona ni dalili mbaya ya ugonjwa wa akili
 
Nini kilichompeleka?

Kuna habari za udaku zinasema kilikuwa kifungo cha aina yake, cha kujihukumu mwenyewe, cha nyumbani, kimya kimya.

Alimcezea simba sharubu, akaparazwa na kucha kidogo.
Bila shaka ni baada ya kukoswakoswa na ile kitu wanayochimba kule Zambia.
 
Natumaini afya yako imeimarika. Nimekusoma, na kupata ufahamy kuwa umekuwa kwenye mfumo wa uongozi wa nchi hii tangu kuzaliwa kwako.
Unapompa kijana uliyemjibu hapa 'Pole ya kuwa mzalendo', na kwamba nchi ina njia ndefu ya kupita, una maanisha nini hasa? Na je unafikiri hii nchi itafika huko inapotegemewa kwenda?
Na hapa nakuchukulia wewe na familia yako kama ndio mliobahatika kuwa juu, elimu nzuri, nje ya nchi, ukarudi nchini, usiwe wa ufanisi wowote, bali kupachikwa hapa na pale, na hata uzi huu unamlaumu rais kwa kukuahidi atakupachika sehemu na haikutokea n.k.
Ndio kusema nchi iko mikononi mwa watu wa aina yako, na kwa kuwa katika hilo kundi, una maoni kuwa nchi ina safari ndefu ya kokote kule mnakoipeleka?
 
Rafiki Auz hauniulizi ila ila unajijibu , pole rafiki ukweli unaujua ila tunaupindisha , i believe ipo siku Tanzania itasimama tena ila jua kuna vizazi vingi vijavyo

Nisamehe kwa ukweli mchungu ila inanibidi niyaseme niwe huru , ukweli ni kuwa raisi tuliyenaye sasa ni mtu wa kuitoa Tanzania sehemu moja kwenda kwingine ila shida amezungukwa na wabaya .

Tuishi humo , nchi ni yetu sote rafiki.
 
Bila shaka ni baada ya kukoswakoswa na ile kitu wanayochimba kule Zambia.
Haikufikia huko.

Vijana wake walishikwa kikomando wakiwa kwenye misheni "red handed" na zana zote. Wakawekwa mtu kati, wakabwabwaja yote kinagaubaga.

Watu waliporidhika na maelezo yao, wakapiga simu ya moja kwa moja, ambayo baada ya kuipokea akastaajabu sana vipi aliyempigia kaijuwa namba hiyo. Akaambiwa, ongea na vijana wako, akaongea na kiongozi wa hao vijana.

Baada ya hapo akaulizwa, vipi, kazi imekushinda?

Mengine ndiyo kama juu huko. Majumba makuu yakawa hayakaliki kabisa. Moto.

Waswahili tunamsemo "usione vinaelea, vimeundwa".
 
Lilikuwa jambo ambalo nahisi kwa roho yake na vile alikuwa anajiona yuko juu ya kila kitu hakuamini .

Safari yake ya pacemaker kuanza kusumbua ilianzia hapo maana presha juu ,kila uchwao maana kwenye akili yake ilikuwa haimithiriki kama yale yanaweza kumkuta yeye akiwa kama namba moja.
 
Nafikiri hawakuwa na strategy vijana wake. Walitumia nguvu nyingi akili chache. Ila hizi ni hekaya tu. Mambo hayapo hivyo kama anavyosimulia FaizaFoxy

Yaani ujue mpaka maswali eti akaulizwa kazi imekushinda?[emoji23][emoji23][emoji23] ni hearsay tu ambazo ni miongoni mwa nyingi zilizotapakaa.
 
Isn't this just a hearsay Sir? Is it fact? In accordance to your view.!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…