Ya MVIWATA yapo gizani, ya Bashiru ndio yanapigiwa kelele

Rufiji dam

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2020
Posts
4,107
Reaction score
9,671
Msukuma na Kibajaji hawa ni watu hatari sana kwa ukomavu wa majadiliano yenye afya. Ukiona hawa watu wameibuka ujue kuna jambo ambalo Wananchi linawagusa, Balozi Bashiru kasema yake, huyu anatabia ya kusema ukweli japo sio mwanaCCM huyu.

Anahoja ya maana sana hapaswi kutishwa, na ujinga huu wa akina Kibajaj unamuweka Rais wa Tanzania kama vile sio mtu wa kawaida hapaswi kusemwa.

Bashiru kaitwa na Wakulima hawa ndio wenye nchi yao hata hao CCM wanajua kabisa nembo yao ina jembe na nyundo! Sijui nani aliweka laana ya jembe la mkono na lile linyundo maana tunataabika tu.

Wakulima wameongea lakini madai ya Wakulima hata hayasikiki tena hata Mavunde na Bashe nao hata hawajitokezi kuyasemea ya wakulima wamekaa nao kumfuatilia Bashiru tu. Tunapaswa kuyajadili matamko ya Mviwata pia na sio ya Balozi tu.
 
Msukuma na Kibajaji hawa ni watu hatari sana kwa ukomavu wa majadiliano yenye afya. Ukiona hawa watu wameibuka ujue kuna jambo ambalo Wananchi linawagusa, Balozi Bashiru kasema yake, huyu anatabia ya kusema ukweli japo sio mwanaCCM
Wakulima wameongea lakini madai ya Wakulima hata hayasikiki tena hata Mavunde na Bashe nao hata hawajitokezi kuyasemea ya wakulima wamekaa nao kumfuatilia Bashiru tu. Tunapaswa kuyajadili matamko ya Mviwata pia na sio ya Balozi tu.
Jukwaa hili haliishi kustaajabisha.

Ukidhani umekwishayaona yote, na kuwaona wote wanaochangia humu na kudhani unawajuwa wote vizuri, mara anaibuka mtu ambaye hata hujawahi kumsikia wala kumsoma.

Mkuu 'Rufiji dam', nakupa 'Heshima', mkuu kwa mada inayogonga penyewe hasa!

Wengine tumebaki tukishangilia au tukilaani kelele za hawa wasio na akili kichwani, akina Lusinde, Msukuma, Kagwangwala na wengine wa aina hiyo, kumbe tunasahau mambo muhimu kabisa tunayotakiwa kuyajadili.

Kwa mfano: imekuwaje hadi hawa wakulima wakaona bora kumwalika Bashiru, na wasiwaalike hao wengine? Bila shaka wakulima walikuwa na agenda maalum iliyowasukuma hadi kufanya uamzi wa namna hiyo.

Mimi ningependa pawepo na makundi mengine mengi zaidi yenye ujasiri wa kufanya maamuzi kama hayo ya wakulima.

Tukienda kwa mwendo huo, Tanzania yetu itapona.
 
Kibajaji, msukuma na UV CCM wao wanamtetea mwenyekiti wao kwamba asifiwe na hawana muda wa kumtetea mwananchi
 
Sina maana mbaya ila Kuna matukio yanaidhihirisha jinsi CCM walivyokuwa wajinga na wapuuzi wa kutupwa, kinachosasitiri ni zile nguo za Kijani kama matembele. Ni kweli hakuna hata Waziri wa kilimo aliyejitokeza kujibu au kuwafariji Wakulima zaidi NASIKIA wamepigwa mkwara Next time wawe makini.

Pia NASIKIA wametoa Statement ya kuyakanusha yaliyosemwa, yaani pamoja na vigelegele vyote vile wamevikana....
 
Msukuma na Kibajaji hawa ni watu hatari sana kwa ukomavu wa majadiliano yenye afya. Ukiona hawa watu wameibuka ujue kuna jambo ambalo Wananchi linawagusa, Balozi Bashiru kasema yake, huyu anatabia ya kusema ukweli japo sio mwanaCCM huyu.

Anahoja ya maana sana hapaswi kutishwa, na ujinga huu wa akina Kibajaj unamuweka Rais wa Tanzania kama vile sio mtu wa kawaida hapaswi kusemwa.

Bashiru kaitwa na Wakulima hawa ndio wenye nchi yao hata hao CCM wanajua kabisa nembo yao ina jembe na nyundo! Sijui nani aliweka laana ya jembe la mkono na lile linyundo maana tunataabika tu.

Wakulima wameongea lakini madai ya Wakulima hata hayasikiki tena hata Mavunde na Bashe nao hata hawajitokezi kuyasemea ya wakulima wamekaa nao kumfuatilia Bashiru tu. Tunapaswa kuyajadili matamko ya Mviwata pia na sio ya Balozi tu.
Bashiru alikuwa mshirika na muasisi wa mateso, matendo maovu kama kuua kuteka, kutesa, kubambikia kesi yaliyotokea ETC, ETC, ETC wakati wa magufuli. Aliunga mkono udhalimu, uvunjjaji wa haki za msingi za binadamu, sheria na katiba na hivyo leo anapojifanya kupinga hayo baada ya kukosa madaraka, LAZIMA AANDAMWE, ASEMWE ALAANIWE na yote yanayosemwa sasa hivvi. BASIRU IS A TRAITOR NUMBER ONE
 
Jamani hawa wakulima wanaonekana kwenye kupiga kura tu
 
Jukwaa hili haliishi kustaajabisha.

Ukidhani umekwishayaona yote, na kuwaona wote wanaochangia humu na kudhani unawajuwa wote vizuri, mara anaibuka mtu ambaye hata hujawahi kumsikia wala kumsoma.

Mkuu 'Rufiji dam', nakupa 'Heshima', mkuu kwa mada inayogonga penyewe hasa!

Wengine tumebaki tukishangilia au tukilaani kelele za hawa wasio na akili kichwani, akina Lusinde, Msukuma, Kagwangwala na wengine wa aina hiyo, kumbe tunasahau mambo muhimu kabisa tunayotakiwa kuyajadili.

Kwa mfano: imekuwaje hadi hawa wakulima wakaona bora kumwalika Bashiru, na wasiwaalike hao wengine? Bila shaka wakulima walikuwa na agenda maalum iliyowasukuma hadi kufanya uamzi wa namna hiyo.

Mimi ningependa pawepo na makundi mengine mengi zaidi yenye ujasiri wa kufanya maamuzi kama hayo ya wakulima.

Tukienda kwa mwendo huo, Tanzania yetu itapona.
Kalamu: kama nchi imepotea kbs, kitendo cha kuwaacha wakulima hewani sio kizuri kbs. Lini tutajua matatizo yao! Matokeo yake wamewageuza kuwa waandamanaji na kumpongeza Samia.
 
Back
Top Bottom