patrickrugera
New Member
- Jul 24, 2022
- 1
- 1
Uwepo wa magonjwa katika jamii zetu si jambo la kushangaza. Bali ni hatari sana kugundua baadhi ya magonjwa hayo yakiwa ni tishio zaidi katika miaka ya sasa kutopewa kipaumbele.
Magonjwa ya akili ni matatizo ya ubongo ambayo humfanya mtu kuwa na hisia, fikra na matendo tofauti na yale yanayotarajiwa na jamii na kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha.
Magonjwa ya akili huenda kinyume na ustawi wa mtu katika ngazi ya: nafsi na utashi, akili na fikra, hisia na mihemuko. Ugonjwa wa Sonoma, Tashwishwi (wasiwasi) na Ugonjwa wa kimawazo na tabia za kukithiri ni baadhi ya magonjwa ya akili yanayokumba jamii zetu.
Mitandao ya kijamii, hii ilitakiwa kuwa chombo cha kuleta watu pamoja wakishirikishana mambo na taarifa tofauti. Mitandao hii Imekuwa kisababishi kikuu cha magonjwa haya hasa kwa vijana. Kushindwa kufikia malengo ikiwa pia ni chanzo.
Ingawa kunaweza kuwa na athari za moja kwa moja kwa mwathirika lakini kwa mapana zaidi, athari moja kubwa iliyombele yetu ni kupungua ama kupotea kabisa kwa upendo kati ya wanafamilia, ndugu, jamaa na marafiki. Mahusiano ambayo huvunjika endapo mhusika atatengwa/kujitenga kutokana na hali yake. Amini, nyumba zetu zimeficha waathirika wengi wa namna hii. Bila mahusiano mazuri, hatari ni kubwa zaidi.
Wengi wetu tunatamani japo dakika tano za mapumziko kutoka kwenye hali zetu za kimaisha. Muda ambao miili yetu, nyoyo zetu pia nafsi zetu zitakuwa huru kuambaa na asili zake halisi. Nikiamini ya kuwa MUZIKI ni jawabu sahihi kabisa kwa magonjwa ya akili, nikitambua pia tunaishi katika nyakati zenye changamoto nyingi za kimaisha. Mabibi na Mabwana, MUZIKI.
Mipangilio maalum ya sauti yenye kuburudisha, kuelimisha, hata kuponyesha pia. Mipangilio hii iliyopewa mahadhi na uzito wa sauti ndio kumeifanya kuwa namna bora zaidi ya matumizi ya lugha za kibinadamu. Naam, huu ni MUZIKI.
Muhimu zaidi, tunatumia muziki kuleta familia pamoja kama kiungo muhimu zaidi kuunda jamii. Lengo kuu ni kuongeza upendo, baada ya upendo kusikilizana, baada ya kusikilizana kuelewana, baada ya kuelewana kukubaliana. Makubaliano hayo yatakuwa misingi na miongozo ya familia husika kwa namna gani wataongoza maisha yao. Ubora wa misingi na miongozo hio kwa ngazi ya familia hujenga jamii imara na baadae taifa madhubuti.
Yatupasa kutambua, mtaji wetu wa kwanza ni afya. Twaweza kuwa na rasilimali hitajika na mipango maalum lakini pasi na afya yote ni batili. Afya ya akili inayolengwa na kalamu hii si tu suluhisho bali maisha na mifumo yake. Mtu mwenye afya njema ya akili huanza kwanza kujitambua, kuwatambua waliomzunguka na mazingira yote kwa ujumuishi.
Hii itathibitishwa kwa namna ya uwajibikaji katika shughuli zinazotekelezwa katika mazingira yake. Kuwajibika na kutenda shughuli hizo husaidia kujenga ujuzi na ufanisi ambao baada ya muda hugeuka na kuwa uzoefu, nguzo imara zaidi ya kuelimika. Yatupasa pia kuweka akilini namna zetu za ufanyaji kazi, na zaidi kutambua wajibu wetu ni matokeo ya mifumo ya kiasili inayojitosheleza katika utendaji wake. Mifumo ambayo ingawa inajitosheleza hutumika na mara nyingine husanifiwa ili tu iweze kutusaidia kutenda kazi zetu. Walio na uzoefu zaidi huenda hatua katika kuboresha na lengo likiwa ni moja tu, kuongeza uzalishaji kwa maana nyingine matunda ya kazi zaidi.
Hatua hizi mara zote huwa chini ya uangalizi,usimamizi kuhakikisha linalopaswa kutendwa linasimamiwa. Viongozi na watendaji hawagombanii fito kwa sababu wanajenga nyumba moja. Uwezo wa viongozi kuweka dira, kuonesha njia, kusimamia mifumo na zaidi kuhamasisha watendaji ni alama ya hatua za kukuza jamii wanazoongoza. Jamii zenye sifa za namna hii huwa zenye nguvu, uwezo wa kujitosheleza na kukabiliana na changamoto.
Hii ni taswira ya jamii tunayopaswa kuwa nayo katika ardhi yetu mama. Jamii yenye uelewa, uwezo wa kujitosheleza na kukabiliana na changamoto, jamii yenye wananchi wenye upendo na uwezo wa kifikra pamoja na ufanisi. Twaweza yote ilihali tutatambua na kuchukua hatua dhidi ya magonjwa ya akili, Tanzania yatusubiri.
Kumbuka, Tanzania yahitaji sana nguvu kazi iliyo imara hasa kwenye afya ya akili ilikuweza kupata majawabu na vumbuzi zitakazo kwenda sawa na kasi ya kimaendeleo ulimwenguni kote. Pengine uzuri wa maisha si tu katika mitandao ya kijamii, ni zaidi ya Hapo!

Upvote
2