Ya SportPesa na Yanga hayatuhusu, Tuhoji Mkataba wa Mo Xtra na Simba

babu onyango

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2023
Posts
378
Reaction score
984
Ndugu zangu wa Simba hili sakata la Malalamiko ya SportPesa kwa uongozi wa Yanga lisitupotezee muda tukashindwa kujadili mambo muhimu yanayohusu klabu yetu ya Simba na maendeleo yake.

Tunatakiwa Tuhoji kwanini uongozi wa Simba uingie Mkataba na Mo Xtra wa milioni 150. Yaani Mbet alipe bilion 5 kwa mwaka halafu Mo Xtra alipe Mil 150 kwa Mwaka?

Simba ni brand kubwa Afrika, ni mpumbavu pekee anaweza kufurahia kifua cha jezi ya Simba kikichezewa namna hii.
Mkataba huu ni wa kinyonyaji sana na unaipunja klabu yetu..
 
Hoji mwenyewe.

Unataka uhoji na nani?

Kwanza unaanzaje kuhoji mkataba halisi hauna. Hawa Utopolo wapumbav sana wanapenda kudandia asiyowahusu
 
Hoji mwenyewe.

Unataka uhoji na nani?

Kwanza unaanzaje kuhoji mkataba halisi hauna. Hawa Utopolo wapumbav sana wanapenda kudandia asiyowahusu
Hivi mnajua paka sasa Mo anaidai Simba Tsh ngap? Mo hatoi msaada bali anaikopesha Simba na kwa taarifa yako simba inadaiwa fedha nyingi na Mo kuliko iyo bil 20 ya uwekezaji
 
Tunatakiwa Tuhoji kwanini uongozi wa Simba uingie Mkataba na Mo Xtra wa milioni 150. Yaani Mbet alipe bilion 5 kwa mwaka halafu Mo Xtra alipe Mil 150 kwa Mwaka?
Jibu ni hili. Mdhamini mkuu (wa klabu) huwa anakuwa ni mmoja tu, na ndiye anayewekewa nembo kubwa kifuani. huyu kutokana na ukubwa wake, hata hela anayotoa ni ndefu. Baada ya kupata mdhamini mkuu, klabu inaweza ikawatafuta wadhamini wengine wadogo ambao nembo zao zinakaa pembezoni mwa jezi sawia na nembo ya mdhamini wa ligi (TFF, CAF, FIFA), sio kifuani. Hawa hata hela wanayotoa huwa sio kubwa kama ya mdhamini mkuu

Kwa kujibu swali lako, NBC, Mo Extra, Africarriers, MO29, ATCL, Vunjabei nk kama wanatakiwa kukaa katika jezi, basi ni pembezoni, maana mdhamini mkuu (M-Bet) nafasi yake ni kifuani. Kwa hiyo ndugu, tuondokane na mawazo ya kulalamikia wadhamini eti wanatoa hela ndogo, tena hasa kwa kuziandama bidhaa za MeTL, hawa wote wanaisaidia sana Simba lakini bado kwa heshima M-Bet anayetoa hela nyingi anakaa kifuani. Kuendelea kulinganisha M-Bet na Mo Extra au Vunjabei ni kuendekeza mawazo yaliyofinyika
 
Hivi mnajua paka sasa Mo anaidai Simba Tsh ngap? Mo hatoi msaada bali anaikopesha Simba na kwa taarifa yako simba inadaiwa fedha nyingi na Mo kuliko iyo bil 20 ya uwekezaji
Tuambie mwanasimba namba moja.

Tunadaiwa shilingi ngapi?

Vinginevyo, acha umbeya
 
Aisee sasa ilikuwaje tukatae mil 100 za gsm kukaa begani kama Mo Xtra yupo kifuani Kwa mil 150??
 
Aisee sasa ilikuwaje tukatae mil 100 za gsm kukaa begani kama Mo Xtra yupo kifuani Kwa mil 150??
GSM hakuwa mdhamini wa klabu,bali aliingia katikati ya ligi kama mdhamini wa ligi, na akatoa sh. 2B tu kwa udhamini timu zote 16 pamoja na TFF, bila vilabu kushirikishwa. Kwa hiyo vilabu vilipewa amri tu kwamba viweke nembo ya GSM na vipokee hiyo hela. Hoja ya Simba haikuwa kuzikataa hela, ila kujua udhamini ulivyo na formula iliyotumika kuvigawia hiyo hela
NB: Tofautisha kati ya mdhamini wa Ligi na mdhamini wa Klabu. Hela ya mdhamini wa ligi ina mgawanyo wa vilabu vingi, TFF, marefa,zawadi za washindi nk. Hela za mdhamini wa klabu zinaenda moja kwa moja kwenye klabu husika pekee
 
Hivi mnajua paka sasa Mo anaidai Simba Tsh ngap? Mo hatoi msaada bali anaikopesha Simba na kwa taarifa yako simba inadaiwa fedha nyingi na Mo kuliko iyo bil 20 ya uwekezaji
Kama Kuna makubaliana ya kimaandishi hapo sawa. Kama hana - kiendacho kwa mganga....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…