Ya SUMATRA na TANESCO: Mwanzo wa JK kupunguziwa Madaraka?

Ya SUMATRA na TANESCO: Mwanzo wa JK kupunguziwa Madaraka?

Malafyale

Platinum Member
Joined
Aug 11, 2008
Posts
13,833
Reaction score
11,173
Nafasi ya sasa ya Mkurugenzi wa Shirika la umeme Tanzania (Tanesco)Dr Idrisa Rashid sambasamba na ya Mkurugenzi wa Mamlaka ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini(Sumatra) Israel Sekirasa zote zimetangazwa kwenye magazeti kama zipo wazi,na kuwahimiza watz wenye sifa kuziwania kwenye soko huru la ajira.

Kinachonishangaza ni kuwa nafasi za Mkurugenzi Mkuu ktk mashirika Tanzu Tanzania huwa ni za kuteuliwa na Rais! Na hata hawa wakurugenzi 2 waliomaliza muda wao waliteuliwa na Rais! Iweje sasa tutangaziwe nafazi hizi badala ya Rais kuwateua?

Hii imenishangaza na naomba msaada wenu wana JF; Kwa uelewo wangu, ni Bunge tu lenye nguvu za kubadili vifungu vya sheria, Je ndiyo kusema Bunge lilibadili katiba kuruhusu baadhi ya nafasi za kuteuliwa sasa ziwaniwe kwenye nguvu ya soko la ajira? Na kama ni Bunge liliruhusu, Bunge la kikao gani lilifanya hivi?

Je kama kweli Rais ndiye mwenye nguvu Za kuteua watendaji hawa,iweje sasa asifanye hivyo?Je ndiyo kusema sasa Rais wa Tanzania kaanza kupunguziwa madaraka? Kama kaanza kupunguziwa madaraka yake, je ni chombo gani halali kimempunguzia Rais madaraka yake ya uteuzi?

Wana JF nisaidieni kwa hili jambo,Maana sielewi hii move;Dr Idrissa Rashid na wakurugenzi wengine waKuu wa mashirika Tanzu ya TZ huwa wanateuliwa na Rais,iweje hawa nafasi zao zitangazwe magazetini?!
 
Mkuu Malafyale,

Swali zuri; mimi nadhani hakuna sheria yoyote iliyobadilishwa kuhusu uteuzi wa wakurugenzi wakuu wa mashirika ya umma. Nadhani kinachofanyika sasa ni kupanua wigo na kuwapa nafasi watu wote wenye sifa kuomba kazi, na at the end of the day Rais atapelekewa short list ya majina kati ya 3-5 (baada ya wengine kuchujwa na "tume maalum"), ambapo atateua mmoja kuwa mkurugenzi (kama ataona yupo anayefaa). Utaratibu wa zamani ni kwamba 'tume maalum" ilikuwa inatafuta candidates (kwa kutumia mbinu zake) huko "underground" (na kuwachuja) na kisha kumpelekea rais majina 3-5 kwa uteuzi wa mwisho.
 
kuna mabadiliko kuu, hapo awali nafasi hizi zilikuwa hazitangazwi hadharani namna hii, pamoja na hiyo veting
 
hata hivyo ni watumishi wa kawaida sana si lazima wateuliwe na rais, bora iwe hivi na itawabidi wawajibike kwa bodi na si kwa rais.
 
Binafsi ningependa kuona kuna bodi moja tu ya mashirika yote ya umma.
 
Taratibu zilisha badilika siku nyingi. Ni kwamba wakuu wote sasa huwajibika kwa bodi zao na siyo kwa rais moja kwa moja. Hii siyo kumpunguzia madaraka rais bali ni kuweka uwazi katika ajira na kuwapa nafasi watz wengine nao kutumia ujuzi na uzoefu wao katika uongozi. Bado Tz POSTAL BANK nayo yafaa mkuu wao naye ang'oke maana ame over stay katika nafasi yake. Ana zaidi ya miaka 15 katika nafasi hiyo chini ya mikataba ya miaka mitatu mitatu. Hana lolote isipokuwa sasa amekuwa another Mugabe pale kazini. Hataki kuona akina Tvangirai wengine wakichipukia sivyo anawapiga zongo wanaishia mbali makaburini looo fisadi mkubwa.
 
Mzee kuna walio-over stay zaidi ya huyo. Kuna yule wa TPDC ana miaka zaidi ya 20, kuna yule wa DAWASA ana miaka zaidi ya 18. Teuzi hizi zinaangalia hasa watu watakaowafaa wanasiasa wetu na CCM yao.
 
haswaa, inabidi kila mtu achezeshe karata yake hata wewe mzee kama una sifa tuma licv lako
 
Mzee kuna walio-over stay zaidi ya huyo. Kuna yule wa TPDC ana miaka zaidi ya 20, kuna yule wa DAWASA ana miaka zaidi ya 18. Teuzi hizi zinaangalia hasa watu watakaowafaa wanasiasa wetu na CCM yao.

Usisahau hawa jamaa wanavyokwenda mlingotini na kuzikiri pale mbuyuni karibu na St. Peter's church Oysterbay nyakati za usiku.
 
Jk ,iwapo kweli ni kwa nia njema, basi atakuwa ameongezewa wigo. Kuapply ni moja lakini gumu ni kuwa shortlisted ili mkuu wa kaya ateue. Akitaka ukweli aombe application zote azipitie. Kimsingi hakuna mabadiliko makubwa ya endprocess!!
 
Back
Top Bottom