Yaa Nana Asantewaa: Mwanamama Malkia wa vita Aliyewapa Shida Waingereza Ghana

Yaa Nana Asantewaa: Mwanamama Malkia wa vita Aliyewapa Shida Waingereza Ghana

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Joined
Apr 29, 2016
Posts
20,743
Reaction score
25,564
Yaa Nana Asantewaa anajulikana sana kwa mchango wake wa kishujaa katika vita vya Kiti cha Dhahabu. Alikuwa mwanamke mwenye nguvu, na ujasiri wa kufanya yale aliyoyaona kwake sawa.

Yaa Asantewaa aliishi katika miaka ipi?

Alizaliwa mwaka 1840 katika mji wa Besease, wakati wa ufalme wa Ashanti.Alifariki dunia akiwa uhamishoni katika visiwa vya Shelisheli tarehe 17 Oktoba mwaka 1921.


KUTAMBULIKA KWAKE:

Alivyochochea na kuunga mkono kile leo kinachoitwa vita vya kiti cha dhahabu. Kiti hicho cha dhahabu kilikuwa moja ya vitu vya kuogofya katika umiliki wa Asante, na mwakilishi wa Uingereza kwa wakati huo Bw. Fredrick Mitchel Hodgson alitaka kiletwe kwake ili akikalie kwa jina la Malkia wa Uingereza.
Kiti cha Dhahabu au GOLDEN STOOL.


Kuteuliwa na wafalme wengi wa Mkoa wa Asante kuwa kiongozi wa vita wa Jeshi la mapigano la Asante - kama mwanamke wa kwanza katika historia ya Asante
Kuwa katika mstari wa mbele kwenye vita kwa nyakati tofauti kutoa ushauri na kusafirisha vifaa kwa wapiganaji wa Asante - akiwa na umri wa miaka 60.

Akitoa maoni juu ya kushindwa kutenda kwa ustadi kwa wanaume wa Asante kuhusiana na ombi la mwakilishi wa Uingereza:
"Siwezi kuamini. Haiwezekani! Lazima niseme jambo hili; Kama nyie wanaume wa Asante hamtasonga mbele, basi tutafanya hivyo. Nitawaita wanawake wenzangu. Tutapigana na wazungu. Tutapiambana hadi mwisho wetu sisi uwe uwanja wa vita. Kama wakuu hawawezi kupigana, mnapaswa kubadilishana nguo zenu za kiunoni na nguo zangu za chini"

ANAKUMBUKWA KWA LIPI:


Yaa Asantewa ni mfano muhimu na msukumo kwa wasichana na wanawake wengi nchini Ghana na afrika kwa ujumla kwasababu ya ujasiri aliouonyesha. Wanawake wengi ambao wanafanya kazi ambazo hapo awali zilikuwa zikitawaliwa na wanaume mara nyingi wamepewa jina la Yaa Asantewaa ikiwa ni njia ya kuwatia moyo na kuwaunga mkono.

Mnamo mwaka 2000, makumbusho moja ilijengwa kwa kumbukumbu ya malkia huyo wa vita huko Ejisu. Familia yake ilikuwa na ukarimu wa kutosha kuchangia vitu maalum vya urithi na makala ambazo Yaa Asantewaa alivitumia, ikiwemo nguo, gamba la kobe ambalo inaaminika alikuwa akitumia kulia chakula. Kwa bahati mbaya, makumbusho hayo yaliungua kwa moto Julai 2004. Vitu vingi vilipotea na makumbusho hayo bado yamesalia tupu.

Shule ya kwanza ya serikali mjini Kumasie ilipewa jina la: Shule ya sekondari ya wasichana ya Yaa Asantewaa.
 
Duu, aliishi miaka 81
Hakika alikuwa ni jasiri..
 
Asante kwa historia mkuu...!! Sikuizi wanawakee kama hao walikufa Vita ya pili ya dunia
 
Nimerudi Jana toka Ghana, nilifika Kumasi hadi mji wa Asante, nikapata bahati ya kutembelea Museum & palace ya kifalme ya "mahnyia".

Kweli nimeona historia nzuri na ya kuvutia ya wafalme/ malkia wa ghana (Asante) kuanzia kwa Yaa hadi wa sasa. Huyu wa sasa ni uzao uleule wa Yaa.

Anaposition inayo fanana na ufalme/umalkia wa uingereza kwa Ghana, Rais wa Ghana lazima apate blessings za malkia/ mfalme wa Asante! Na tuliambia kuna kiasi cha kodi kinaenda kwa mfalme/malkia wa Asante.

Utawala wake uli extend hadi sehemu ya Shelisheli na Nigeria.
Na anatambulika kimataifa.

In fact support ya malkia/mfalme wa Asante ni muhimu sana kwa rais na utawala wa kisiasa wa Ghana.
 
Wanawake mashujaa kwa sasa ni akina Joyce Kiria wanaotaka kuishi kwa kuhongwa mjini au wale walionyeshewa mvua siku nzima hapa majuzi wakishtaki ati wameshindwa kulea mtoto mmoja!
 
Wanawake mashujaa kwa sasa ni akina Joyce Kiria wanaotaka kuishi kwa kuhongwa mjini au wale walionyeshewa mvua siku nzima hapa majuzi wakishtaki ati wameshindwa kulea mtoto mmoja!




Je wewe ni shujaa?
 
Back
Top Bottom