Yaani mimi nimlipe mwenye nyumba kodi ya Jengo kupitia LUKU?

ngebe

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2020
Posts
1,789
Reaction score
5,117
Wakuu, itoshe tu kusema Serikali ya CCM imechoka na haina mbinu mpya tena

Mawaziri na Wabunge hawana lolote la msingi wanaloweza kufanya kwa sasa

Mimi mpangaji mnanilipisha kodi ya jengo? hivi mlikaa kabisa mkanywa na chai mkalipwa na posho mkatoka na hii idea?

Nilikuwa namkubali sana Mama Samia lakini hapana mambo yamemuendea mlama, nchi imemshinda kuimudu
 
Ya Kaisari mpe Kaisari na ya Mungu mpe Mungu
 
Mkuu ili kuepuka kumlipia mwenye nyumba,Jenga yako ujilipie Kodi ya jengo uache kumlipia mtu mwingine.
 
Serikali BATILI haijawahi kufanikiwa kwa lolote
 
Hii ilitakiwa iingizwe kwenye land rent, Lukuvi aliwaandalia mazingira mazuri kabisa kupitia mpango wa urasimishaji wa ardhi.
 
Ongea na mwenye nyumba akupunguzie kodi ya nyumba kwa kiasi utakacholipa kodi.

Vitu vingine tusolve sisi wenyewe tusiilamu sana serikali
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…