Sijali
JF-Expert Member
- Sep 30, 2010
- 2,672
- 1,814
Yaelekea kuna mkanganyiko wa ufahamu baina ya wale wanaosema Tanzania ni nchi maskini na wale wanaosema ni nchi tajiri. Wote hawakukosea. Makosa yapo katika kinachokusudiwa.
Miaka yote ya uongozi wa Mwalimu Nyerere alikuwa akisema Tanzania ni nchi maskini. Wakati mwingine alisema bara zima la Afrika ni maskini. Mwalimu alikuwa kwa kweli anajua maana ya utajiri.
Mtu huwezi kuwa tajiri hadi hapo utajiri uweze kuufasiri katika ubora wa maisha yako ya kila siku. Mfano mzuri ni ndugu zetu Wamasai ambao baadhi wana ng'ombe elfu kumi, lakini kutokana na kushindwa kufasiri utajiri huo kwenye maisha yao ya kila siku, watu hao ni maskini.
Sasa ninakuja katika hizi kauli za siku hizi kwamba Tanzania ni tajiri, hadi kuwapelekea baadhi ya watu kuanza kuwa na majivuno! Hii ni kweli, kama nchi, lakini Watanzania si tajiri. Maisha ya Watanzania ni duni mno hata kuliko ya Wasomali, Wasudan au WaComoro (moja ya nchi maskini sana), ukilinganisha uwezo wao wa kununua (purchasing power) wa walio wengi.
Ukitazama jinsi serikali inavyowachukulia raia wa Tanzania, utaona wazi kwamba kauli hii ya utajiri unaodaiwa wa Tanzania imewaingia kichwani, na wanaamini kuwa Watanzania wengi wanafaidi 'utajiri' huo.
La sivyo, unawezaje kuweka kodi ya laki tatu, milioni moja nk wakati ni kazi chache sana zinalipa mshahara huo? Sikuambii malipo ya matibabu, dawa nk.
Tozo na kodi za serikai haziendani kabisa na pato la raia.
Dhana hiyo hiyo potofu inawatesa wanaotembelea Tanzania. Nimewasikia watalii wakilalamika kuwa Tanzania "is expensive".
Ndiyo maana sishabikii hata hayo 'maendeleo' kwa vile si wengi watakaoweza kufaidi.
We wadhania tiketi ya SGR kutoka Dar hadi Morogoro tu itakuwa shs ngapi? Tuishaona nauli za ndege, mwendo kasi etc.
Yaelekea kuna mtu hajui hali halisi za Watanzania.