Yafahamu magari ya bei nafuu unayoweza kununua Tanzania

Yafahamu magari ya bei nafuu unayoweza kununua Tanzania

Lyamber

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2012
Posts
11,716
Reaction score
18,828
Kwa utafiti usio rasmi kwa mtazamo wangu baada ya kupita pita kwenye magroup ya Whatsapp na Kurasa za facebook za wauza magari yaliyotumika hapa Tanzania ni kama yafuatayo:

Toyota Vitz, IST, Raum, Passo, Run X Mark II, Grande,Altezza Cresta, Brevis, Nissan X - Trail haya bei zake huanzia 3,000,000-7,500,000 angalizo lipo kwenye Brevis na Nissan X-Trail maana hayo magari kuuza hua ni shughuli kubwa sana.

Ila ajabu ni kwamba magari yanayouzwa Dar es salaam huwa yana bei kubwa ukilinganisha na yanayouzwa mikoani sijui tatizo lipo wapi.
 
Kwa dar, Chain huwa kubwa, Gari moja inapita kwa watu zaidi ya wawili, na kila mmoja [dalali] anaweka cha juu, Tofauti na bei iliyowekwa na mmiliki wa gari husika.
Naunga mkono hoja mkuu.

dodge
 
Hata kwenye yard ya magari kuna dalali? Mikoa mingi haina sehemu maalum ya kuuzia magari, unakuta mtu binafsi anauza gari na anaogopa alipandishwa bei hapati wateja ndio maana yanakuwa bei rahisi
 
Back
Top Bottom