Yafahamu magari yaliyotumiwa na hayati baba wa Taifa Mwl Nyerere

Ushimen

JF-Expert Member
Joined
Oct 24, 2012
Posts
40,828
Reaction score
99,523
USTIN MORRIS A-40

-Gari aina ya- Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na Baba wa Taifa na Rais wa kwanza Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwalimu Nyerere alilitumia gari hilo toka mwaka 1955 – 1960 katika shughuli mbalimbali za kuendeleza chama cha TANU likiendeshwa na dereva wake maarufu kwa jina la SAID TANU. Baadaye Mwalimu Nyerere alilikabidhi gari hilo kwa vijana wa TANU kwa kazi za chama kabla ya kupelekwa Makumbusho ya taifa na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.
 
Attachments

  • 1444390150009.jpg
    1444390150009.jpg
    48.4 KB · Views: 2,025
USTIN MORRIS (A-40 VAN GUARDS)

Gari aina ya Austin Morris A-40 maarufu kama Van Guards lilitengenezwa kati ya miaka ya 1945 – 1950. Gari hili lilitumiwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa shughuli za TANU akiwa Dar es Salaam na ziara za mikoani kuhamasisha shughuli za chama. Dereva wake alikuwa ni SAID TANU.
 
  • 1444390401666.jpg
    1444390401666.jpg
    27.9 KB · Views: 700
ROLLS ROYCE

-Gari aina ya ROLLS ROYCE lilitengenezwa -1938 na kuletwa na Gavana wa wakati huo Harold Mac Michael katika utawala wa wakoloni waingereza na lilitumiwa na Gavana wa mwisho kuitawala Tanganyika Sir Richard Turnbull.

Rolls Royce lilitumika kupokea wageni mbalimbali waliotembelea Tanganyika wakati huo wakimwemo Rais wa zamani wa Liberia Hayati William Tubmann na Mfalme wa zamani wa Ethiopia Hayati Haille Sellasie.

Gari hilo lilitumika hadi mwaka 1962 baadaye -mwaka 1978 Rais wa kwanza Tanzania Hayati Julius Kambarage Nyerere aliagiza Rolls Royce kuhamishwa toka Ikulu hadi Makumbusho ya Taifa. Kwa sasa ni sehemu ya Historia ya Taifa la Tanzania.
 
ROLLS ROYCE (PHANTOM V)

-Gari aina ya Rolls Royce Phantom V lilitengenezwa nchini Uingereza na kutolewa na nchi hiyo kwa Rais wa kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Novemba 05,1965.

Rolls Royce -Phantom V lilianza kutumika mwaka 1970 kwa kupokea viongozi wa nchi mbalimbali wakiwemo Marais na mabalozi wa nchi mbalimbali waliotembelea Tanzania.

Gari hilo lina sifa za kipekee kwa wakati huo likionekana la- kisasa zaidi kwani lina sehemu ya mbili za kuweka bendera, moja upande wa kulia ambako aliketi mgeni na upande wa kushoto bendera ya Tanzania alikoketi mwenyeji wake (Mtanzania).Sehemu ya juu ya -Rolls Royce Phantom V yaweza kufunguliwa kwa minajili ya kuwaruhusu viongozi kusimama na kuwapungia mikono wananchi au kuruhusu hewa kuingia hasa wakati wa joto (hapa ni kama AC/kiyoyozi kwa magari ya sasa). Kwa kweli tumetoka mbali na huu ndio uhondo wa historia.

-

Rais wa awamu ya pili wa Tanzania Alhaji Ali Hassan Mwinyi alilitumia gari hilo na Rais wa awamu ya tatu Benjamini William Mkapa akalitumia pia kabla ya kuamua kulipeleka Makumbusho ya Taifa Machi 08,2006 na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.
 
Mercedez Benz 230.6 lilijulikana kama gari la jumuiya kwani lilitumiwa na Rais wa Tanzania Hayati- Mwalimu Julius Kambarage Nyerere kwa shughuli za jumuiya Afrika Mashariki iliyoundwa mwaka 1967 na nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambapo kila nchi ilikuwa na gari kama hilo.

Moja ya sifa ya gari hilo kwa wakati huo ni kuwa na uwezo wa kubeba watu wengi zaidi.Uwezo wake ni kubeba marais wageni wawili, mpambe wa Rais, mwandishi habari wa Rais na Rais mwenyeji kwa mara moja.

Mercedez Benz 230.6 lilikuwa na namba za kipekee ambazo ni RE-1 (yaani Royal Excellecy 1).Hata hivyo Jumuiya ya kwanza ya Afrika Mashariki ilidumu kwa miaka 10 tu (1967 – 1977) ambapo ilivunjika kwa sababu mbalimbali. Gari- hilo likapelekwa Makumbusho ya Taifa Oktoba mwaka 2002 na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.
 
MERCEDEZ BENZ E 300

-Mercedez Benz E 300 lilitengenezwa nchini Ujerumani na kununuliwa na serikali ya Tanzania Desemba 17, 1996- ambapo Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alilitumia kwa shughuli za kitaifa na binafsi katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani baada ya kustaafu Urais.

Mercedez Benz E-300 litaendelea kukumbukwa zaidi kwani ndilo gari la mwisho kwa Hayati Mwalimu Nyerere kulitumia enzi za uhai wake hapa nchini kwani alilitumia kwa mara ya mwisho kabisa Agosti 31,1999 akienda kupata matibabu huko nchini Uingereza.

Alisafiria gari hilo kutoka nyumbani kwake Msasani hadi uwanja wa kimataifa wa Dar es Salaam (kwa sasa Mwalimu Julius Nyerere).

Hata hivyo kwa MASIKITIKO MAKUBWA Baba wa Taifa hakurudi tena kulitumia tena gari hilo kwani alifariki dunia Oktoba 14, mwaka 1999 katika hospitali ya Mtakatifu Thomas huko nchini Uingereza. MUNGU AIWEKE ROHO YAKE MAHALA PEMA PEPONI,AMEN.

Gari lake alilotumia kwa mara ya mwisho (Mercedez Benz E 300)-likatolewa na mkewe Mama Maria Nyerere kwa ajili ya kuhifadhiwa katika Makumbusho ya Taifa Septemba 24, 2004.

Katika utalii wa ndani-.
 
USTIN MORRIS A-40

-Gari aina ya- Austin Morris A-40 lilitengenezwa nchini Uingereza kati ya mwaka 1940 – 1950. Ni gari la kwanza kutumiwa na Baba wa Taifa na Rais wa kwanza Tanzania hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Mwalimu Nyerere alilitumia gari hilo toka mwaka 1955 – 1960 katika shughuli mbalimbali za kuendeleza chama cha TANU likiendeshwa na dereva wake maarufu kwa jina la SAID TANU. Baadaye Mwalimu Nyerere alilikabidhi gari hilo kwa vijana wa TANU kwa kazi za chama kabla ya kupelekwa Makumbusho ya taifa na kuwa sehemu ya Historia ya Tanzania.

Ushiboy,
Hili gari Mwalimu Nyerere alipewa na Dossa Aziz.
Napenda nikuwekeeni hapa historia ya gari hili:

''...Dossa Aziz alipokwenda Nairobi mwaka wa 1946 alimkuta Ally Sykes, kijana maarufu na mwenye shughuli zake pale mjini akijulikana na takriban kila mtu. Dossa Aziz alikuwa amekwenda Nairobi kufanya usaili wa mafunzo ya urubani. Kulikuwa na vijana wawili kutoka Tanganyika, wote watoto wa matajiri. Dossa Aziz alikuwa katika usaili na mtoto wa Mwarabu mmoja tajiri, Ally Mmanga. Dossa Aziz alikataliwa kufanyiwa usaili kwa kuwa alikuwa Mwafrika.

Waingereza walidai kuwa Waafrika hawakuwa tayari kufundishwa urubani. Dossa Aziz alifadhaika sana. Alimpigia simu baba yake huku akilia na kumpasha habari hizo. Ili kumliwaza mwanae, baba yake Dossa, Aziz Ally, alimtumia fedha anunue gari kama kifuta machozi. Gari hili lilikuja kuwa ndiyo chombo cha kwanza cha usafiri kwa TAA, TANU na Julius Nyerere.

Ally alimpeleka Dossa Aziz kwenye mkutano wa KAU ambao Kenyatta ilikuwa ahutubie. Wajaluo wakiwa kabila hasimu na maadui wa Wakikuyu, kabila ya Kenyatta, walikuwa wakipita huku na kule katika mkutano ule wakimtukana Kenyatta. Jambo hili lilianzisha mapigano kati ya Wajaluo na Wakikuyu. Mapigano yalifuatia pande zote mbili zikitupiana mawe. Askari wa kuzuia fujo wakiongozwa na maafisa wa Kizungu waliitwa kutuliza fujo. Waliizingira River Road, mahali ambapo mkutano ulikuwa ukifanyika na wakaanza kushambulia kwa virungu Mwafrika yoyote waliyemwona.

Dossa Aziz alishuhudia mambo haya yote kwa mshangao mkubwa. Baada ya kununulia gari, Dossa Aziz alikaa na Ally siku chache kisha akarudi nyumbani. Alirudi Dar es Salaam na kumbukumbu zile alizozishuhudia pale River Road, mjini Nairobi.''
 
Asante kwa kujazia hizi mambo mkuu
 
Mkuu huyu Aziz Ally ana uhusiano wowote na Mtoni kwa Aziz Ally kule Dar ?
 
Mboona mmezsahau landrover 109 alokuwa akfanyia ziara mikoani? Pia aliwaitumia nissan patrol saloon TD-42 nyeupe na sticker nyekundu,alionekana nayo 1996 mwanza ikulu ndogo ya capripoint kwny musiba wa ajari ya mv-bukoba,nlkuwa darasa la nne enzi hizo.gari hiyo pia ndo iltumika kumsafirisha toka butiama-mwanza ili apande ndege aelekee dar kwny matibabu na ndo hakurudi tena,hiyo nayo ipo kama siyo butiama itakuwa dar,hapo vp vijana waleo?.
 
Back
Top Bottom