rajabumahede
Member
- Jan 30, 2020
- 6
- 21
Yajuwe maradhi ya ini na dalili zake
JE! UNAJUWA KUWA:-
Ini ni katika viungo muhimu sana katika mmeng'enyo wa chakula mwilini. Ini husaidia kuondosha sumu za vyakula na katika utunzaji wa glucose ambayo hutumika katika kutupatia nguvu na nishati. Kiungo hiki kinaweza kushambuliwa na maradhi mengi. Endapo kiungo hiki kitaathirika kwa namna yeyote ile basi afya ya mtu haiwezi kuwa sawa. Makala hii itakwenda kukuorodheshea baadhi tu ya maradhi ya ini, na dalili zao kwa jumla, na pia tutaona namna ya kujilinda dhidi ya maradhi haya.
NI YAPI MARADHI YA INI NA NINI CHANZO CHAKE?
Huu ni mkusanyiko wa maradhi mbalimbali ambayo yanashambulia na kuathiri ini na utendaji kazi wa ini. maradhi haya yanaweza kathiri ini ama nyongo.Zipo sababu nyingi za kutokea maradhi haya, miongoni mwazo ni kama:-
- Maradhi ya ini yanayosababishwa na mashambulizi kama virusi mfano Hepatitis A, hepatitis B na hepatitis C.
- maradhi ya ini yanayosababishwa na mfumo wa kinga kushambulia seli za ini (immune system abnormality), maradhi haya ni kama Autoimmune hepatitis, primary biliary cirrhosis na primary sclerosis cholangitis.
- Maradhi ya ini yanayosababishwa na saratani kama saratani ya ini na saratani ya nyongo.
- maradhi ya ini yanayosababishwa na kurithi. Mtu anaweza kurithi maradhi haya kutoka kwa moja ya mzazi wake ama wote. Mfano wa maradhi haya ni Hemochromatosis, Hyperoxaluria na oxalosis na Wilson’s diseases
NI ZIPI DALILI ZA MARADHI HAYA YA INI:
Kama nilivyotangulia kutaja maradhi haya ya ini, basi kila moja kati ya hayo lina dalili zake. Lakini kwa kuwa maradhi haya yote yanalenga kuathiri ini na utendaji wake wakazi, basi yana dalili ambazo huwa zinafanana kwa kiasi. Hivyo hapa nitakuorodheshea tu dalili ambazo zinafanana ambazo hzinonyesha uwepo wa moja ya maradhi haya ya ini. Dalili hizo ni kama:-
- Macho na ngozi kuwa na rangi ya njano
- rangi ya mkojo inakuwa nyeusi ama mkojo kuwa na giza
- mgonjwa anakosa hamu ya kula
- kuuma kwa ngozi pamoja na kuchubuka kwa urahisi
- kuvimba hasa kwenye vifundo vya miguu na miguu
- kupata choo kikubwa kikiwa na damu ama kuwa na rangi ya kupauka
- maumivu ya mwili na ngozi,
- kuvimba kwa mwili
- uchovu mkali usio wa kawaida.
NINI TUFANYE KUEPUKA MARADHI YA INI?
Kwa kuwa tumeshaziona dalili za maradhi haya, na pia tumeona sababu za kutokea kwa maradhi haya, sasa nini tufanye ili kuepuka ama kujilinda na maradhi haya. kwa ufupi tunaweza kufanya mambo yafuatayo:-
- Kama unatumia kilevi cha pombe hakikisha hunywi kupitiliza, kujirudiarudia tabia hii kwa muda mrefu inaweza kuhatarisha afya ya ini lako
- Kama una uzito zaidi ya kawaida hakikisha unachukuwa tahadhari za kupunguza uzito, pia itambulike kuwa kuzidi kwa uzito kunaweza pia kukuletea kisukari.
- hakikisha unafanya mazoezi walau kwa muda mchache mara kwa mara ili kufanya mfumo wa kinga kuwa active. Yapo mazoezi unaweza kufanya hata ukiwa ndani, jitahidi kufanya hivyo.
- Pata chanjo ya baadhi ya maradhi haya kama chanjo dhidi ya hepetitis
- kama unapuliza dawa ya kuuwa wadudu hakikisha unaziba pua na mdomowako kwa mask ama kitambaa.
- jiepushe na tabia hatarishi za kujidunga sindano kwa kushea vifaa vya nzcha kali ama ngono zembe.
- hakikisha hutumii dawa kiholela bila ya kupata ushauri wa mtaalamu wa afya. kwani kuna madawa mengine yakitumiwa vinginevyo huweza kuhatarisha afya ya ini.
Chanzo:https://bongoclass.com/magonjwa/ini.html