greater than
JF-Expert Member
- Sep 22, 2018
- 1,653
- 3,060
Ifuatayo ni Orodha ya masoko ya Mitaji/Financial markets ambapo unaweza ukafanya uwekezaji
1. HATI FUNGANI
Ni soko ambapo muwekezaji anakopesha fedha kwa kipindi cha mda flani huku akipatiwa riba.Kwahiyo Hati fungani ni hati ya makubaliano kati ya mkopeshaji na mkopaji ikiwa na maelezo ya riba na mda wa kurejesha mkopo.1. HATI FUNGANI
kuna hati fungani za aina mbili.
- Hati fungani za Serikali :Hapa serikali huomba mkopo kupitia benki,,mkopeshaji anaweza kuwa Mwananchi wa kawaida au taasisi na kampuni binafsi.
- Hati fungani za makampuni : Makampuni makubwa yanapo hitaji mikopo kwa ajili ya kujiendesha au kuendesha shughuli zao,nayo huweza kutoa hati fungani.mfano: Benki ya CRDB ilitoa hati fungani ya KIJANI BOND ili kuweza kufadhili shughuli za mazingira.
- Hati fungani ndogo kabisa ni ya shillingi 1,000,000
- Riba ndogo kabisa ni 9.3% hii ni kwa hati fungani ya miaka mi5
- riba kubwa ni 15.9% ni kwa hati fungani ya miaka 25
- Serikali ina rekodi nzuri ya kulipa madeni yake yanhati fungani 99%
- unaweza pata hati fungani moja kwa moja kutoka benki kuu,ama ukanunua kutoka mtu ambaye ameamua kuiuza yake kuptia wakala
- Uwezekano wa hela yako kupotea ni 1% , Licha ya umaskini wa nchi za Afrika lakini ni nadra kusikia zimefirisika.
2. SOKO LA HISA/DAR ES SALAAM STOCK EXCHANGE
Hisa ni kununua sehemu ya umuliki wa kampuni,ambapo katika soko hili kuna jumla ya makampuni 25 yaliyo jiorodhesha.Kampuni ya DSE ndiyo inayosimamia masuala yote yanayoendelea katika soko hili la hisa.Unaweza kunua hisa za makampuni 21 tu,hayo mengine ni makampuni ya kenya ambapo mpaka ujiandikishe kwenye soko la Nairobi ndiyo unaweza nunua hisa zao.
Sifa za uwekezaji wa Hisa
- Ukinunua hisa,haziozi wala kuisha,unabaki kuwa sehemu ya umiliki katika kipindi chote cha umiliki
- unapata gawio la sehemu ya faida ya kampuni
- unaweza tumia Hisa zako kama dhamana ya mikopo na ufadhili.
- uwezekano wa hela yako kupotea ni 10% tu,hii utokea pale kampuni inapo firisika tu,
- Kwa kipindi cha miaka 20 ya karibuni ni kampuni moja tu ndiyo lililo firisika na kufutwa.
- Unaweza mrithisha mwanao
3. SOKO LA BIDHAA/TANZANIA MERCANTILE MARKET
Kwenye hili soko, Ufanyika ununuzi wa bidhaa kukiwa ahadi ya malipo kufanyika kabla hata hayajavunwa .Kwa Tanzania hili.Hili soko bado ni jipya na nadharia ya mfumo wa wake bado ni mgeni kwa watanzania,na nina imani wengi wenu ndiyo kwanza mnaskia leo kuhusu TANZANIA MERCANTILE MARKET.
Sifa za soko hili
- Bidhaa hukaguliwa na wataalam
- Hauangaiki na usafishaji kutoka shambani
- Mzalishaji mazo hupata uhakika wa soko
- Rahisi kupata mteja nje ya nchi kwani bidhaa huwa na vibali vyote vya serikali.
4. SOKO LA UBADILISHAJI FEDHA
almaarufu kama FOREX,ambapo uankuwa busy kukisia kama fedha ya nchi flani itapanda kithamani dhidi ya nchi nyengine ama lah.Sifa zake
- uwezekano wa kupoteza fedha ni 80%,kwani kauli ya Rais wa Marekani inaweza ikakufanya uwe na kicheko au kilio papo hapo.
- Hii hi kitu kwa Tanzania ni siyo rasmi,kwani hakuna mamlaka inayosimamia....
5. CRYPTOCURRENCY
Hili soko nalo ni sawa na kubadilisha fedha, ila fedha zake hazipo chini ya Benki kuu za nchi yoyoteuwezekano wa kupoteza fedha ni ni 90%
KUMUBUKA
- Masoko rasmi ya fedha ambayo unayotakiwa ushiriki ni yale ambayo yapo chini ya Usimamizi wa MAMLAKA YA MASOKO YA MITAJI NA DHAMANA (CMSA)
- Ili uweze kushiriki katika masoko ya mitaji,ni lazima upatiwe CDS number
- FOREX NA CRYPTOCURRENCY,siyo masoko rasmi
- UTT siyo soko la fedha bali mfuko wa fedha.