Peter Mwaihola
JF-Expert Member
- Jun 23, 2022
- 276
- 460
Aliyekuwa rais wa kwanza mweusi wa taifa huru la Afrika ya kusini alifahamika zaidi kwa majina mawili ya Nelson Mandela.
Hayati Mandela aliyezaliwa 1918 na kufariki 2013 alikuwa na majina mengine zaidi aliyoitwa katika Kipindi cha maisha yake.
Kila jina aliloitwa kilikuwa na maana yake lilipotumika.
1. Rolihlahla. Hili lilikuwa jina lake la kuzaliwa, lilikuwa jina la kabila ka Khosa lililokuwa na maana ya kuvunjavunja matawi ya miti. Jina hili alipewa na baba yake.
2. Nelson. Jina hili alipewa na mwalimu wake siku ya kwanza shuleni, Mwalimu Mdigane alimpa jina hilo ikiwa ni kawaida kwa kipindi hicho kuwabatiza majina ya kizungu watoto wa Kiafrika ili kuendana na utamaduni wa kizungu.
3. Madiba. Hili ni jina la ukoo ambao hayati Mandela alitoka, jina la ukoo lilikuwa na umuhimu mkubwa kuliko na baba mzazi katika utamaduni wa vizazi vya Afrika kusini. Madiba lilikuwa ni jina la mtawala wa kiasili "Thembu" ambaye alitawala eneo la Transkei katika karne ya 18.
4. Tata. hili lilimaanisha "Baba" kwa lugha ya kikhosa, Mandela aliitwa jina hilo ikiwa ni heshima kwa kile alichokifanya katika taifa lake, watu wote walimuita jina hili hata wale waliomzidi umri.
5. Khulu. Mandela aliitwa Khulu ikimaanisha Mkuu, pia walimuita "Tat'omkhulu" likimaanisha "Babu" kwenye lugha ya kikhosa.
6. Dalibhunga. jina hili alipewa akiwa na umri wa miaka 16 alipotoka jandoni, lilikuwa na maana ya uongozi wa baraza au muongoza mjadala.
Follow Peter Peter Mwaihola