SoC02 Yafanyike haya kuikomboa NHIF

Stories of Change - 2022 Competition

Deogratias_01

Member
Joined
Sep 3, 2022
Posts
18
Reaction score
141
Chanzo: Picha na JamiiForums

Yafanyike haya kuikomboa NHIF

Katika kutekeleza dhima na dira ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika kutimiza majukumu ya utoaji wa huduma ya Afya kwa kuzingatia Dira ya Taifa ya Maendeleo (2025), Sera ya Afya ya mwaka 2007, Mpango Mkakati wa Tano wa Sekta ya Afya (Health Sector Strategic Plan (HSSP) V 2021/22 – 2025/26) pamoja na makubaliano ya Kimataifa na kikanda yenye lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za afya kwa wananchi, yafaa kuzingatia uwepo kwa uongozi shupavu na wenye mipango kazi makini, miradi yenye tija na endelevu pamoja na ushirikiano wa wadau, mawakala na kila mwananchi ili kuweka mazingira wezeshi katika utimizaji na utekelezaji wa malengo na maadhimio ya uboreshaji na upanuzi mpana wa kiutendaji, umakini na ubunifu wa utoaji wa huduma bora za afya nchini Tanzania.

Licha ya jitihada zinazofanywa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika kuimarisha huduma za afya kwa kuwa na uongozi imara na shupavu, kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wote kuwa na uhakika wa kupata huduma bora za afya, uwekezaji katika ujenzi wa miundombinu ya utoaji wa huduma za afya ikiwemo Zahanati, Vituo vya Afya, Hospitali za Wilaya na Mikoa katika maeneo mbalimbali nchini sambamba na ununuzi wa vifaatiba vya kisasa, kuongeza bajeti ya dawa na vitendea kazi na kuongeza ajira kwa watumishi katika Sekta ya Afya katika ngazi zote, endapo Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) ukiporomoka, utapelekea kuhatarisha afya za wananchi, kudorora kwa shughuli za kiuchumi na uchumi wa nchi kudidimia.

Katika muktadha huo, athari nyingi zaweza kushika hatamu kama mikakati na hatua stahiki zikichelewa kuzingatiwa katika kuukomboa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) hususani katika kutafuta mbinu mbadala za kuhudumia Wanachama wagonjwa wa magonjwa yasioambukiza yenye malipo ghali kuyahudumia na yanayochangia asilimia 71% ya vifo vyote duniani kwa kila mwaka kama vile magonjwa ya huduma za matibabu ya figo kwa wanachama wanaopata huduma ya kuchuja damu (hemodialysis services), tiba za mionzi ya saratani na chemotherapia na matibabu ya upasuaji wa moyo (minimal and invasive cardiac procedures pamoja na sababu nyinginezo zilizochambuliwa, kuorodheshwa na kusadikika kuelemea na kuporomosha utendaji na uhimilivu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), basi tutazamie kushuhudia Mfuko kushindwa kutimiza majukumu yake kadiri ya mujibu wa sheria ya Bima ya Taifa ya Afya (Act, Cap 395) iliyotungwa kwa lengo kuu la kuhakikisha upatikanaji wa huduma za ki-Afya kwa watu wote nchini.

Uhalisia wa matokeo kama Mfuko wa Taifa wa Bima ukishindwa kutimiza majukumu yake na kufa ni pamoja na kugota kwa zoezi la utoaji wa elimu kwa jamii juu ya dhana ya bima ya afya na umuhimu wa kujiunga na bima ya afya kabla ya kuugua, pamoja na kukwama kwa shughuli za uimarishaji wa mfumo wa bima ya afya nchini (NHIF na CHF) katika kuhamasisha Wananchi wengi kuwa na bima ya afya. Pili, watu wengi watakufa, haswa wale Wanachama waliosajiliwa na walio na matibabu ya gharama kubwa kama vile dialysis ikiwa hawawezi kulipa kutoka kwenye mifuko yao wenyewe. Benki na Makampuni ya uwekezaji yatapoteza mabilioni ya fedha zilizowekwa/ kuwekezwa na NHIF. CHF itapoteza dhamana/ chelezo na hivyo basi zaidi ya 15% ya wanachama wa CHF wanaweza kupoteza bima zao za matibabu. Pia, manufaa mengine ya NHIF kwa uchumi kama vile udhibiti wa ubora wa huduma za afya na bei, ajira na kodi zitapotea.

Nini kifanyike kuendeleza uhai na utendaji wa (NHIF)? Mosi, utambuzi wa haraka wa kitaalamu na mipango thabiti ya kutathmini viwango vya bei kitakachowezekana na endelevu dhidi ya kiwango cha manufaa kilichopo.

Pili, kuweka upya manufaa au/ na viwango vya malipo.

Tatu, kuangalia upya njia za malipo za mtoa huduma na kuchagua zile zinazofaa zaidi kama vile malipo ya awali au/na ada kwa kila kesi.

Nne, kutengeneza kifurushi cha uokoaji ili kuleta utulivu wa mfuko wakati hatua tajwa zikitekelezwa kama vile kutafuta mikopo yenye masharti nafuu kutoka benki/ taasisi za maendeleo.

Tano, kubuni dhamana za kijamii ili kupata fedha kupitia Soko la Mitaji (CMSA). Sita, kutafuta fedha za dharura kwa ajili ya uokoaji kutoka GoVT URT (MoFP & Disaater Fund PMO), WHO, UNICEF, IMF, Benki ya Dunia, AfDB. Mwisho, kuwezesha rasilimali watu kubuni na kuendesha NHIF endelevu.

Nakala hii inafungwa kwa kushauri bodi ya Wakurugenzi wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) kuendelea kufanya kaguzi za mara kwa mara katika bohari nzima ya Sekta ya Afya nchini pamoja na kwenye vituo vya kutolea huduma za Afya kwa lengo la kusimamia na kuimarisha ubora wa upatikanaji na utoaji wa huduma za Afya. Utoaji wa elimu na miongozo mbalimbali ya tiba inayotolewa na Serikali. Vilevile, katika kuhakikisha uhai na uendelevu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Serikali kupitia Wizara ya Afya na idara zake, wawekezaji na wadau wote kudumisha ushirikiano, kusikiliza, kuchambua taarifa na kufanya tathmini (actuarial valuation) ya uhai na uendelevu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
 
Upvote 52
Ahsante kwa maoni mkuu.
 
Njia hizi wanazijua tena ukisoma andiko lao kipindi kile mfuko huu unaanzushwa hakika utasema tulipata mkombozi, kinachojitokeza sasa hivi no ufisadi tu, hawa NHIF wanashirikiana na Hizi Polyclinic kupiga kwa kutumia mfumo, pia watumishi wanajilpa stahiki na marupurupu kibao, pia kumekuwa na undugulization kwenye ajira.
 

Mkuu kwa hakika nisingependa kukupaka mafuta kwa mgongo wa chupa.

1. Kuna upigaji mkubwa sana kwenye kiachoitwa bajeti ya dawa. Hapa tunazungumzia trillions za pesa kwa mwaka wakati dawa zenyewe hakuna mahospitalini.

Sijawahi kwenda hospitali au kupeleka mgonjwa tukapewa dawa yoyote kwa miaka mingi sasa.

2. Matumizi ya anasa kwa walioko jhuko uu ni mzigo mkubwa kwetu walipa kodi.

Wao wanatibiwa nje na Mzena kwa gharama zetu. Sisi je?

3. Tunaambiwa tozo na kodi lukuki eti kwa ajili kujenga hospitali wakati wenzetu wananunua magari ya thamani ya kupindukia million 500 kwa mtu kwa pesa za mlipa kodi asiyeweza kumudu gharama zake za mlo wake tu.

Kipi kwanza mlo au hospitali? Hospitali za kutibu watu wenye njaa?

Kwa maoni yangu bima ya afya kwa wote inawezekana ila tujItue mizigo ya ha ndugu huko juu. Tuanze nao hawa kuwaweka wanapostahili kwa maslahi ya wote, mengine yote yatafuata.

Bila kujitambua mbona tutatwanga mno maji kwenye kinu?
 
Ahsante sana ndugu. Naomba "quote" seheme kwenye ukakasi nami sitosita kuieelezea kwa maneno mengine.
Pili, kuweka upya manufaa au/na viwango vya malipo.
 
Hongera Sana Kwa nakala nzuri [emoji122][emoji122][emoji122]
 
Ahsante sana ndugu, naomba uipigie kura (vote) angalau haya maoni yangu
 
Ahsante sana ndugu,, naomba uipigje kura hata haya mawazo yangu🙏
 
Hapo, yafaa kama ni lazima, watathimini viwango vilivyopo vya uchangiaji wa wanachamaa wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ili kutegemeza uhimilivu na uendelevu wa hayo magonjwa yasadikikayo kuwa ni ghali katika kugharamia.
 
Yaani hiyo 8% tu ya watanzania ambao ndio wanachama wa NHIF, ikipolomoka ndio itakuwa hatari kwa taifa?
Hapa cha kufanya ni serikali kutumia nguvu kulazimisha kila mwanachi ajiunge kwenye mfuko huu wa bima, ndio utaweza kujiendesha bila matatizo.Sasa wachangiaji ni 8% lakini wanufaikaji utakuta ni wengi zaidi, kutokana na mtu kumpa mtu mwingine kadi yake na akaenda kuitumia.
 
Kuna totauti kati ya kuona na kuangalia
 
Sijaelewaa. Unataka kusema nini, ndugu?
 
Sijaelewaa. Unataka kusema nini, ndugu?
Mimi nilikuwa nambishia jamaa aliyesema kuwa NHIF, ikifa, basi itakuwa ni kiama, kwa watz na kudidimiza uchumi wa taifa, ndio nikasema, kuwa hao wanaochangia huo mfuko ni 8% ambao ni namba ndogo sana ukilinganisha na population yetu.Hivyo ni bora kwanza ikaja hiyo sera ya bima ya matibabu kwa wote, kapu litakuwa kubwa, hivyo itakuwa rahisi.
 
Naomba kifaham "population" unayoizungumzia wewe ni ipi? Maana tunaongelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya na Wanachama wake WALIOJISAJILI kwa huduma za mfuko huu.
 
Chapisho zuri kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…