Yafuatayo ni majina ya wanafunzi wa kidato

Msimamia Ukucha

Senior Member
Joined
Feb 11, 2013
Posts
146
Reaction score
42
TANGAZO
MKUU WA JKT MEJA JENERALI RAPHAEL MUHUGA ANAWAITA VIJANA 10,849 WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA MWAKA 2013 KUJIUNGA NA JKT KWA MUJIBU WA SHERIA KAMA IFUATAVYO:-

1. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOPATA DIVISION I NA DIVISION II.

2. VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA WALIOSOMA MASOMO YA MCHEPUO WA SAYANSI NA KUPATA DIVISION III.

3. VIJANA HAO WANATAKIWA KURIPOTI KATIKA MAKAMBI YA JKT TAREHE 24 JUNI 2013 BILA KUKOSA. AMBAYE HATARIPOTI ATACHUKULIWA HATUA ZA KISHERIA.

4. TANGAZO HILI HALIWAHUSU VIJANA WOTE WALIOHITIMU KIDATO CHA SITA 2013 KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA UNGUJA NA PEMBA. AIDHA, SHULE 27 AMBAZO VIJANA WAKE WAMEHITIMU MAFUNZO YA JKT AWAMU YA KWANZA HAZIHUSIKI.

5. VIJANA HAO WATUNZE TIKETI ZAO KWA AJILI YA KUREJESHEWA NAULI WATAKAZOTUMIA MARA TU WATAKAPORIPOTI VIKOSINI.

6. TAARIFA ZAIDI ZITATOLEWA KWENYE MAGAZETI MBALIMBALI YA HAPA NCHINI.

Zifuatazo ni selection za kambi walikopangiwa


Attached Files

 
Afadhali wapelekwa tu Jeshini wakajifunze nidham na uzalendo!!!safi sana!!!
 
Hao wazalendo waliopitia jkt ndo wanalipeleka taifa pabaya. Impact ya jkt ni ndogo sana imekaa kisiasa n kichaka cha walafi kupiga hela za tenda.
 
Mikwara tu ya Serikali, hata wasipoenda hakuna atua itakayochukuliwa na watu kama kawa wataenda chuo kikuu. Nani anabisha?
 
Kwani huko wanagawa smart phones na earphones? Tablets na macbook pro zitakuwepo huko? Na yale mambo yetu ya mlegezo na na vitop?Vipi zile style zetu za viduku na rasta,wanaruhusu?

Tehetehetehetehe... natania tu wakuu.Maana naona vijana huku mtaani wameishaanza kuzeeka hata kabla hajaingia hiyo depo.

Safiii sanaaa..
 
JKT Certificate itakuwa sehemu ya cheti kuambatanishwa wakati wa application za vyuo vikuu kwa fresh from school?
 
JKT Certificate itakuwa sehemu ya cheti kuambatanishwa wakati wa application za vyuo vikuu kwa fresh from school?
Aliyeturudishia JKT nampa hongera sana,anaona mbali na analitakia mema sana taifa letu,hivi unaelewa karibu ya asilimia 70 ya vijana awa wanaomaliza form 6 tangu wazaliwe hawajawahi kugusa jembe,hawajui jembe linashikwaje,mtu unalimaje,lini wakati wa kulima etc wengi wao hawajui hata kuku anahatamia mayai kwa siku ngapi,hawajui ng'ombe anabeba mimba siku ngapi,akiwa kwenye joto ana dalili gani,hawajui artificial insermination ni nini.Kusema kweli ni kizazi kilichokuwa kinaelekea pabaya sana.Watoto wa siku hizi hawaangalii hata tarifa za habari,hawajui current affairs,hawasomi magazeti,wakisoma ni ya udaku na michezo,muda wote wako kwenye BIG brother,na ndio maana sikushangaa wengi wao walipopata F kwenye somo la GS.Mfano swali moja la GS mwaka jana liliwataka wanafunzi waeleze challenges zilizojitokeza kwenye zoezi la Sensa na ushauri kwa Serikali.Sasa mwanafunzi alitegemea hata mambo kama hayo wafundishwe darasani?sio kila kitu unafundishwa darasani vingine unatafuta mwenyewe.
Nimeparticipate kwenye interview nyingi siku za karibuni,moja wapo ya kitu kilichonisikitisha sana kwa wahitimu wetu wa Kitanzania \kiulizwa swali lolote kuhusu current/global affairs ni watupu,atasema ilo sikufundishwa shule,hivi unategemea Mwalimu akufundishe kuwa Mandela yuko mahututi ?
Nafurahi kwani wengi wakitoka JKT usharobalo kwisha,watakuwa wanaona aibu kuvaa kata K na miwani ya Commedy,watajua the other side of life na kuacha kudanganyana mitaani,watjua kuwa ajira sio peke yake,wengi wtapenda ku practise kilimo na ufugaji waliojifunza JKT. Uoni wabunge waliotoka JKT japo ya wiki 2 wamepunguza kelele? Naomba JKT itiliwe msisitizo na watakaogoma kwenda wasiruhusiwe kujiunga na vyuo vya Tanzania,na hata wakikimbilia kusomea vyuo vya nje wakirudi wasipewe ajira serikalini hadi waonyeshe vyeti vya JKT,pia JKT miezi mitatu ni michache sana,angalau iwe miezi 8 ili watoke wameiva barabara
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…