Yajue maandiko 5 katika Biblia yanayoeleza kuhusu hatari ya kupenda Fedha na mali

Yajue maandiko 5 katika Biblia yanayoeleza kuhusu hatari ya kupenda Fedha na mali

Samweli Mwangosi

New Member
Joined
Jan 15, 2025
Posts
1
Reaction score
0
Maandiko yafuatayo yanaonyesha wazi kwamba Biblia inatuhadharisha kuhusu hatari ya kupenda fedha na mali, ikisisitiza umuhimu wa kuweka kipaumbele kwa mambo ya kiroho na uhusiano wetu na Mungu badala ya kutegemea mali za kidunia.

01. 1 Timotheo 6:10 "Maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi."

02. Mathayo 6:24 "Hakuna mtu awezaye kutumikia mabwana wawili; kwa maana atamchukia huyu, na kumpenda huyu; ama atashikamana na huyu, na kumdharau huyu. Hamwezi kumtumikia Mungu na mali."

03. Waebrania 13:5 "Msiwe na tabia ya kupenda fedha; mwe radhi na vitu mlivyo navyo; kwa kuwa yeye mwenyewe amesema, Sitakupungukia kabisa, wala sitakuacha kabisa."

04. Marko 10:23-25
"Yesu akatazama kotekote, akawaambia wanafunzi wake, Jinsi itakavyokuwa shida wenye mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Wanafunzi wakashangaa kwa maneno yake. Yesu akajibu tena, akawaambia, Watoto, jinsi ilivyo shida wenye kutegemea mali kuingia katika ufalme wa Mungu! Ni rahisi ngamia kupenya katika tundu ya sindano kuliko tajiri kuingia katika ufalme wa Mungu."
05. Luka 12:15 "Akawaambia, Angalieni, jilindeni na choyo, maana uzima wa mtu haumo katika wingi wa vitu vyake alivyo navyo."

ZINGATIA: si vibaya kuwa na mali ama fedha bali visiwe vyanzo vya kutuingiza jehanam.
 
Back
Top Bottom