Chakula safi na najisi
Kumbukumbu la torati 14
3 Usile kitu chochote kichukizacho. 4 Wanyama mtakaokula ni hawa ng'ombe, na kondoo, na mbuzi, 5kulungu, na paa, na kongoni, na mbuzi wa mwitu, na paa mweupe, na pofu, na mbuzi wa mlima; 6na kila mnyama aliyepasuliwa ukwato, ukapasuka ukwato wake zikawa mbili, naye ni mnyama mwenye kucheua akatafuna tena, katika wanyama wote, ndiye mnyama mtakayemla. 7Lakini, hawa msile katika wale wenye kucheua, na hao waliopasuliwa ukwato; ngamia, na sungura, na kwang'a, kwa kuwa hucheua, lakini hawakupasuliwa kwato, ni najisi kwenu; 8na nguruwe, kwa kuwa amepasuliwa ukwato lakini hacheui, huyu ni najisi kwenu msile nyama zao, wala mizoga yao msiiguse.
9Mtakula hawa katika wote walio majini; kila kilicho na mapezi na magamba mtakula; 10na kila kisichokuwa na mapezi na magamba msile; ni najisi kwenu.
11
Mna ruhusa kula katika ndege wote walio safi. 12 Lakini hawa msiwale; tai, na furukombe, na kipungu; 13na kengewa, na kozi, na mwewe kwa aina zake; 14 na kila kunguru kwa aina zake; 15na mbuni, na kirukanjia, na dudumizi, na kipanga kwa aina zake; 16na bundi, na mumbi, na bundi mkubwa; 17na mwari, na nderi, na mnandi; 18na membe, na koikoi, kwa aina zake; na hudihudi, na popo. 19Na wadudu wote watambaao wenye mabawa ni najisi kwenu; msiwale. 20Mna ruhusa kula katika ndege wote walio safi.
21 Msile nyamafu yoyote; waweza kumpa mgeni aliye ndani ya malango yako, ili apate kula; au kumliza mtu wa mataifa; kwa kuwa wewe u taifa takatifu kwa BWANA, Mungu wako. Usimtokose mwana-mbuzi katika maziwa ya mamaye.