Yajue magonjwa ya fangasi ya ngozi na matibabu yake

Yajue magonjwa ya fangasi ya ngozi na matibabu yake

Kurzweil

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
6,621
Reaction score
8,411
Fangasi ni magonjwa yanayoathiri ngozi, kucha na nywele, pia huathiri mdomoni na ukeni. Magonjwa haya huambukiza kwa njia ya kugusana ua kshirikiana nguo hasa za ndani na tauro.

Hapa tutaangalia fangasi katika kundi la magonjwa yanayoathiri ngozi, nywele na kucha (dermatomycosis).

Kuna aina kuu 5 za magonjwa ya fangasi wa ngozi, nywele na kucha kama ifuatavyo;

Fangasi wa kichwani, ugonjwa huu huanza na sehemu ndogo ya ngozi ya kichwa na kukua kuwa sehemu kubwa. Huathiri nywele na kuzifanya dhaifu, laini na nyepesi kukatika au kung'oka. Huwaathiri sana watoti chini ya miaka 10 na hupotea mtu akisha barehe. Matibabu take ni griseofulvin na fluconazole, dozi zake huanzia siku 6-14.

download.jpg


Fangasi wa mwili, ugonjwa huu hutokea mwilini, sehemu ya ngozi iliyoathiriwa huwa nyekundu, duara kama shiringi na kukua huku ikiacha sehemu ya katikati kuwa na ngozi nzuri. Maduara haya yanaweza kukaa yakiwa kadhaa katika sehemu moja ya ngozi. Dawa nzuri kutumia ni za kupaka zinazokuwa katika tyubu, cotrimazole au ketoconazole. Kwa ugonjwa uliokua sana na kwa wagonjwa wenye kinga ya mwili ndogo kama wenye VVU, nivema wakatumia dawa ya kunywa

tmp-cam-264180180.jpg


tmp-cam--1225780016.jpg



Fangasi wa nyayo na vidole, ugonjwa huu hutokea kama mabaka na kuchanika katikati ya vidole na huwacha sana na kuuma pia. Matibabu yake maranyingi huwa dawa ya kupaka kwa wiki 4, kwa ugonjwa uliokua sana tumia dawa ya kunywa kama griseofulvin kwa wiki 6-12.

Screenshot_20170504-012252-1.jpg


Fangasi wa kucha, ugonjwa huu huathiri kucha na hubadilisha rangi ya kucha. Huzalishwa vitu kama chaki na ambavyo vikisuguliwa huweza kupukutika. Kucha huweza kulika na inaweza kuisha. Ili kutibu ugonjwa huu nibora kutumia dawa za kunjwa na terbinafine na itraconazole zimeonekana dawa bora zaidi.

images-2.jpg


Pityriasis, huu ni ugonjwa wa fangasi ambao huathiri sehemu ya huu sana ya ngozi katika sehemu za usoni, shingoni na mgongoni. Hutokea kama viduara vyenye mng'ao vinavyo washa. Huongezeka na huathiri sehemu kubwa ya ngozi visipotibiwa ingwa vinaweza kupotea vyenyewe. Maranyingi ugonjwa huu hauambukizwi Ila hutokea kama ajari tu yaapotikea mabadiliko fulani ya mwili. Sio ugonjwa hari sana kiafya ila haukubaliki kwani huharibu mwonekano wa mtu has a unapotokea maeneo ya uso na shingoni. Matibabu yake ni sawa na yale ya fangasi wa mwili.

Screenshot_20170504-012331-1.jpg
 
Mkuu hata kuweka onyo hujaweka! hizo picha ni mbaya sana zinahitaji utayari kuzitazama.

Kuna watu wanaperuzi JF wanakula au kunywa kuna watu wakiona picha za kinyaa kama hizi huweza hata kutapika weka Tahadhari kwanza
 
Mkuu nina fungus ya kichwa cha dushelele, huwa natumia epiderm huisha ila badae unarudi unarudi tena. Nini suruhisho lake kama fungus zingine ulizotaja?
 
Back
Top Bottom