Yajue mambo 14 ya busara

Yajue mambo 14 ya busara

RIGHT MARKER

Senior Member
Joined
Apr 30, 2018
Posts
129
Reaction score
473
Mhadhara - 44:
Mnamo Oktoba 1, 2024 niliwaletea MAMBO 13 YA BUSARA. Leo nawaongezea mambo mengine kumi na nne (14) ya busara ambayo yataongeza au yatalinda heshima, thamani na utu wako. Ikumbukwe kuwa watu pia ni mtaji wa kujipata kimaisha.

MAMBO 14 YA BUSARA:
1.
Acha tabia ya kucheuwa ovyo wakati unapokuwa unakula na wenzako. Utasababisha wenzako wapatwe na kinyaa.

2. Usipenge makamasi au kukohoa ovyo na kutema makohozi wakati unapokula na wenzako. Unaweza kusababisha wenzako wapatwe na kinyaa.

3. Punguza kuongea sana (Ikiwezekana usiongee) wakati ukiwa unatafuna chakula pindi unapokula na wenzako. Wengine watakapokutazama mdomoni hupatwa na kinyaa.

4. Kama upo kwenye mkusanyiko wa watu hasa kwenye utulivu (mfano kwenye Bus, msibani, darasani, nyumba ya ibada, n.k) usipende kusinzia ovyo. Kama una usingizi jikaze kwa sababu unaweza kujamba kwa nguvu mwishowe upatwe na aibu.

5. Unapokuwa kwenye malumbano na mwanandoa mwenzako epuka kutamka maneno ya kumtambia mwenzako dhidi ya watu wengine - Kwa mfano: (ME) "Wanawake warembo kukuzidi wewe wanaonitaka wapo wengi"/- (KE) "Wapo wanaume wenzako wenye pesa wananitaka kila siku" - Usisahau kuwa unapendwa kwa sababu upo kwenye ndoa.

6. Kama hakuna ulazima wa kusogeza kinywa chako karibu na uso wa mwenzako pindi mnapozungumza basi usifanye hivyo. Mara nyingi haileti sana furaha na uhuru kwa mtu mwingine.

7. Ukipewa fursa ya kutazama kitu (picha, video, memes, n.k) kwenye simu ya mwenzako, baada ya kumaliza epuka kutazama/kupekua/kutafuta vitu vingine ambavyo hakukuruhusu.

8. Usimtext SMS ya ghafla ya mapenzi au yenye kiashiria cha mapenzi mtu ambaye mpo kwenye mazoea ya kikazi au urafiki wa kawaida; unaweza kuharibu au kushusha heshima yako kwake. Kama umevutiwa nae mpe appointment, au muandae taratibu kwa hizo SMS. Usisahau si kila anayekuzoea sana anahitaji kufanya mapenzi na wewe.

9. Kama unaishi kwenye nyumba ya kupanga au mtaa wenye nyumba zilizobanana - halafu shughuli zako ni za kuamka asubuhi (alfajiri) sana, jaribu kuepuka kufanya mambo yafuatayo;
✓ Usifungulie redio/TV kwa sauti ya juu.
✓ Usiwe na tabia ya kuswaka nje kwa fujo na kukohoa kwa nguvu huku unatema makohozi kwa sauti ya juu.

10. MWANAUME: Epuka kukaa tumbo wazi kwa watu au eneo ambalo si mtindo wao wa maisha. Jifunze kuishi na mazingira - Kwa mfano umetoka mikoa yenye joto ambayo watu wanakaa tumbo wazi kwa sababu ya joto, na sasa umekwenda mikoa ambayo haina joto au mikoa ambayo hawana mtindo huo wa maisha.

11. Kama umezoea kula kwa mkono vyakula ambavyo wengi hula kwa kutumia kijiko kama vile wali, makande, maharage, n.k - Kuna mazingira ambayo ukitumia mkono utawafanya watu wengine wahisi kinyaa; hivyo kama watu hao ndio wafadhili wako huko ulikokwenda, jaribu kuomba ruhusa yao au ishi kulingana na mazingira ili mambo yako yaende.

12. Usitumie hela ya mtu bila ruhusa yake hasa ukijiona huna uwezo wa kuilipa, utashusha heshima yako au kuvunja kabisa urafiki wenu.

13. Kama una urafiki na watu waliokuzidi uwezo wa kifedha, madaraka, au umaarufu; watumie kwa ajili ya kufungua milango yako (connection) ya maisha. Epuka kuwa omba omba wa vihela vidogo vidogo vya kununua wali nyama. Jukumu la kujilisha chakula ni la kwako. Na kama utakuwa unawaomba hela ya kula ukinyimwa usichukie na wala usitoe maneno ya kashfa kama vile;- "Bosi mkubwa kama wewe unaninyima elfu kumi" - "Bosi roho mbaya haijengi" - "Bosi kutoa ni moyo si utajiri" --- Hakika hayo maneno na tabia yako ya omba omba itakupotezea watu muhimu sana. Mara nyingi watu waliofanikiwa kimaisha hupenda kuambatana na watu wenye kufanana mawazo (fikra) ya kufanikiwa, hivyo ficha njaa zako ili uchote fikra zao.

14. Epuka kuzunguka mtaani na kanda mbili (malapa) hata kama unakwenda safari fupi kama vile dukani, n.k - Hii ni kwasababu malapa yameshakaririwa kuwa ni kifaa kinachotumika chooni, hivyo utashusha heshima na thamani yako.​

UNAWEZA KUONGEZA MAMBO MENGINE YA BUSARA KWENYE COMMENTS....

Right Marker
Dar es salaam
 
😂😂
Kama upo kwenye mkusanyiko wa watu hasa kwenye utulivu (mfano kwenye Bus, msibani, darasani, nyumba ya ibada, n.k) usipende kusinzia ovyo. Kama una usingizi jikaze kwa sababu unaweza kujamba kwa nguvu mwishowe upatwe na aibu
 
Back
Top Bottom