SoC04 Yakifanyika haya lazima Tanzania tuitakayo itakuwa na maendeleo makubwa

SoC04 Yakifanyika haya lazima Tanzania tuitakayo itakuwa na maendeleo makubwa

Tanzania Tuitakayo competition threads

Berick Lucas

New Member
Joined
May 31, 2024
Posts
1
Reaction score
0
UTANGULIZI

Kwanza ninamshukuru Bwana Mungu na kuniwezesha, kunipa Afya njema. Pia nashukuru Jamii zote za hapa Tanzania kwa Sekta zote za Kijamii na ninatoa shukrani katika Uongozi uliopo katika Nchi yetu Tanzania kuanzia kwa Rais hadi Wajumbe wa Nyumba kumi au zaidi.

Basi katika Jamii Forum , nitazungumzia kuhusu Elimu Jamii, Afya Jamii, Sekta za Umma pamoja na Sekta Binafsi katika Jamii

Elimu Jamii katika Ujamaa

Elimu Jamii ni ile hali ya Watu flani katika kuelimishana kikamilifu katika Jamii husika kwaajili ya Ujamaa ili kitu walichokipanga kifanyike katika upendo wa kushirikishana. Kwahiyo kwa kutaka haya yote ndani ya Tanzania Tuitakayo, lazima kushirikishana Kijamii ambapo kutapelekea ndani ya Miaka 5 mpaka 25 kufanikisha hilo kwa njia ya Upendo.

Afya ya Jamii

afya ya Jamii ni ile hali ya Watu wanao zunguka Mazingira flani kwaajili ya Kiafya.

Kwa hiyo tukiboresha Afya bora kwa kila Jamii, katika Mazingira yote yanayozunguka Nchi yetu Tanzania hakika kutakuwa na Afya katika Jamii zote kwa maana katika Rasilimali Watu ni lazima tuwe na Afya iliyo njema kwasababu Maendeleo ya Nchi yanatakiwa katika Jamii yenye Afya njema ambayo sio hafifu, kwahiyo inatakiwa Jamii zote ziwe zenye Afya njema. Pia Rasilimali Watu inatakiwa Jamii yote iwe na Afya njema kwa kila namna yoyote ili Tanzania tuitakayo ndani ya Miaka 5 mpaka 25 inatakiwa Jamii yote iwe na Afya njema kwa ajili ya Maendeleo inatakiwa kuboresha Afya iwe nzuri katika Jamii zote.

Sekta Binafsi katika Jamii

Sekta Binafsi katika Jamii ni ile hali kuwa na ukaribu na Watu katika Ujamaa au Umoja katika kufanya kazi za Maendeleo katika Jamii. Hii inahitaji kuwa karibu na Jamii inayozunguka kwaajili ya Maendeleo ya Kijamii katika Ujamaa na ushikamano wa Upendo pamoja na kuelekezana katika utaratibu wa kufanya kazi kwa nia moja.

Pia kunahitajika kuwa na kusikilizana na Watu walioko katika Sekta husika kwenye Jamii hiyo kwa usikivu wa kuelekezana katika hekima ya Uongozi, Maarifa na Busara ya Kijamii katika Ujamaa huo kwa kufanya kazi kwa weledi wa Uongozi, kwakufanya hivyo ndani ya Miaka 5 mapaka 25 tutafikia Tanzania tuitakayo

Sekta za Umma katika Jamii za Ujamaa

Sekta za Umma ni ile hali ya kuwa na umoja katika Jamii za Ujamaa kwaajili ya kufanya vitu vya Maendeleo ya Kijamii kwa kushirikishana baina ya Wananchi na Jamii pamoja na viongozi wanaotawala katika Jamii zote.

Kwa ushauri wangu kwa Sekta za Umma ningependa kushauri kuwa tutumie Rasilimali zetu ambazo Mungu ametupatia katika Nchi yetu ya Tanzania, pia tutumie Rasilimali Watu kwa ajili ya kufanya kazi ya uchimbaji wa Rasilimali za Nchi kwa kuwaelekeza namna ya uchimbaji kwa mfano, tukitumia fursa za Madini yetu ya Tanzanite, Makaa ya Mawe pamoja na Madini mbalimbali yaliyomo Tanzania, kwakufanya hivyo hakika hata Miaka 5 mpaka 25 haiwezi kufika. Pia tukiweka imani na kuwaamini Rasilimali Watu wetu, Tanzania tuitakayo kwa Miaka 5 mpaka 25 basi tutafanikisha na kufanikiwa katika Maendeleo ya Nchi yetu Tanzania.

Mbali na hayo yote lakini pia tukitumia Maziwa, Mito na Bahari kwaajili ya uvuvi pamoja na uvunaji wa Samaki kuanzia dagaa hadi Samaki na upande wa Bandari kwa kuweka wasimamizi walio katika Rasilimali Watu wetu kwaajili ya Maendeleo ya Nchi yetu ndani ya Miaka 5 mpaka 25 hakika Tanzania tuitakayo itakuwa safi sana.

Kwa kutumia Rasilimali Watu katiak Jamii ya Kijamaa kwa kushirikishana katika Jamii zote kwa njia ya Hekima, Busara, Maarifa, Ufahamu na Umoja kwa ajili ya kuelekezana, kuonyana pamoja na kufundishana. Kwahiyo hayo yote yanahitaji kuwa na Neema ya Upendo katika Utawala wa Nchi yetu Tanzania ndani ya Mika 5 mpaka 25 tutafanikisha hakika.

Tupende kuwa na tabia ya kushirikishana katika Jamii za Ujamaa kwaajili ya Utawala wenye Maendeleo katika Jamii zote za Nchi yetu Tanzania kwaajili ya manufaa ya Jamii zote zilizopo hapa Nchini.

HITIMISHO

Hakika hayo yote tukiyatumia na kuyafanya mambo yote ni lazima Tanzania tuitakayo ndani ya Miaka 5 mpaka 25 itakuwa na Maendeleo makubwa sana.

Pia tumtangulize Mungu Mwenyezi kwa sababu yeye ndiye chanzo cha Nchi yetu Tanzania.
kwahiyo kwakuyazingatia hayo yote na kuyafuata kwa kumtanguliza Mungu mbele ni dhahiri kabisa tutafikia mahali ambapo Tanzania tuitakayo itakuwa kwa namna ambayo tunaitarajia iwe.

Asanteni sana Wapendwa

Wenu

Berick Lucas Hulilo

Amina
 
Upvote 2
Back
Top Bottom