Yakubu: Ukaguzi wa AFCON umeenda vyema

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo Bw Saidi Yakubu amesema timu ya Wakaguzi kutoka Shirikisho la Mpira wa Miguu Barani Afrika (CAF) kwa maandalizi ya AFCON 2027 imemaliza ukaguzi wao vyema katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda kupitia kapeni ya EA Pamoja Bid.

Akiongea katika Kipindi cha Jambo kinachorushwa ya Shirika la Utangazaji la Tanzania (TBC) Agosti 5, 2023 jijini Dar es salaam, Katibu Mkuu Bw Yakubu amesema timu hiyo imemaliza kazi yao vizuri hapa ambapo ukaguzi wao ulianzia nchini Kenya, Uganda na Tanzania na kuhitimisha kazi yao kikao cha majumuisho kilichofanyika Zanzibar.

Maeneo mengine waliyokagua ni pamoja na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, HospitaIi ya Taifa Muhimbili, Uwanja wa Amaan Zanzibar, Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Hospitali ya Mnazi Moja, Uwanja wa uwanja wa Mao Tse Tung Zanzibar pamoja na hoteli zitakazotumiwa wakati wa mashindano hayo kulingana na viwango vya CAF.

“Baada ya ziara yao hiyo Kenya, Uganda na Tanzania, walifanya mkutano wa majumuisho, Hatupo vibaya, tupo vizuri. Kinachotazamwa na wakaguzi ni pamoja na utayari wa Serikali namna ilivyojipanga katika kuhakikisha tukio hili tumelipokea, ukweli ni kwamba ziara yote hii ilikuwa inaongozwa Katibu Mkuu tayari inaonesha kwamba Serikali ipo tayari” amesema Katibu Mkuu Bw Yakubu.

Vigezo zingine ambavyo wakaguzi hao wa AFCON waliangalia ni mtiririko wa matukio kuelekea AFCON, kwa maana ya miundombinu ni lazima yote ikamilike kabla ya tarehe 31 Desemba 2025, Tanzania inajenga kiwanja kipya cha Arusha ambapo walioneshwa michoro, nyaraka zote muhimu na mapango wa mtiririko wa fedha utakavyokuwa katika kukamilisha ujenzi wa uwanja huo.
 
Hii nchi inafurahisha sana. Yaani wanajenga uwanja Arusha ambako tayari kuna uwanja wa Sheikh Amri Abeid! Na ambao huo uwanja unahitaji tu maboresho!!

Kwa nini wasijenge Dodoma! Na tayari eneo lipo!! Maana ule uwanja ulioporwa na ccm wa Jamhuri una nafasi finyu, na hauwezi kutanuliwa.
 
Arusha sio wapenzi wa mpira wa miguu, kwa nini hicho kiwanja kisijengwe Mwanza au Mbeya au Dodoma makao makuu ?
Ufinyu wa maarifa ndugu zanguni. Tunafanya mambo bila kuzingatia tafiti.
 
Arusha ni Makao Makuu ya EA... Na AFCON itaandaliwa na nchi za EA.
Acha ujinga, kuwepo kwa jengo la ofisi za EA haihusiani na serikali ya Tz kujenga uwanja wa mpira mkoa au sehemu ambayo haina hata passion na hilo, Mbeya au Mwanza au Dodoma ndio huo uwanja ulitakiwa ujengwe, siasa za kibinafsi zinaendelea hapo, hamna kingine.
 
Define ujinga Kwanza, then rudia kusoma bandiko lako...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…